Waziri Mwambe: Kinachojengwa ni Bagamoyo Economic Zone Bandari ni sehemu ndogo tu ya huo mradi. Bandari itatumia hekta 800 tu kati ya 9800!

Kuna kitu hakipo sawa na tena ambacho kinafichwa kuhusu huu mradi huu wa Bagamoyo Economic Zone ikiwemo na bandari ya Bagamoyo. Kwa nini watu wanapewa habari nusu nusu tena zenye kukinzana kuhusu huu mradi?

Waziri anazungumza hiki, spika anabadili msimamo na kusema hiki eti JPM alishauriwa vibaya juu yake, kamarade Mangula anasema katika ilani hakuna kitu kama ujenzi wa bandari bali kuna ujenzi wa gati!? Kila mtu ni msemaji na mwenye kusema lile alijualo yeye mwenyewe.

Serikali si ina msemaji wake rasmi, kwa nini asiliongelee jambo hili kwa kina ili wananchi tupate kujua msimamo wa serikali ni upi. Hii inatokana na ukweli kwamba Rais aliyepita alishatoa msimamo wa serikali kuhusu vipengele vingi vyenye masharti magumu katika mkataba kitu ambacho alilazimika kuachana nao.

Sasa hivyo vipengele vyenye masharti hayo vimebalishwa lini kiasi kwamba serikali sasa imeamua kuanza tena kuupigia upatu mradi huu! Ni lazima serikali ikachukua tahadhari kubwa kabla haijafanya maamuzi na kujiingiza katika miradi mikubwa na yenye kugharimu fedha nyingi.

Ni vyema serikali ikajifunza kutoka kwa nchi jirani ambayo imechukua mikopo yenye masharti magumu kiasi cha kushindwa kulipika na hatimaye mali za nchi zilizowekwa kama dhamana kuanza kutaifishwa. Nikiangalia kwa jicho la tatu, katika mradi huu ninaona "risk appetite" ya uwezaji huu mkubwa unasumwa na maslahi ya watu binafsi ambao watafaidika kiuchumi zaidi ya uwepo wa msukumo wenye kuzingatia uzalendo na maslahi mapana ya taifa.

Baniani mbaya kiatu chake dawa. JPM katika mradi huu daima utakumbukwa kwa uzalendo wako.
Msimamo wa serikali ni Mradi kujengwa no matter what.
 
Ccm hawajawai kufanikiwa tuliwai oneshwa picha za kigamboni wanavyotaka iwe. Watu tukajaaa kununua maeneo kigamboni kumbe janja janja.

Mfano dege eco village
Uko sahihi.
Wakaanzisha nida -hewa.
Hata haya mamiradi ya awamu ya Tano yote yatawashinda na kufa.
BRT, Kwa mpango wa awali ilitakiwa tuwe phase 3 or 4 Leo hii ni zero.
GDP data kuupdate kila mwaka hawawezi hafi IMF na world bank wawasaidie, wakati nchi jirani kila mwaka wana update GDP na income per capital ya wananchi wao, tuna taifa na viongozi wa hovyo sana hadi wasukumwe ndo wanafanya kazi.
 
Kwa hiyo mji wa kisasa hadi tujengewe na wachina, hivi haiwezi kutolewa masterplan ya mji wa kisasa wakapewa designers ambao watabuni aina ya nyumba na majengo ya kibiashara na ya kijamii na wakanunua wazawa wenye uwezo na wawekezaji wa kutoka nje? ndo yale yale ya kigamboni tuliambiwa utajengwa mji wa kisasa kama Newyork. Cha muhimu kama kunahitajika uwekezaji mkubwa kwenye bandari ya bagamoyo ambao utahitaji kushirikisha wawekezaji wa nje kama china na saudi arabia, ni bora mkataba huo uzingatie maslahi ya nchi kwanza.......na wawekezaji wapewe muda ambao watakuwa wamerudisha gharama na kupata faida na baada ya huo muda mkataba mwingine uingiwe endapo watahitaji kuendelea.​
 
Tusipojenga Bandari ya Bagamoyo tutakuwa wajinga na wapumbavu.

Kuna miradi ya ovyo imefanyika kama uwanja wa ndege wa Chato, ambapo pesa zilizotumika huko zingepelekwa kwenye miradi ya muhimu kama Bandari ya Bagamoyo
Sio lazima kujenga. Kwani bandari ziko ngapi? 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂
 
Waziri wa Uwekezaji Mh Mwambe amesema kinachojengwa Bagamoyo siyo Bandari tu bali unajengwa mji wa kisasa utakaoungana na Dar es salaam ambao utakuwa na miradi mingi ikiwemo Viwanda Mahotel uwanja wa mpira, appartments na mengine mengi kwahiyo Bandari ya Bagamoyo ni sehemu ndogo tu ya huo mradi na TPA imepewa hekta 800 kati ya hekta 9800 za mradi.

Bandari ya Bsgamoyo ni ya TPA na jiwe la msingi lilishawekwa na Rais mstaafu mzee Kikwete.

