Waziri Mwandosya: Kikwete Angeniacha Nipumzike

Mleta thread inabidi aweke source. Otherwise ni majungu tu. Haiingii akilini kwamba Prof Mwandosya hakujua uteuzi wake. Lazima alifahamishwa kabla. Kama alikubali na wakati hawezi kufanya kazi, hiyo ndo tamaa ya fedha na madaraka sasa. Kwenye uwaziri kuna Chenji ya kumwaga ndo maana hakukataa.

Bongo kila kitu kinawezekana. Kwa vile tangu tuzaliwe hatujawahi sikia kuna mtu kakataa uteuzi na CCM ndiyo zao hizo. Inawezekana kabisa JK akawateua bila kuwataarifu (existing ones) maana akili yao ni maslahi na ulaji zaidi kazi na uwajibikaji.
 
Jaribu kuwa unafikiria kutumia kichwa chako usiongee kama kama Mtu mjinga usielewa tatizo la Tanzania, tatizo hapa CCM na mfumo zee ambao umeoza na haufai,unategemea hao wasomi wao watafanya nini? ulishaambiwa CCM inawenyewe mbona watu wengine mnakuwa wagumu kufikili! hata umweke nani ndani ya serikali ya CCM utaishia kutukana na maneno ya Kejeli,angalia sasa mnataka kufanya JF kama Genge la majungu na maneno ya hovyo! mmekalia kumshambulia Mwandosya na mtu mwenyewe mgonjwa haya sasa yeye ndiyo amifikisha Tanzania hapa ilipo katika miaka hamsini? yeye ndiyo angeleta Maji? hebu shirikisha Ubongo wako kufikiri vizuri. CCM ndiyo tatizo kama hujui akina Nundu wasomi wazuri na ozoefu wa kimataifa wenyekushimika wameishia kufedheheka na Mfumo wa hovyo ambao mnaupigia kura kila uchaguzi na kuishia kulalama kwenye keyboard huku hamchukui maamuzi yeyote ya maana.

Watanzania tukiendelea na maneno bila vitendo tutaona cha mtema kuni,mtapiga kelele wenzenu wataendela kuiba na sisi tutabaki kutukana tu kwenye keyboard! UFINYU WA MAWAZO
wewe ndio unatakiwa kutumia kichwa kufikiria badala ya mikono yako yeye kwa mfano yeye alikuwa na ngo yake kuhusu renewable energy, je ametumia fursa hiyo hata kuwekeza umeme wa namna hiyo kijijini kwake, kwa wapiga kura wake? au hiyo inahitaji kibali cha sereikali kuu? mufilisi ya ccm? wewe ukiweka renewable energy kwenye nyumba yako utakatazwa? au ukiwaelimisha majirani zako juu ya hilo mkafanya mradi huo?
 
mchango wa mtu mwenye busara na hekima au mchapakazi mara nyingi huwa unahitajika siku zote, nadhani kikwete kwa kuzingatia uzoefu wa Profesa mwandosya uchapakazi wake na hata hekima zake ameona bado anamuhitaji sana katika baraza lake la mawaziri. kumpa uwaziri usio na wizara ni kumpunguzia majukumu pia kwani hatokuwa bounded na kazi flani flani na nadhani kazi yake kubwa ni kuangalia mahala palipo na mapungufu katika wizara mbali mbali na kutoa mchango wake.

hebu tuangalie enzi zile MREMA akipewa unaibu waziri mkuu chao ambacho hakipo kwenye katiba yatu but kutokana na uchapakazi wake na umuhimu wake Mwinyi aliona mtu huyu anahitajika kupewa nafasi ambayo itamfanya aweze kuingia katika wizara zingine na kutoa mchango wake pia

pia sitaki kuamini kuwa Mwandosya hakupewa taarifa awali, maana nachokifahamu kabla ya kutangazwa lazima muhusika (hasa wale katika nafasi muhimu na nzito), aelezwe kisha atoe maoni na akubali. So nahisi ili nalo limekuzwa tuu.

HOJA SAHIHI

NZITO

INAELEWEKA

INAKUBALIKA

YOU ARE A GREAT THINKER

BIG UP

WATU WAMEKALIA KUSIGINA TU, NA KUGEUZA GEUZA

MWANDOSYA HAWEZI KUSEMA MANENO HAYO KWA UTEUZI WA MKUU WA NCHI

ASANTENi
 
Waziri mpya wa Ofisi ya Rais(Asiye na Wizara Maalum),Prof.Mark Mwandosya amekaririwa akisema kuwa kama Mhe.Rais angezingatia hali yake ya kiafya na ushauri aliopewa na Madaktari juu ya kupata mapumziko,angemuacha apumzike.Akizungumza na Waziri Mkuu,Mizengo Pinda,jana nyumbani kwake Kunduchi-Dar es Salaam,Prof Mwandosya alionyesha kutoridhishwa kwake na uteuzi wa Rais juu yake.

'Nahitaji mapumziko makubwa Mkuu' alisema Prof.Mwandosya akimueleza Pinda aliyeonekana kukubaliana naye. 'Niheri nirudi UDSM nikafundishe Wahandisi wangu' aliongeza Prof Mwandosya.Mimi tu kuwaletea habari...
Kwa wasomaji wa gazeti la mwananchi la leo, picha iliyopo front page kwakweli prof anaumwa! Bila kusoma maelezo ya picha yenyewe huwezi kuamini kama kweli ni prof. Jk please mpumzishe achana na bifu zenu za zamani.
 
Mkuu unazijua siasa za Mbeya? Ili CCM iendelee kuishi lazima huyo mtu aitwe waziri.

Yaani wanasiasa bana hawaaminiki kabisa. Ni unafiki kwa kwenda mbele!

Kama kweli anataka apumzike kulikuwa na ugumu gani kwa yeye kuomba kujiuzuru hata kabla ya mabadiliko yaliyofanywa karibuni? Na hata baada ya kujua kuwa Rais anafanya mabadiliko angeweza pia kumpigia simu Rais na kuomba apumzishwe! Nakumbuka vema tu kina Kingunge waliwahi kuomba kupumzika kipindi kile baada ya baraza la EL kuanguka.

Hata hivyo nampa pole Mh Mwandosya na namuombea apone kwa haraka.
 
Kwani ni lazima kukubali posti?

Si ndo hapo.

Na hizi appointment rais anataja tu watu kwenye redio bila kukubaliana nao? Au anawashikia fimbo kwamba msipokubali nitawachapa?
 
Pole sana Prof kwa kuchelewa kugundua unafiki wa bosi wako na mtandao wake, now its too late, subili polonium ifanye kazi yake, mwisho wa siku.. "nenda mwalimu"... In short imekula kwako for miscalculation...
 
si aseme tu kuwa haridhishi na ka-wizara kasikokuwepo? Waziri hewa.....
 
Uvivu wa kufikiri, leo ndiyo unatambua kuwa inafaa ufundishe wahandisi UDSM? Hii ni baada ya kuugua au!? Acha unafiki porof!
 
wewe ndio unatakiwa kutumia kichwa kufikiria badala ya mikono yako yeye kwa mfano yeye alikuwa na ngo yake kuhusu renewable energy, je ametumia fursa hiyo hata kuwekeza umeme wa namna hiyo kijijini kwake, kwa wapiga kura wake? au hiyo inahitaji kibali cha sereikali kuu? mufilisi ya ccm? wewe ukiweka renewable energy kwenye nyumba yako utakatazwa? au ukiwaelimisha majirani zako juu ya hilo mkafanya mradi huo?

Upumbavu
 
Waziri mpya wa Ofisi ya Rais(Asiye na Wizara Maalum),Prof.Mark Mwandosya amekaririwa akisema kuwa kama Mhe.Rais angezingatia hali yake ya kiafya na ushauri aliopewa na Madaktari juu ya kupata mapumziko,angemuacha apumzike.Akizungumza na Waziri Mkuu,Mizengo Pinda,jana nyumbani kwake Kunduchi-Dar es Salaam,Prof Mwandosya alionyesha kutoridhishwa kwake na uteuzi wa Rais juu yake.

'Nahitaji mapumziko makubwa Mkuu' alisema Prof.Mwandosya akimueleza Pinda aliyeonekana kukubaliana naye. 'Niheri nirudi UDSM nikafundishe Wahandisi wangu' aliongeza Prof Mwandosya.Mimi tu kuwaletea habari...

Hivi angetaa uteuzi angelazimishwa? Naomba kuelimishwa.
 
Ukisikia unafki ndio huu anatuletea Mwandosya, ni kwa nini asimuandikie barua Rais au kwenda Ikulu kumueleza Rais kwamba anashukuru kwa uteuzi wake lakini afya yake haimruhusu kufanya kazi hiyo!!??
Nadhani hakuapa hivyo ilikuwa signal kwa Mkuu wa kaya kuwa hataki post hiyo
 
Waziri mpya wa Ofisi ya Rais(Asiye na Wizara Maalum),Prof.Mark Mwandosya amekaririwa akisema kuwa kama Mhe.Rais angezingatia hali yake ya kiafya na ushauri aliopewa na Madaktari juu ya kupata mapumziko,angemuacha apumzike.Akizungumza na Waziri Mkuu,Mizengo Pinda,jana nyumbani kwake Kunduchi-Dar es Salaam,Prof Mwandosya alionyesha kutoridhishwa kwake na uteuzi wa Rais juu yake.

'Nahitaji mapumziko makubwa Mkuu' alisema Prof.Mwandosya akimueleza Pinda aliyeonekana kukubaliana naye. 'Niheri nirudi UDSM nikafundishe Wahandisi wangu' aliongeza Prof Mwandosya.Mimi tu kuwaletea habari...

Kwani huou waziri aliopewa si mapunziko tu ya kusoma magazeti na ...... kupata matibabu class A.mwndosya Hajachaguliwa uwaziri afanye kazi

Alafu anasema ni heri afudishe UDSM!!!!!!!!!!. Hivi kazi gani inahitji energy akili zaidi kati ya siasa na kufundisha ?
 
Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom