Waziri Mwambe: Kinachojengwa ni Bagamoyo Economic Zone Bandari ni sehemu ndogo tu ya huo mradi. Bandari itatumia hekta 800 tu kati ya 9800!

Waziri wa Uwekezaji Mh Mwambe amesema kinachojengwa Bagamoyo siyo Bandari tu bali unajengwa mji wa kisasa utakaoungana na Dar es salaam ambao utakuwa na miradi mingi ikiwemo Viwanda Mahotel uwanja wa mpira, appartments na mengine mengi kwahiyo Bandari ya Bagamoyo ni sehemu ndogo tu ya huo mradi na TPA imepewa hekta 800 kati ya hekta 9800 za mradi.

Bandari ya Bsgamoyo ni ya TPA na jiwe la msingi lilishawekwa na Rais mstaafu mzee Kikwete.

Mwambe amesema hapakuwa na mkataba wowote ambao serikali imeshasaini na China ndio maana hayati Magufuli aliunda timu za majadiliano kabla ya kufikia hatua ya kusaini.

Mjadala uko mubashara ITV kipindi Meza Huru

My take; Kiukweli Bagamoyo ngoma bado mbichi.
Mangura mzee wa chama amesema mladi huo haupo katika ilani ya chama hivyo kafunga mjadala.
 
Tusipojenga Bandari ya Bagamoyo tutakuwa wajinga na wapumbavu.

Kuna miradi ya ovyo imefanyika kama uwanja wa ndege wa Chato, ambapo pesa zilizotumika huko zingepelekwa kwenye miradi ya muhimu kama Bandari ya Bagamoyo
CCM inamitaji ya watu wajingawajinga kama wewe na kikundi chako .. sumaleda wewe
 
Tusipojenga Bandari ya Bagamoyo tutakuwa wajinga na wapumbavu.

Kuna miradi ya ovyo imefanyika kama uwanja wa ndege wa Chato, ambapo pesa zilizotumika huko zingepelekwa kwenye miradi ya muhimu kama Bandari ya Bagamoyo
Kwa hiyo walipize kisasi
 
Nikusaidie tu kinachotafutwa ni monopoly ya badari ya daresalaam , bandari ya bagamoyo itakuwa inaufanisia wa hali ya juu na very high tech sasa nani atapitisha vitu kwenye bandsri yetu aache ile ya bagamoyo kwa hiyo vikampuni vyetu vitakufa kabisa na ajira zitapotea kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
Bandari yetu ya sasa itakuwa kama shirika la post haina ufanisi.
 
Wahamasishe na mataga wenzako sasa.
Swala la Bagamoyo lisubiri tume huru ya uchaguzi, katiba mpya then kwavile tutakuwa na Bunge lenye fair representation likajadiliwe bungeni kulinda maslahi ya Taifa kuzuia lobbyists wenye nia ovu kutuingiza mtegoni.
 
Jiwe la msingi liliwekwa na Jk awamu ileeeeee
Sasa mtasubiri ujenzi miaka 30 mingine wakati hela zitakuwa zimeishapigwa huku mkiambiwa feasibility study zinaendelea
 
IMG_3396.jpg
 
Porojo za nini, wekeni mkataba mezani tuuone kwanini mnasemea uvunguni?

Kigugumizi kinatoka wapi? Wekeni mkataba wazi, MOU, kama mnajadiliana mtuambie vipengele vya majadiliano ni vipi?

Kama ni mkataba mzuri, mtaungwa mkono na wengi.

Hatutaki ile mikataba ya kikoloni ya kina Chief Mangungo, mikataba ya kuuza nchi.
 
Umemjibu kizalendo kweli. Labda nikuulize, unadhani huu mradi katika ukamilifu wake na katika dunia ya sasa utamuathiri vipi mkazi wa bagamoyo na pwani mzalendo mnyonge yule wa chini kabisa anayeshindia kitumbua?
Sioni ukimgusa mtu wa chini ukiachilia upatikanaji wa vibarua tu small wages! Wa mwanzo watainjoy fidia tu
 
Kundi la wahuni liko kazini, ila patachimbika ile mbaya na huenda ndio ukawa mwisho wa CCM hii ya wezi.
HUU MRADI NI MUHIMU SANA,NI LAZIMA UJENGWE HARAKA SANA,TUPANUE UKANDA WA UCHUMI WA BANDARI NA JIJI LETU TULIUNGANISHE NA BAGAMOYO.
 
Kigugumizi kinatoka wapi? Wekeni mkataba wazi, MOU, kama mnajadiliana mtuambie vipengele vya majadiliano ni vipi?

Kama ni mkataba mzuri, mtaungwa mkono na wengi.

Hatutaki ile mikataba ya kikoloni ya kina Chief Mangungo, mikataba ya kuuza nchi.
DAI MKATABA WA MAUZIANO YA NDEGE,NA MIKATABA YOTE YA KANDARASI YA FLY OVER NA KILA MRADI.
N.B,MRADI HUU NI MUHIMU KWA USTAWI WA TANZANIA YETU.
 
Kwa mama kila mradi wenye maslahi kwa wapiga dili utafanyika,JPM ni JPM.
Songs mbele rais wetu,tunahitaji miradi mingi zaidi ya aina hii,ili vijibwa vinavyopiga kelele watoto wao waje kupata AJIRA.
EVERYTHINGS IS FOR FUTURE GENERATIONS
 
Mikataba ya huo mradi iwekwe hadharani nani kashinda dhabuni na kandarasi tuwajue wanafanya kwa fedha za ndani aunza mkopo na masharti ya uanzaji na kumalizia hadi kuanza rasmi mradi kufanya kazi ni yapi. Yasomwe bungeni wabunge wetu japo wengi vilaza lakini yasomwe redioni na sisi wa huku SAMVU LA KUCHORE tujue tusije ambiwa mambo yamebuma kila mtanzania alipie mradi wachina wakisha utaifisha
 
Back
Top Bottom