Waziri Mwakyembe,vipi kuhusu mambo haya mawili? Ndiyo imetoka tena?

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,136
17,871
Waziri wa Katiba na Sheria,Daktari Harrison Mwakyembe tayari amewasilisha Bajeti ya Wizara yake. Wizara yake ndiyo inayohusika na masuala ya katiba na mahakama. Binafsi,sikusikia wala kuona mahali panapoonesha muendeleko wa mchakato wa katiba mpya wala uundwaji wa mahakama ya mafisadi.

Mambo hayo mawili yanahitaji sheria na bajeti yake. Bunge ndilo lenye kuombwa na kutoa au kuunda sheria na bajeti. Kuna ukimya juu ya mambo haya mawili. Mafisadi watashughulikiwaje bila ya mahakama mahsusi kwa ajili yao iliyoahidiwa? Vipi kuhusu katiba mpya?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Ruvuma)
 
Mahakama ya mafisadi! Hii siyo mhimu sana kama kuviwezesha vyombo vya uchunguzi -takukuru na polisi. Mahakama tunazo na zimepewa uwezo wa kusikiliza mashauri yote
 
Hata kwa akili ya kawaida tu unaweza ukaona kuwa haya ni miongoni mwa hadaa za CCM za kwa wapiga kura.....kama kuna watu wana matumaini ya kupata katiba mpya kutoka kwenye serikali hii ya CCM ni kama wanasubiria meli kwenye stendi ya bus.....
CCM kuja na katiba mpya ni sawa kujichimbia shimo yenyewe na kujizika......
 
Wanamuogopa Magu kuliko kitu chochote, CCM kwa unafiki hawajambo, ila ukimuona Nape, January na Kinana waambie tumewamisi sana bila kumsahau Mzee wa Ushahidi wa Mbinguni - Nchemba
 
Hivi mzee tupatupa hivi chama kina nguvu au MTU ndio ananguvu maana naona kuna unafiki upande wenu
 
Waziri wa Katiba na Sheria,Daktari Harrison Mwakyembe tayari amewasilisha Bajeti ya Wizara yake. Wizara yake ndiyo inayohusika na masuala ya katiba na mahakama. Binafsi,sikusikia wala kuona mahali panapoonesha muendeleko wa mchakato wa katiba mpya wala uundwaji wa mahakama ya mafisadi.

Mambo hayo mawili yanahitaji sheria na bajeti yake. Bunge ndilo lenye kuombwa na kutoa au kuunda sheria na bajeti. Kuna ukimya juu ya mambo haya mawili. Mafisadi watashughulikiwaje bila ya mahakama mahsusi kwa ajili yao iliyoahidiwa? Vipi kuhusu katiba mpya?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Ruvuma)
Kwa mwana ccm yeyote hataki kusikia habari za katiba mpya maana hii iliyopo wanaitumia kama kichaka cha kujifichia
 
yale yalikuwa ni ya kuombea kura tu! sasa wako busy kutumbua majipu
Mkuu tuliyasema sana lkn watu walitokwa na mapovu kukanusha,sasa nadhani ndiyo watajua kuwa ile ilikuwa ni kiingilio cha kutafutia kura
 
AMINI USIAMINI, KUKATISHWA KWA MISAADA KAMA HUU WA MCC kutaathiri mambo mengi sana muhimu japo yatafunikwa kama hivi. Kwani matumiz ya pesa LAZIMA yabanwe kuziba matundu yaliotokea baada ya misaada kusitishwa. Hili vijana wa Lumumba hawataliongelea kamwe.
 
Back
Top Bottom