Waziri Mwambe: Mazungumzo ya ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo kuanza rasmi

Waziri wa uwekezaji Mr Mwambe amesema hakuna mkataba wowote uliosainiwa hapo awali kuhusu bandari ya Bagamoyo zaidi ya minutes tu za vikao.

Mwambe amesema serikali itaanza rasmi mazungumzo na Oman na China ikiwa na maagizo ya Rais Samia baada ya kuwa amezipitia nyaraka zote.

Chanzo: ITV habari
Hatujapigwa?
 
In the first place we were told that the Bagamoyo Port Project lacked economic sense and that it aimed at exploiting the country but today it's a shifting narrative.

It's obvious that Kikwete is behind the scenes pulling the strings in this project. He is the one who coined this project apparently owing to his personal interests as a native of Bagamoyo.

This simply shows how development projects in this country are being manipulated by greedy politicians to fulfill their personal selfish interests to the detriment of the people they hypocritically claim to be defending their interests.

It's time to get rid of these wolves masquerading as the sheep.
 
Huu mradi utaharakishwa kwa manufaa ya watu wachache wakishirikiana na wawekezaji wanyonyaji bila kutazama kwamba kuna kizazi cha kesho kitaumia.

Megaproject kama hii inaitaji uwazi na busara za hali ya juu sio kuendekeza njaa. Utaliuza taifa na vijana wake. Ova
 
Who is Dr. Chamuriho....unaambiwa mkataba haukuwepo unaleta undezi hapa simama katika HOJA.
Acha undezi kenge nyie. Haukuwepo vipi wakati makubariano yanarudi tena kwa wale wale China na Oman?.
 
Sasa mwendazake yale maneno aliokuwa anadanganya Umma wa Watanzania aliyatoa wapi , kwa maelezo haya ya Mwambe naamini kwa asilimia mia 100 yule mzee hakuwa na nia ya dhati kutusaidia watanzania... Halafu anasema msema kweli mpenzi wa mungu... hakika tutaendelea kumshukuru mungu.
Daaah! Hakika Africa ni ile ile
 
Sasa mwendazake yale maneno aliokuwa anadanganya Umma wa Watanzania aliyatoa wapi , kwa maelezo haya ya Mwambe naamini kwa asilimia mia 100 yule mzee hakuwa na nia ya dhati kutusaidia watanzania... Halafu anasema msema kweli mpenzi wa mungu... hakika tutaendelea kumshukuru mungu.
Kweli watu mpo kimatumbo zaidi
 
Sasa bado najiuliza hivi ilikuwaje kwa Rais Kikwete tarehe 16/10/2015 pale bagamoyo aliweka jiwe la msingi la kuanza kujengwa bandari hiyo ya Bagamoyo ikiwa mkataba ulikuwa bado haujasainiwa?

Hawa jamaa wanatufanya sisi mazuzu.
Hakika tumepigwa na kitu kizito kichwani
 
Wameandika wapi bandari nyingine zitakufa, Hayati kawatia upofu watu wengi sana aisee. Inabidi itolewe elimu kubwa sana kwa Umma. Mtu alijenga uwanja wa ndege kijijinii kwake na bila bunge kupitisha sijui tulirogwa.

Kushabikia ujenzi wa hiyo bandari pasipo kujiridhisha kwa hiyo mikataba ni uzwazwa.
Wewe ulijirizisha na mkataba wa ujenzi wa bwawa la umeme mto rufiji?? Mbona uliushadadia??
 
SERIKALI imesema hivi karibuni itaanza mazungumzo na wawekezaji wa Bandari ya Bagamoyo ili kuendeleza eneo kwa ajili ya kujenga bandari, eneo la viwanda na eneo la masuala ya usafiri na usafirishaji.Hayo yalibainishwa jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Uwekezaji, Geoffrey Mwambe, jijini Dar es Salaam.Mwambe, alisema Kampuni za China Merchants Holdings (International) Co. Ltd (CMHI) na Mamlaka ya Uwekezaji Oman (OIA) ambayo awali ilikuwa ikijulikana kama Mfuko wa Uwekezaji wa Serikali ya Oman (SGRF)

 
Ule ambao mlevi taahira tu ndio anaweza kusaini? JPM ndio alisema hivyo, kwahiyo hii ni serikali ya walevi?
 
