Waziri Mwandosya arejea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Mwandosya arejea

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Dec 2, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Dec 2, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  2nd December 2011  [​IMG]
  Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya,


  Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya, aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Apollo, nchini India, kwa takriban miezi minane, amerejea nchini, baada ya afya yake kuimarika.
  Habari zilizopatikana jijini Dar es Salaam zilizothibitishwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Gerson Lwenge, Profesa Mwandosya alirejea nchini juzi.
  Mwingine aliyethibitisha jana kurejea kwa waziri huyo mwandamizi, ni mkewe, Lucy Mwandosya. Hata hivyo, Mhandisi Lwenge, ambaye alizungumza na NIPASHE jana, alipotakiwa kueleza maendeleo ya afya ya Waziri Mwandosya, alijibu: “Sijamuona, ndio naenda.
  Ukinitafuta baadaye nitakwambia.”
  Awali, Mhandisi Lwenge, alipoulizwa kama Waziri Mwandosya amerejea nchini, alijibu: “Ndio amerudi” na alipotakiwa kueleza lini alirejea, alijibu: “Jana (juzi).”
  Baadaye, majira ya saa 11.05 jioni jana, NIPASHE ilimtafuta Profesa Mwandosya kwa simu yake ya mkononi, ambayo ilipokelewa na mkewe, Lucy.
  Baada ya mwandishi kujitambulisha na kueleza shida yake ya kutaka kuzungumza na Profesa Mwandosya, Lucy, alisema muda huo waziri asingeweza kuzungumza kwa vile alikuwa anapumzika.
  “(Waziri) anapumzika, hawezi kuongea na wewe,” alisema Lucy, ambaye aliongozana na Profesa Mwandosya katika safari hiyo ya matibabu.
  NIPASHE pia jana iliwasiliana na Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, ambaye alisema ofisi yake haina taarifa za kurejea nchini kwa Waziri Mwandosya.
  “Kama amerudi aje atuambie. Tunavyofahamu bado yuko India,” alisema Dk. Kashililah.
  Profesa Mwandosya alilazwa India kwa zaidi ya miezi minane kwa matibabu baada ya kufanyiwa upasuaji wa mgongo.
  Kutokana na kulazwa muda mrefu, alilazimika kuzungumzia hali yake kuwa ilikuwa inaendelea vizuri na kutaka Watanzania waendelee kumuombea.
  Alilazimika kusema hivyo baada ya kuzuka uvumi kuwa amefariki dunia na kuwashtua wengi.
  Pamoja kuelezea maendeleo ya afya yake, Profesa Mwandosya, alisema ameshtushwa na uvumi huo.
  Hata hivyo, baadhi ya viongozi waandamizi serikalini wamekuwa wakitoa taarifa mara kwa mara wakieleza kwamba afya ya Profesa Mwandosya ilikuwa ikiimarika.
  Kutokana na matatizo hayo, Profesa Mwandosya, alishindwa kuhudhuria mkutano wa Bunge la Bajeti mwaka huu.
  Hali hiyo ilisababisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira, kusoma kwa niaba yake Bajeti ya Wizara ya Maji kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012.
  Kurejea kwa Profesa Mwansosya kunaifanya idadi ya mawaziri wanaoendelea na matibabu nchini India kubakia wawili, ambao ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Cyril Chami.  CHANZO: NIPASHE


   
 2. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #2
  Dec 2, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,058
  Likes Received: 7,518
  Trophy Points: 280
  Kuhusu Cyril Chami naibu wake si alisema haumwi vile kama tunavyofikiri?
  Na akasma ni kuwa amejisikia vibaya tu hivo ameenda kuangalia afya?
  Inakuwaje mpaka sasa hajarudi? Au yupo kwenye foleni ya kumuona daktari na zamu yake haijafika?
   
 3. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #3
  Dec 2, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Tunamshukuru Mungu.............na kumwomba awajalie afya njema wote!
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Dec 2, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  hivi tatizo la chami ni lipi?
   
 5. Sita Sita

  Sita Sita JF-Expert Member

  #5
  Dec 2, 2011
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 1,196
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mi niliambiwa ana matatizo ya mgongo.

  Am Happy he's back and wish him all the best in his recovery
   
 6. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #6
  Dec 2, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Mkuu mbona alirudi zaidi ya masaa 72 yalopita, na ilishatangazwa sana
   
 7. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #7
  Dec 3, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,058
  Likes Received: 7,518
  Trophy Points: 280
  Tuliambiwa haumwi bali hajisikii vizuri.
   
Loading...