Waziri Mwakyembe usifikirie kupunguza idadi ya wachezaji wa kigeni

Nov 21, 2018
29
26
Mheshimiwa Waziri wa Michezo nakuomba sana usifikirie Kupunguza idadi ya wachezaji wa kigeni kwenye timu zetu za ligi kuu.

Kwa hivi karibuni timu zetu za Simba na Yanga zimekuwa zikishindana katika kununua wachezaji wa nje kiukweli wapo ambao ukiwaona wanastahili kuitwa wachezaji wa nje ila kuna wengine kweli viwango vyao ni vya kawaida sana kama mshambuliaji wa yanga Yikpe, na Sibomana ni wa kawaida sana na pia simba mtu kama Shibob, nao uwezo wao wakawaida sana.

Jinsi wachezaji wabovu na wenye viwango vidogo wanavyosajiliwa:-

Kwanza kabisa viongozi wetu ndio wanaohusika na kusajili wachezaji wabovu kwa kutengeneza mazingira ya kupiga cha juu na ndio maana wanagombana sana na makocha kwa sababu kocha anataka mchezaji wa maana lakini wao wanaenda kuchukua garasa lao ili kutengeneza 10%.
Jinsi ya kuzuia wachezaji wenye viwango vibovu kuingia Bongo:-

1. Awe anacheza ligi kuu ya nchi husika au daraja la kwanza kwa nchi zinasohesabika sinasukuma kandanda kwelikweli.

2. Awe alishawahi kuchezea timu ya Taifa. yaani ndani ya miaka mitatu angalau ameitwa hata mara moja au mbili kuchezea au anaichezea timu ya taifa.

3. Kuongeza kodi kwa wachezaji wa kimataifa :- huku kutafanya timu kuwaza mara mbili kwamba wanamchukua mchezaji wanakuja kumlipa milioni ishirini kwa kipi.

4. Serikali Kufuatilia malipo ya mchezaji. Hapa kwenye kumnunua mchezaji kutoka timu moja kwenda nyingine ndipo huwa tunapigiwa. Mchezaji anaweza kuwa ana dhamani ya milioni 50 lakini kutokana na wapiga dili wanamfanya dhamani kuwa 100 ili wapate hapo cha juu sasa wizara inatakiwa ijue mchezaji kanunuliwa kiasi gani na pesa ilitoka kweli ikaingia kwenye acount ya hiyo timu?

Maboresho
Mwakembe tunakuomba boresha soka la vijana jenga vituo kila mkoa vya vijana kujifunza mpira na Faida yake utaiona tutakuwa na timu ya taifa nzuri na simba na yanga watavuna kutoka katika soka la vijana.

Weka ushindani timu moja ya vijana itengenezewe mazingira ya kucheza ligi kuu ambapo vijana wote wataandaliwa kutoka kwenye vituo na kutoa timu ya kucheza ligi kuu.

Kuwepo Na shule ya kufundisha Makocha wazawa chuo kabisa. na baada ya hapo waajiriwe katika secondary na shule za msingi.
 
Back
Top Bottom