Waziri mwenye dhamana unayesimamia mawasiliano naomba utoe ufafanuzi kwa watanzania juu ya hili swala

5997

JF-Expert Member
Jan 19, 2019
514
1,204
Kuhusu kusajiri upya simcard kwa fingerprint,
Ndugu waziri usajili huu unatutaka tuwe na vitambulosho vya nida,
Ndugu waziri wengi wetu hatuna hivyo vitambulisho na wengine hata tu kujiandikisha hawakujiandikisha kutokana na sababu zilizokua nje ya uwezo wao,
Sasa mweshmiwa waziri naomba uitishe press uongee na watanzania,
Je ambao hatuna vitambulisho tufanyeje?
Na ambao hawajawai hata kujiandikisha tufanyeje?
Mh waziri huoni kwamba hili zoezi litakua gumu?
Je kwanini msingehakikisha kwanza angalau 60% ya watanzania wanavitambulosho ndipo muanze zoezi la usajili mpya?

Pia angalia hii changamoto waziri
Nilijiandikisha na kupigwa picha Mwanza lakini tangu nimejiandikisha mpaka sasa sijapata kitambulisho na hivi sasa nimehamia morogolo kikazi, mh waziri unaiona hiyo changamoto lakini?

Mh waziri hivi hilo swala mlikaa mkajadili kweli halafu mkatoka na azimio hilo?
Mh waziri ASANTE
 
Wewe ata usiwe na wasi vitambulisho vya NIDA nadhani ni aslimia mbili ya watanzania ndo wanavyo wengine hatuna kula maisha wewe achana na upumbavu wao.
 
Wewe ata usiwe na wasi vitambulisho vya NIDA nadhani ni aslimia mbili ya watanzania ndo wanavyo wengine hatuna kula maisha wewe achana na upumbavu wao.
😂😂😂😂😂👏👏👏👏
 
hii serikali ya mwendokasi ukikaa kuifikiria kila wanachosema utawehuka bure! huenda wanapima upepo/ wanatest mitambo ili mwakani wazime line zote ambazo hazitakua zimesajiliwa ili kusiwepo na wasumbufu wa mitandaoni hadi uchaguzi upite. Kwa ujinga wa viongozi wa ccm anything i repeat anything is possible
 
Back
Top Bottom