Waziri Mwalimu: Wanafunzi wanaopata ujauzito waendelee kusoma

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu amesisitiza kuwa wanafunzi wa kike wanaopata mimba wakiwa mashuleni waendelee na masomo yao, ili kufikia malengo walioyanayo nchini.

unnamed-45.jpg

Waziri Ummy ameyasema hayo leo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa masuala ya kijinsia ulioandiliwa na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu DUCE( Dar es Salaam University College of Education) alipomuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

“Tunapokataza watoto wa kike wasiendelee na masomo pindi wanapopata ujauzito wakiwa mashuleni, tunawaadhibu watoto wa masikini washindwe kutimiza malengo yao kwa wakati waliotarajia,”alisema Waziri Ummy.

Kwa upande wa Mkuu wa Chuo cha DUCE, Profesa William Anangisye amesema lengo la mkutano huo ni kuleta chachu ya kuwatia moyo wanafunzi wa kike kupenda masomo ya sayansi ili kupata wanasayansi wanawake nchini.

Chanzo: Bongo 5
 
Ameeeeeen! Leo ndio mnashtuka?Wajanja walishakuwa na plan B mapema, binti akipata mimba kabla shuleni hawajagundua walikuwa wanaomba uhamisho, anajichimbia kwa ndugu na kujifungua, mtoto analelewa na ndugu huku binti anaendelea na elimu yake.
Uzuri wa hawa mabinti waliopitia shida hii huwa ni "bookworms" wa hatari, hawatakagi kudanganyika mara ya pili!

Ngoja tusikie wenzetu wa imani ile ambayo inahimiza kuoana na kuzaana huku kipimo cha mke bora kikiwa ni kusema yes 24/7!
 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu amesisitiza kuwa wanafunzi wa kike wanaopata mimba wakiwa mashuleni waendelee na masomo yao, ili kufikia malengo walioyanayo nchini.

Waziri Ummy ameyasema hayo leo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa masuala ya kijinsia ulioandiliwa na Chuo Cha Ualimu (DUCE) alipomuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

“Tunapokataza watoto wa kike wasiendelee na masomo pindi wanapopata ujauzito wakiwa mashuleni, tunawaadhibu watoto wa masikini washindwe kutimiza malengo yao kwa wakati waliotarajia,”alisema Waziri Ummy.

Kwa upande wa Mkuu wa Chuo cha DUCE, Profesa William Anangisye amesema lengo la mkutano huo ni kuleta chachu ya kuwatia moyo wanafunzi wa kike kupenda masomo ya sayansi ili kupata wanasayansi wanawake nchini.

Chanzo: Bongo 5
Anawatia moyo kupnda masomo yasayansi????au ana halalisha ngono huyuu
 
Wakati tunasoma tulipotezwa vichwa vingi kwa mimba.
Sky, Bonde ni kitu cha kawaida mapenzi na mimba au nadanganya. Strange mtot anapata mimba wazazi wanashangilia kupata mjukuu, nimeona mwenyewe! It is true mlipoteza vichwa sana. Kwetu it was a rare thing , sasa vipo tele!
 
Shule za kata zimezalisha mimba nyingi sana.
 
Veeeery Goood, Excellent, hili swala lilikua linanikereketa sana unakuta aliyempa mimba anaendelea na masomo huku binti akizuiwa kuendelea na masomo. Hili mmenifurahisha sasa mjitahidi muwafutie na adhabu vijana wanaowapa hizo mimba, mana kusema na ule ukweli Mungu fundi jamani, unakuta ka student kamejazia vimapaja tena viko natural kabisa.
 
Ameeeeeen! Leo ndio mnashtuka?Wajanja walishakuwa na plan B mapema, binti akipata mimba kabla shuleni hawajagundua walikuwa wanaomba uhamisho, anajichimbia kwa ndugu na kujifungua, mtoto analelewa na ndugu huku binti anaendelea na elimu yake.
Uzuri wa hawa mabinti waliopitia shida hii huwa ni "bookworms" wa hatari, hawatakagi kudanganyika mara ya pili!

Ngoja tusikie wenzetu wa imani ile ambayo inahimiza kuoana na kuzaana huku kipimo cha mke bora kikiwa ni kusema yes 24/7!
24/7 ndiyo nn?
 
Na ndio maana kuna imani zingine wala hawana haja ya kutiana mimba bali wanaoana kabisa wanaume kwa wanaume sasa Sijui wanazaaje hapo
 
Hawa wanahitaji semina elekezi..... Suala linalohusu elimu anapaswa kulisemea Waziri wa elimu..... Waziri wa afya kutoa mwongozo kuhusu masuala ya elimu sidhani kama amefuata autaratibu. Pili.... Hivi hawa wanasiasa wetu, wanapotoa matamko kama haya huwa wameyatafakari kweli.?
 
Back
Top Bottom