Waziri mwenye dhamana kubwa anapowadanganya Wananchi mara kwa mara; Je ana akili TIMAMU???

mariavictima

Senior Member
Jul 8, 2010
179
39
Nanukuu gazeti la mwananchi la tarehe 15/9/2011:

"Septemba 3, mwaka huu, Waziri Nishati na Madini, William Ngeleja, aliwaeleza waandishi wa habari kuwa makali ya mgawo wa umeme yatapungua kwa kiasi kikubwa kuanzia Septemba 5, mwaka huu kutokana na uzalishaji wa megawati 235.7.

Ahadi hiyo ya Ngeleja si ya kwanza kwani mapema mwaka huu akiapishwa baada ya kuteuliwa tena kushika wadhifa huo, aliutangazia umma kwamba mgawo wa umeme ungekuwa historia, lakini wiki moja baadaye nchi ilitikiswa na mgawo mkubwa.Lakini pia, hata baada ya kutoa ahadi ya Septemba 3, badala ya mgao kupungua kama alivyoahidi, makali ya umeme yalionekana kuongezeka katika maeneo mengi ya nchi.

Ngeleja aliwaeleza waandishi wa habari kuwa, megawati 235.7 zitazalishwa katika mitambo ya Jacobsen, Symbion na Aggreko iliyopo Ubungo, Dar es Salaam, huku akisisitiza kwamba mpaka kufikia Desemba, mwaka huu kutakuwa na uzalishaji wa megawati 572 ambazo zitamaliza kabisa tatizo la umeme."
 
Back
Top Bottom