Waziri (Mwanayanga) Innocent Bashungwa toa kauli ya mwisho ya Serikali je, Dar es Salaam "Derby' ya tarehe 3 July, 2021 ipo au haipo?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,544
108,871
Katika ile Barua ya Kusimamisha Mchezo (Mechi) ilisema Serikali yako na kupitia Wizara yako ya Michezo ndiyo mliisimamisha.

Siku zinakaribia na kuna Timu inasema haitocheza hadi ipewe sababu ya maana ya Kusimamisha ile ya awali.

Tafadhali Waziri Bashungwa jitokeze hadharani, toa sababu ya Serikali juu ya Kusimamisha Mchezo ule na Tamko lenu pia.

Waziri Bashungwa usipoangalia na kuwa makini na hili nakuhakikishia linaweza Kugharimu hata Uwaziri wako.

Tunaomba Tamko la Serikali juu ya wale waliolipia Tiketi, Uhakika wa Mechi na sababu ya Kuihairisha ghafla vile.

Nimelileta hili tena Kwako kwakuwa tayari Wadau wa 'Derby' hii kutoka Mikoani na nje ya nchi wanataka Kuja Kuiona.

Najua Waziri Bashungwa unapatwa na 'Kigugumizi' kwakuwa ni mwana Yanga SC ila jitoe Mhanga ulimalize rasmi hili.

Sitokukumbusha hili tena ila jiangalie.
 
Atakua anajiandaa kula lunch hii mida mpe muda kidogo atakujibu
na warembo kwa raha zake, enzi za JIWE hata ukiteuliwa hakuna kufanya party, ndio maana makampuni ya cataring yalifiliska, hakuna party, office party, birthday yaani kununua ndge kwa cash tu.
 
na warembo kwa raha zake, enzi za JIWE hata ukiteuliwa hakuna kufanya party, ndio maana makampuni ya cataring yalifiliska, hakuna party, office party, birthday yaani kununua ndge kwa cash tu.
Mkuu si nimesikia yule michepuko yuko mbali nayo yeye ni mkewe tu mkewe na yeye,
 
Back
Top Bottom