Shangililia baada ya kujua mkataba ukoje. Acheni kuwa mazuzu.
Mlivyokuwa mnashangilia mikataba ya mwendazake mlikuwa mmeisoma? mwacheni mama apige kazi. Bora ht yeye tunaweza tukaiona mikataba kuliko ya yule aliyeficha mikataba na kuanza kuwekea Kinga Hadi spika wa bunge
 
Waziri wa uwekezaji Mr. Mwambe amesema hakuna mkataba wowote uliosainiwa hapo awali kuhusu bandari ya Bagamoyo zaidi ya minutes tu za vikao.

Mwambe amesema serikali itaanza rasmi mazungumzo na Oman na China ikiwa na maagizo ya Rais Samia baada ya kuwa amezipitia nyaraka zote.

Chanzo: ITV habari

Pia soma
Hivyo viwanda vya mbolea kwanini visijengwe Mtwara Lindi na Bandari Mtwara kuimarishwa tena ni natural port
 
Kipindi fulani kwenye issue za negosition kama hizo unakuta timu kama wakina Dr. Chamuriho ambae aliongoza timu ya negosition mradi wa SGR, Ununuzi wa ndege pamoja Bwawa la Mwalimu Nyerere ila kwasasa anaonekana hafanyi kazi vizuri chini ya Rais Samia, pembeni ungemkuta Marehemu Mfugale, wingi ya kulia ungemkuta Engineer Kakoko then unakuta watu wa Tanroads, watu sheria, etc na hao wote walikuwepo kwenye ile team ya mwendazaje iliyosema kwa masharti haya hapana kama vipi ya kwetu ni haya hamtaki rudini mkajipange tena.

Lakini safari hii tarajia kukutana na wanasiasa na wanadiplomasia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimesikia clous eti watajenga kisha watakusanya mipesa yao mpaka itakapo rudi ndo tuachiwe bandali sasa sijui itakua miaka mingapi?
Wakipata hasara tutasunili, nadhani kizazi kijacho ndo kitapewa hiyo bandali.
 
Who is Dr. Chamuriho....unaambiwa mkataba haukuwepo unaleta undezi hapa simama katika HOJA.
Nadhani tunang'ang'ania neno mkataba bure. Mkataba utakuwepo tu pale sahihi zitakapowekwa. Kabla ya mkataba kunakuwa na mazungumzo. Baada ya mazungumzo, kunakuwa na makubaliano (memorandum of understanding kwa kifupi MoU). Yale makubaliano yakitiwa sahihi tu, ndiyo unapatikana mkataba.

Kwa maana hiyo MoU ilikuwepo na ndiyo ilikuwa na madudu yaliyowahi kusemwa. Wachina wakati mwingine ni wabaya saana. Walipokubali kujenga reli ya Kenya kulikuwa na madudu mengi. Madudu hayo yalikujajulikana walipoanza kuyatekeleza. Ile reli waliyojenga Kenya inaendeshwa na wao na pesa yote wanakusanya wao. Huku deni watalipwa lakini mapato wanakusanya kwa miaka 10. Pia kulikuwa na makubaliano kuwa ikianza kazi, basi mizigo yote ya bandari za Mombasa na Lamu itabebwa na hiyo reli. Wafanya biashara walifungiwa kujihusisha na mizigo ya bandarini. Hapo umeua ajira ngapi.

Nadhani sisi wananchi tunachotakiwa kujadili ni je kama ni kweli hayo yaliyosemwa yamo kwenye MoU ni vipi kama nchi na wananchi wake tutaathirika. Tuachane na haya kubishana kisiasa na kiitikadi bali tuangalie kama hayo masharti ni kweli tuyakubali au tuyakatae. Nadhani imefika wakati muafaka, wa kuanza kutumia pesa kuinunua hiyo mikataba na kuiweka wazi. Wakati wa nyuma, mambo yalivyokuwa mabaya saana, mikataba ilianza kupatikana kirahisi. Kwenye hii mikataba kuna walaji, wasiyokula, na waliyodhulumiwa upigaji. Hao ambao wamedhulumiwa au waliyonyimwa mgao ni rahisi saana kuwarubuni kwa kiasi kidogo na wanaweza kutumegea nakala za mikataba. Mnakumbuka. Kuliko kupiga kelele kwenye mitandao usiku kucha, tutafute njia ya kuiweka mikataba na MoU bayana. Ni rahisi kuipata. Unaweza kuipata chini ya 1% ya ile pesa iliyopigwa. Kuna sponsors wengi wenye kuitakia TZ mazuri, na wanaweza kukupa hiyo hela kidogo ya kuinunua mikataba na kuiweka hadharani. Hii ndiyo njia pekee, maana mikataba mingi ina kifungu cha confidentiality kinachowafunga kutoa yaliyomo kwenye mikataba.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom