Waziri Mwandosya: Kikwete Angeniacha Nipumzike

BTW hii Wizara isiyokuwa na kaazi maalum, inafanya kazi gani... Hii si kula hela za wavimba macho bila sababu?? Where else in this world unapata cheo cha hivi??/ NAKULILIA TANZANIA......
 
Waziri mpya wa Ofisi ya Rais(Asiye na Wizara Maalum),Prof.Mark Mwandosya amekaririwa akisema kuwa kama Mhe.Rais angezingatia hali yake ya kiafya na ushauri aliopewa na Madaktari juu ya kupata mapumziko,angemuacha apumzike.Akizungumza na Waziri Mkuu,Mizengo Pinda,jana nyumbani kwake Kunduchi-Dar es Salaam,Prof Mwandosya alionyesha kutoridhishwa kwake na uteuzi wa Rais juu yake.

'Nahitaji mapumziko makubwa Mkuu' alisema Prof.Mwandosya akimueleza Pinda aliyeonekana kukubaliana naye. 'Niheri nirudi UDSM nikafundishe Wahandisi wangu' aliongeza Prof Mwandosya.Mimi tu kuwaletea habari...
Bwana/Bibi aliyetoa taarifa hii ulipataje wakati Prof na WM walikaa peke yao kuzungumza???? Kwanini watu mnapenda kusema uongo kila wakati???
Ungekanusha au huseme kama WM alikueleza hivyo kwasababu Prof hujaongea nae.
 
mchango wa mtu mwenye busara na hekima au mchapakazi mara nyingi huwa unahitajika siku zote, nadhani kikwete kwa kuzingatia uzoefu wa Profesa mwandosya uchapakazi wake na hata hekima zake ameona bado anamuhitaji sana katika baraza lake la mawaziri. kumpa uwaziri usio na wizara ni kumpunguzia majukumu pia kwani hatokuwa bounded na kazi flani flani na nadhani kazi yake kubwa ni kuangalia mahala palipo na mapungufu katika wizara mbali mbali na kutoa mchango wake.

hebu tuangalie enzi zile MREMA akipewa unaibu waziri mkuu chao ambacho hakipo kwenye katiba yatu but kutokana na uchapakazi wake na umuhimu wake Mwinyi aliona mtu huyu anahitajika kupewa nafasi ambayo itamfanya aweze kuingia katika wizara zingine na kutoa mchango wake pia

pia sitaki kuamini kuwa Mwandosya hakupewa taarifa awali, maana nachokifahamu kabla ya kutangazwa lazima muhusika (hasa wale katika nafasi muhimu na nzito), aelezwe kisha atoe maoni na akubali. So nahisi ili nalo limekuzwa tuu.

Unajaribu kusema ili Rais aombe ushauri kwa raia yeyote ni lazima huyo raia awe na cheo cha Uwaziri?
 
Mleta thread inabidi aweke source. Otherwise ni majungu tu. Haiingii akilini kwamba Prof Mwandosya hakujua uteuzi wake. Lazima alifahamishwa kabla. Kama alikubali na wakati hawezi kufanya kazi, hiyo ndo tamaa ya fedha na madaraka sasa. Kwenye uwaziri kuna Chenji ya kumwaga ndo maana hakukataa.
Mleta thread hii ni muongo muongo muongo. Hakuna mtu aliyesikiliza mazungumzo ya WM na Mwandosya, wote tulikua nje labda kama ni WM aliye post hii taarifa!!!:mad:
 
In this case, Pro. Mwandosya was (and is still) free to resign! On medical grounds
 
Waziri mpya wa Ofisi ya Rais(Asiye na Wizara Maalum),Prof.Mark Mwandosya amekaririwa akisema kuwa kama Mhe.Rais angezingatia hali yake ya kiafya na ushauri aliopewa na Madaktari juu ya kupata mapumziko,angemuacha apumzike.Akizungumza na Waziri Mkuu,Mizengo Pinda,jana nyumbani kwake Kunduchi-Dar es Salaam,Prof Mwandosya alionyesha kutoridhishwa kwake na uteuzi wa Rais juu yake.

'Nahitaji mapumziko makubwa Mkuu' alisema Prof.Mwandosya akimueleza Pinda aliyeonekana kukubaliana naye. 'Niheri nirudi UDSM nikafundishe Wahandisi wangu' aliongeza Prof Mwandosya.Mimi tu kuwaletea habari...

Hii inaitwa nataka sitaki. Kwa mwaka mzima Wizara ya Maji ilikaa bila waziri na watu wa Rungwe hawakuwakilishwa ipasavyo bungeni. Kwa nini hukuonyesha nia ya kupumzika?
 
Ndio maana nasema habari hii imetoka Udaku street
 
Kama ni kweli,

Huo ujumbe si angempa rais kwamba yeye hataweza hayo majukumu,kwani rais amemlazimisha?
 
mchango wa mtu mwenye busara na hekima au mchapakazi mara nyingi huwa unahitajika siku zote, nadhani kikwete kwa kuzingatia uzoefu wa Profesa mwandosya uchapakazi wake na hata hekima zake ameona bado anamuhitaji sana katika baraza lake la mawaziri. kumpa uwaziri usio na wizara ni kumpunguzia majukumu pia kwani hatokuwa bounded na kazi flani flani na nadhani kazi yake kubwa ni kuangalia mahala palipo na mapungufu katika wizara mbali mbali na kutoa mchango wake.

hebu tuangalie enzi zile MREMA akipewa unaibu waziri mkuu chao ambacho hakipo kwenye katiba yatu but kutokana na uchapakazi wake na umuhimu wake Mwinyi aliona mtu huyu anahitajika kupewa nafasi ambayo itamfanya aweze kuingia katika wizara zingine na kutoa mchango wake pia

pia sitaki kuamini kuwa Mwandosya hakupewa taarifa awali, maana nachokifahamu kabla ya kutangazwa lazima muhusika (hasa wale katika nafasi muhimu na nzito), aelezwe kisha atoe maoni na akubali. So nahisi ili nalo limekuzwa tuu.

Rais anaweza kumtumia mtanzania yoyote ambae anaona anaweza kumsaidia bila kumpa uwaziri, jamaa ni mgonjwa sasa uwaziri wa nini, hiyo ni tabia ya JK kutaka kufurahisha mtu hata pale pasipotakiwa kufanya hivyo
 
Rais anapoteua kabla ya kutangaza mhusika anapewa taarifa ya uteuzi .....kwa vyovyote Mwandosya alikuwa na taarifa hizo na kukubali mpango wa Rais kumpa nafasi hiyo.

Mtoa mada hamtendei haki Mwandosya kwa kuusemea moyo wake
 
We VUTA - NKUVUTE Lini umepata shahada ya uzamivu katika uongo?
05_12_cu2q31.jpg
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiongozana na Waziri Mark Mwandosya (kulia) wakati alipomtembelea nyumbani kwake, Kunduchi jijini Dar es Salaam juzi kumjulia hali. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom