Waziri Mwambe: Bei ya Mafuta ya Kula imepanda kutokana na ongezeko la bei kwenye Soko la Dunia iliyosababishwa na Corona

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,616
141,445
Waziri wa biashara Mh. Mwambe amesema bei ya mafuta ya kula imepanda kutokana na ongezeko la bei ya bidhaa hiyo kwenye soko la dunia.

Mwambe amesema bei kwenye soko la dunia imepanda kutokana na fakta mbalimbali kubwa ikiwa ni ugonjwa wa Corona.

Mwambe amesema kwa sasa kuna meli mbili za mafuta bandarini na uhalisia wa kupungua kwa bei kutaangaliwa baada ya mafuta hayo kupakuliwa.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama
 
Hahaha, Tanzania hakuna Corona Sasa inapandishaje Bei ya Mafuta?

Na anadai eti Kuna Meli ya Mafuta ilishwasili bandarini tangu Desemba 10 mwaka Jana hadi leo haijapakua Mafuta, hivi huu si ni Ujinga na Ulaghai?😅😅

Haiwezekani Meli ikae bandarini mwezi mzima kusubiri Kupakua shehena ya Mafuta, huo mzigo hautauzika Sokoni na mwenye mzigo hawezi tena kulipia Shipping costs wala marine charges za bandari.

Na kwa jinsi biashara ya bandari ilivyo na ushindani mkali siku ikitokea Meli zinasubiri mwezi mzima Kupakua shehena bandarini kama anavyotaka kutuaminisha Bwn Mwambe basi hakuna Meli zitakuja Bandari za Tanzania.

Mwambe aache Uongo wake

Viongozi waache Uongo!
 
Sasa si ndio wale wazalishaji wa mafuta wako njia ya Dodoma kutoka Moro wapige hela mpaka washangae
 
Ngoja tumuulize Kakoko!
Meli ikikaa sana ni siku 7 tu, tena Meli za Mafuta ndo hazikai kabisa kwa sababu siyo nyingi na zina dedicated berths, Kurasini Oil Jetty(KOJ) kwa meli ndogo za 5000 hadi 45000 Metric tons au SPM kule deep sea kwa meli kubwa za kubeba 150,000 Metric Tons,

Sasa hiyo Meli ya Mwambe ya kukaa miezi miwili kusubiri Kupakua shehena imewasili bandari ipi?
 
Waziri wa biashara Mh Mwambe amesema bei ya mafuta ya kula imepanda kutokana na ongezeko la bei ya bidhaa hiyo kwenye soko la dunia...
Huyu jamaa ni mwehu kabisa,bei ya soko la dunia inaathili vipi kilimo Chetu Cha mafuta?

Tatizo hapa ni kwamba hatuna uzalishaji wa kutosha wa mafuta hapa nyumbani tunategemea kuagiza nje,leo ni korona,kesho utakuwa Ugonjwa mwingine,

suluhisho hapa ni sera bora za kilimo,na uwekezaji katika uzalishaji wa mafuta,sio kujenga uwanja wa mpira chato,ofisi ya msd Chato,ofisi ya TRA Chato,
 
Back
Top Bottom