Waziri mwenye dhamana fuatilia NIDA wamalizie mchakato wa kugawa vitambulisho vya taifa

gimmy's

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
3,056
2,000
Zipo taasisi za serikali ni kero sana hapa nchini,huwa hazifanyi kazi mpaka zisukumwe,

Wapo watanzania kwa mamilioni tumepewa no za NIDA pale awali lakini kupatiwa vitambulisho sasa ni zaidi ya miaka miwili hakuna kitambulisho wala taarifa kutoka NIDA kwamba ni lini tutasambaziwa vitambulisho hivi.

Ni vema mamlaka husika zikamalizia huu mchakato kwani sio busara watu kutoka vijijini kujazana kwenye ofisi za NIDA kufuatilia vitambulisho.

Kuna vijiji vilipo ni mbali ni gharama kusafiri kwenda ofisi za nida.

Ni busara vitambulisho vikagawawiwa kama ilivyofanyika awali watu walivipata vitambulisho ofisi za kata.

Kuwaacha watanzania na namba za NIDA pasipo kuwapatia vitambulisho kunasababisha usumbufu mkubwa kwa raia kwani hivi vitambulisho vinahitajika kila pahala.

Tafadhali wahusika fuatilieni hili.
Asante
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom