Waziri Mwanamke Aiba Mme wa Mwingine!!!

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
15,744
19,783
Nimesoma hadithi hii kutoka mojawapo ya magazeti ya udaku ya bwana Shigongo; sina uhakikai kama ina ukweli wowote. Kama ni kweli basi serikali yetu ina miamba kweli kweli kuhusu mambo haya ya ngono: waume kwa wake mtindo mmoja. Watakuwa wanaelewana sana.

Mmoja kati ya mawaziri wa kike aliyepewa dhamana kubwa na Rais Jakaya Kikwete, amehusika kupora mume wa mtu.

Habari za kuaminika na zilizofanyiwa utafiti wa kina kwa muda mrefu sasa, zimebainisha kuwa waziri huyo mwenye dhamana kubwa, ameingia katika mtego huo kutokana na maelewano na mume wake wa ndoa kupungua.

Waziri huyo ambaye aliwahi kuwa na dhamana katika taasisi moja, alianza uhusiano huo wa kimapenzi na mume huyo wa mtu kabla hajala kiapo cha utii mbele ya Rais Kikwete mapema mwaka 2006.

Ilitegemewa kwamba wakati akila kiapo hicho na hasa kutokana kuwa anafuatiliwa na wengi, angeacha ‘mchezo mbaya’ wa kumtoka mumewe na kwenda kwa ‘kidume’ chake, lakini ikawa kama amekula pilipili za Kihindi kwa jinsi alivyozidi kuhaha.

“Hii ni kashfa kubwa na mumewe mpaka sasa hajui, ila mke wa jamaa ameamua kwa dhati kabisa kulifikisha suala hili Ikulu ili lishughulikiwe, kwani ameona hatendewi haki na hapati huduma zinazostahili kutoka kwa mumewe.

“Mara nyingine utakuta wanakuwa wote kwenye gari na kibaya zaidi kwa watu wengine anatambulishwa kama msaidizi wake binafsi, lakini kumbe ndiyo anamtendea vibaya mwanamke mwenzake,” kilisema chanzo chetu.

Chanzo hicho chenye kuaminika zaidi kilizidi kutupasha kuwa, waziri huyo ameshafika mara kadhaa na mume huyo wa mtu kwenye nyumba aliyokabidhiwa na Serikali, huku mumewe akidanganywa kwamba ni mmoja kati ya wasaidizi wake.

Mbali na kudanganywa kama mmoja wa wasaidizi wake, mume wa waziri pia amekuwa hana hofu yoyote pale anapowaona wawili hao wakiwa pamoja kwani anajua anatekeleza majukumu ya Kitaifa.

Inadaiwa tatizo kubwa linalomkumba waziri huyo ni ‘kupenda kushikwa masikio’ na kiongozi mwingine mwandamizi ambaye wengi wanadai ana ‘kauzoefu’ ka-kutosha katika kuisaliti ndoa yake.

Chanzo chetu kinasema kuwa, kabla ya kuanza kwa kikao cha Bunge ambacho mpaka sasa kinaendelea huko Dodoma, mwanamke aliyekuwa analiwa mali alifikisha lalamiko lake kwa familia ya waziri huyo.

“Wazee wa familia wameamua kuanza kulishughulikia wao kwanza, kwani wanaona itakuwa aibu kubwa mumewe akijua. Wanachohofia ni ndugu yao kuporomoka kisiasa.

“Hata la kwenda kushitaki Ikulu yule mwanamke aliyeporwa ameambiwa asubiri kwanza, kuna kikao kingine kinafanyika Jumapili wiki hii ambacho ndicho kinachotarajiwa kutoa maamuzi juu yake,” kilisema chanzo chetu.

Mwanamke aliyeporwa mume alipozungumza na gazeti hili, alikiri kutokea kwa jambo hilo na kudai tayari alishafika Ikulu juzi Jumatano na kuahidi kuleta ushahidi kamili kwetu pamoja na nakala ya barua ya malalamiko yake aliyotaka ifike mikononi mwa Rais Kikwete.

Waziri huyo alipotafutwa kabla ya kwenda Dodoma, alimshangaa mwandishi na kuomba asiulizwe vitu hivyo, huku akidai kuna vitu vingi si vya kweli, ila maadui wa kisiasa ndiyo wanamuandama.

“Aende tu huko Ikulu, lakini hawa ni wanasiasa ndani ya jimbo langu ndiyo wanaucheza mchezo huu na mimi nahakikisha nitawashinda tu. Ila naona na wewe tayari umeshanunuliwa kunimaliza wakati ni ndugu yangu,” alisema.

Sakata hili tunalifuatilia kwa makini zaidi, na tunaahidi kuweka wazi kila kitu na jina lake hivi karibuni.
 
Magazeti ya shigongo bwana ya ajabu sana sijui huwa anatumia uandishi upi labda kwakuwa kila mtu ni msanii na anaweza kuwa mwandishi vile vile bila kujali taaluma kwanini asieleze kinagaubaga kwa kumtaja na jina na aweke picha kabisa ya huyo waziri...magazeti ya udaku yapo kila sehemu, na pia husaidia kuwafanya watu wajiheshimu...sasa nikosoma hiyo article hapo juu sipati chochote udaku ndani ya udaku....hebu wajifunze kwa wenzao magazeti kama la the sun la UK waliandika udaku na picha, si mnaona walivyo mmaliza Ashley Cole analivyo cheat mkewe Chery?
 
kichuguu mpaka na wewe umeweka udaku wa shigongo hapa, basi mzee naanza kupata wasiwasi na wewe.
 
kichuguu mpaka na wewe umeweka udaku wa shigongo hapa, basi mzee naanza kupata wasiwasi na wewe.

  1. Mwnamama, karibu ukumbini hapa. Naona umejiunga JF ili upate nafasi ya kujibu post hii ambayo ni ya udaku. Hiyo ni hatua nzuri kwa vile siyo tu kuwa umenongeza namba ya wanachama wa JF, bali pia ninategemea kuwa hukuvutiwa na udaku tu bali utaweza kuchangia mada nyingine za maana zaidi ya hizi za udaku.
  2. Nilipoweka hapa kopi ya article hiyo kutoka gazeti la Shigongo, nilitahadharisha wazi kabisa kuwa nimeitoa wapi na sina uhakika kama ni ya kweli. Sababu yangu kuiweka hapa ilikuwa ni kutaka kujua kama udaku huo una ukweli wowote; inawezekana kuna mwanachama wa JF anaielewa stori hii kiundani zaidi. Tumekwisha jionea daku mbalimbali zinakuja thibitishwa kuwa ni za kweli.
  3. Binafsi nimeshakuwa na mashaka sana na credibility ya viongozi wetu wa serikali yetu, ndiyo maana naweza kutafuta zaidi kuhusu daku zozote zinazowahusu kama hizi.
 
Magazeti ya shigongo bwana ya ajabu sana sijui huwa anatumia uandishi upi labda kwakuwa kila mtu ni msanii na anaweza kuwa mwandishi vile vile bila kujali taaluma kwanini asieleze kinagaubaga kwa kumtaja na jina na aweke picha kabisa ya huyo waziri...magazeti ya udaku yapo kila sehemu, na pia husaidia kuwafanya watu wajiheshimu...sasa nikosoma hiyo article hapo juu sipati chochote udaku ndani ya udaku....hebu wajifunze kwa wenzao magazeti kama la the sun la UK waliandika udaku na picha, si mnaona walivyo mmaliza Ashley Cole analivyo cheat mkewe Chery?

Nimeteta mara nyingi jamani bongo tuna ma reporter na sio ma journalist...usiende mbali angalia jurani zetu e.g Kenya.
 
Kama kuna wazinifu ktk Baraza la Mawazir nao hawafai...maana uzinifu kama kama mkikubaliana ni UFISADI kwenda Mbele. Vipi wale waliokubaliana ktk Mikataba FEKI, na UZINIFU ni MKATABA FEKI...WATU wanaoharibu Marriage Institution hawafai hata kupewa UJUMBE wa NYUMBA 2..sembuse madaraka ya nchi...

Mawaziri FISADI ktk UZINIFU WAKIFA NJE ya nchi jambo la kwanza kutafuta vimwana na ndo maana hawataki kusafiri na wake ZAO. WATALETA VISINGIZIO LUKUKI.
 
wana JF tusiwe tuna jump conclusion kwa sababu ya dhana..hakuna specific kuhusu swala hilo besides imetokea kwenye tabloid paper yetu ya bongo kama mjuavyo mara nyingi wanaandika udaku ambazo ni pumba tupu...kama ni kweli where are the names za wahusika?
 
Back
Top Bottom