Waziri Mwambe: Mazungumzo ya ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo kuanza rasmi

Sasa mwendazake yale maneno aliokuwa anadanganya Umma wa Watanzania aliyatoa wapi, kwa maelezo haya ya Mwambe naamini kwa asilimia mia 100 yule mzee hakuwa na nia ya dhati kutusaidia watanzania... Halafu anasema msema kweli mpenzi wa Mungu... Hakika tutaendelea kumshukuru Mungu.
Kipi kimekufanya umuone mwenda zake ni myongo na huyu ndo mkweĺi
 
Wameandika wapi bandari nyingine zitakufa, Hayati kawatia upofu watu wengi sana aisee. Inabidi itolewe elimu kubwa sana kwa Umma. Mtu alijenga uwanja wa ndege kijijinii kwake na bila bunge kupitisha sijui tulirogwa.
Haa sio lazima uambiwe mkuu jiòngeze tu kila mtu akikwambia usiendeleze bandari yoyote kutoka dar mpaka pangani according tu mwambe ni lazima anatafuta monopoly ya biashara
 
Wameandika wapi bandari nyingine zitakufa, Hayati kawatia upofu watu wengi sana aisee. Inabidi itolewe elimu kubwa sana kwa Umma. Mtu alijenga uwanja wa ndege kijijinii kwake na bila bunge kupitisha sijui tulirogwa.
Kwani mpaka uandikiwe au uambiwe. Wewe huwezitumia akili zako. Dar inapanuliwa tena kwa mikopo. Huku unajenga bandari nyingine kwa mikopo. Vitu vya kusafirisha huna.

Unategemea Burundi na Rwanda ziazolingana na mkoa wa Mara. Matumizi ya bandari yanategemea maelewano ya kisiasa. Kesho na kesho kutwa Zam,bia inapitisha copper yake Msubiji.

DRC wanatutegemea kwa sababu ya vita. Vita ikiisha wana njia nyingi za kupitisha mizigo. Uganda ikimpata kichaa, atapitisha mizigo Mombasa na Lamu, sasa Bagamoyo itabeba mizigo gani. Ya wachawi Mlingotoni!
 
Kusikia Kwa Kenge Hadi Atoke Damu Puani Na Masikioni

Mabeberu Ya China Yanakuja Kujichotea Vyote Mkataba Wa Miaka 1000 Oops

Yale Ya Loliondo Waarabu Wamechukua Nchi Viongozi Wakiona Na Hawana La Kusema
Hapa umepigilia msumari kwenye kidonda. Si wote wanaolijua hili ila kiukweli loliondo imeuzwa na kipande kile hakuna mwenye uwezo wa kuingia wala kukagua. Madege ya mzigo yanatuambugani ni ajabu kweli.
 
Awamu ya sita ipo sahihi kabisa. Yawezekana kabisa Mkataba ulisainiwa kipindi cha JK na awamu ya tano ilipoingia iliukuta na ikapaswa kuutekeleza.

Hata hivyo awamu hiyo ikaupiga teke kule na kuupeperushia mbali sana baada ya kuuchana chana.

Sawa imeingia awamu ya sita na haiuoni huo Mkataba, sasa itasemaje upo? WaTanzania wagumu kuwelewa.

Tena ungekuwepo halafu tukae kuutekeleza wale jamaa si wangetulalamika na kutushtaki kabisa! Mkataba haupo bhana!
 
Hizo kelele za chawa wa mwenda zake zisitukatishe tamaa kamati maalum iupitie urekebishwe inapobidi watu waingie kazini vijana wapate ajira maisha ni mafupi sana na yanakimbia kweli,mtapigizana makelele hapa kazi Hamna na hamfaidiki na lolote mje kujifia vibudu,mkataba ufufuliwe uangaliwe upya urekebishwe,kazi ianze Mara moja.
 
Usiwaamini hawa watu.

Sawa amezipitia, swali ni je, ana utaalamu wa mikataba na maswali mengine ya kitaalamu?

Kama ambavyo Mbowe sio gaidi, na sisi wananchi sio wajinga.
Enzi za JK hiyo wizara ya uwekezaji haikuwepo.Kama nyaraka zilikuwa Ikulu atatuambia nini?
Kwenye viapo huwa nasikia
"Sitatoa siri bila idhini ya Rais"
Hivyo kuwakana marais wa awamu ya 4&5 Luna baraka za awamu ya 6.
 
Waziri wa uwekezaji Mr. Mwambe amesema hakuna mkataba wowote uliosainiwa hapo awali kuhusu bandari ya Bagamoyo zaidi ya minutes tu za vikao.

Mwambe amesema serikali itaanza rasmi mazungumzo na Oman na China ikiwa na maagizo ya Rais Samia baada ya kuwa amezipitia nyaraka zote.

Chanzo: ITV habari

Pia soma
Mwambe anajua kabisa kuwa kabla ya mkataba wowote kusainiwa kunakuwa na MoU ambayo ndo huwa basis ya mkataba husika. inawezekana mkataba ulikuwa haujasainiwa ila MoU ilisainiwa, asitake kumdhalilisha hivyo huyu mzee aliyejipumzikia, RIP JPM
 
Hatimaye malengo yametimia Rasmi.

Lengo lilikuwa Bandari ya Bagamoyo na Gesi sasa mafisadi wameshinda.

Kwaheri mama Tanzania.
 
Dhahabu tunaibiwa mwaka wa 30 huu, gas kibao lakini hata umeme wa kuwasha kibatari hakuna, usiamini hili kundi la wahuni wasio na akili na wapo pale kwasababu ni wezi wa kura
 
Tatizo la Watanzania ujuaji wa kila kitu hata kwa kile hatuna ufahamu nacho umetujaa. Sikushangaa awamu ya tano kuingia mikataba kimyakimya iliogopa ujuaji wa namna hii. Tuache Tanzania ya kisasa ijengwe walau tutaweza kupata japo hata kakibarua ili familia iweze kuishi
Sio ujuaji, watu wana haki ya kuhoji na kujua kinachofanyika ni nchi ya wote na hao viongozi sio baba au mama wa familia ni raia tuu kama wengine wafuate sheria na sio kutupa mikataba ya kitapeli kama uzoefu unavyoonyesha, kama wewe umezoea kuburuzwa ni shida yako na pole sana
 
Sio ujuaji, watu wana haki ya kuhoji na kujua kinachofanyika ni nchi ya wote na hao viongozi sio baba au mama wa familia ni raia tuu kama wengine wafuate sheria na sio kutupa mikataba ya kitapeli kama uzoefu unavyoonyesha, kama wewe umezoea kuburuzwa ni shida yako na pole sana
Tatizo ninyi mnaohoji awamu ya sita mmejiona mnahakimiliki ya nchi hii wakati wa awamu ya tano walipokuwa wanahoji mliwaona sio raia wa nchi hii.
 
Back
Top Bottom