Mwambe amesema hapakuwa na mkataba wowote ambao serikali imeshasaini na China ndio maana hayati Magufuli aliunda timu za majadiliano kabla ya kufikia hatua ya kusaini.

Mjadala uko mubashara ITV kipindi Meza Huru

My take; Kiukweli Bagamoyo ngoma bado mbichi.
Bwashee dawa ya huu mradi ni Katiba Mpya ya Wananchi. Hivi huyo Waziri anajua anawakilisha watu zaidi ya 60m!
 
Tumeshang'atwa na nyoka Mtwara, Buzwagi, Geita, North Mara nk

Tuwe makini, tusingwate tena. Muhimu maswala muhimu kuweka wazi, kuwa na uwazi, ukweli.

Muhimu pia kupata maoni ya shareholders, Wadau muhimu ni sisi Watanzania wote.

Dili likibuma sisi ndio tutalipia kwa vizazi na vizazi. (99 years)
 
Chato hata billion 10 hazikufika ila hamuoni billion 400 za covid mkopo wakaolipa watanganyika umepelekwa zanzibar kwa watu million 1.5 huku watanganyika million 60 wakiachiwa billion 700, akili huna
Mpumbavu huyo
 
Mpumbavu huyo
Mpumbavu kweli, ni mara Mia Chato Geita wanachangia mapato makubwa serikalini kupitia migodi ya dhahabu na mtanzania yeyote anaweza kumiliki ardhi Geita

Huyu mjambiani kachukua billion 400 kwenda zanzibar ambayo mtanganyika ni second citizen kule, ni wabaguzi na mtanzania hawezi kumiliki hata hatua 1 ya ardhi

Mkopo wote huu ni mtanganyika ataulipa sababu sio pesa za msaada na Zanzibar haiwezi kulipa huu mkopo wala mkopo haukutoka kwa zanzibar , lakini hili wana harakati hawalioni kama ni ufisadi mkubwa na kinyume cha mambo ya muungano watu million 1.5 wamepewa billion 400 wakati watanganyika million 60 wakiachiwa billion 700
 
Inasikitisha sana, kwan unafikiri nchi ina wanaharakati? Kuna wapumbavu tu ambao hujiita wanaharakati
 
Waziri wa Uwekezaji Mh Mwambe amesema kinachojengwa Bagamoyo siyo Bandari tu bali unajengwa mji wa kisasa utakaoungana na Dar es salaam ambao utakuwa na miradi mingi ikiwemo Viwanda Mahotel uwanja wa mpira, appartments na mengine mengi kwahiyo Bandari ya Bagamoyo ni sehemu ndogo tu ya huo mradi na TPA imepewa hekta 800 kati ya hekta 9800 za mradi.

Bandari ya Bsgamoyo ni ya TPA na jiwe la msingi lilishawekwa na Rais mstaafu mzee Kikwete.

Mwambe amesema hapakuwa na mkataba wowote ambao serikali imeshasaini na China ndio maana hayati Magufuli aliunda timu za majadiliano kabla ya kufikia hatua ya kusaini.

Mjadala uko mubashara ITV kipindi Meza Huru

My take; Kiukweli Bagamoyo ngoma bado mbichi.
Huyu ndio anazidi kutuchanganya
 
Tusipojenga Bandari ya Bagamoyo tutakuwa wajinga na wapumbavu.

Kuna miradi ya ovyo imefanyika kama uwanja wa ndege wa Chato, ambapo pesa zilizotumika huko zingepelekwa kwenye miradi ya muhimu kama Bandari ya Bagamoyo
Urojo mtupu dada ni Mapesa mangapi yametimika huko Chato airport ? Kwa uwezo wako mdogo unayafamu?
 
Mpumbavu kweli, ni mara Mia Chato Geita wanachangia mapato makubwa serikalini kupitia migodi ya dhahabu na mtanzania yeyote anaweza kumiliki ardhi Geita

Huyu mjambiani kachukua billion 400 kwenda zanzibar ambayo mtanganyika ni second citizen kule, ni wabaguzi na mtanzania hawezi kumiliki hata hatua 1 ya ardhi

Mkopo wote huu ni mtanganyika ataulipa sababu sio pesa za msaada na Zanzibar haiwezi kulipa huu mkopo wala mkopo haukutoka kwa zanzibar , lakini hili wana harakati hawalioni kama ni ufisadi mkubwa na kinyume cha mambo ya muungano watu million 1.5 wamepewa billion 400 wakati watanganyika million 60 wakiachiwa billion 700
Kuna watu, watu wengi hawana akili timamu.
 
Duh, sasa ujenzi wa hii bandari inaya bagamoyo kwa upande mwingine inaweza ikawa ni White elephant kwa taifa....
Kwa sasa tungepanua gati ya bandari ya dare salaam. Then tukiona productivity ni kubwa basi tupanue ya bagamoyo ila kwa sasa tungoje kwanza unless otherwise kama.... mkere hanataka msoga ipanuke kiuchumi...
Kumbuka wachina wapo too objective na hii project ya bandari ya bagamoyo..
Anyway ruombe uzima tule mema ya nchi
 
Back
Top Bottom