Waziri Mwakyembe: Rushwa haina nafasi awamu hii ya tano

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,196
25,515
mwakyembe.gif

Waziri wa Katiba na Sheria,Mhe. Dr. Harrison Mwakyembe amesema kuwa rushwa na ufisadi havina nafasi katika awamu hii ya tano. Akifungua wiki ya Huduma za Kisheria, Waziri Mwakyembe amesema rushwa na ufisadi vina athari kubwa kwa jamii na nchi kwa ujumla. Amewaasa wananchi kutotoa wala kupokea rushwa.

Katika uzinduzi huo uliofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam,walikuwepo pia Waziri wa Utumishi, Mhe. Angela Kairuki,Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU,Kamishna Valentino Mlowola na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binaadamu,Mhe. Bahame Nyanduga.

Chanzo: ITV Habari
 
1480960401252.jpg
 
  • Thanks
Reactions: Gut
Kaishashiba kwa rushwa za wakati ile sasa NFO unasema kwasasa hazina nafasi. Mbona awamu iliyopita alikua hasemi hivyo. Maana YAKE alikua anachukua na ilikuwepo.?
 
Rushwa ya Elfu tano haina noma, Rais alishasema tuwape Trafiki police, hiyo ni ya ku-brush viatu vyao tu!
 
upload_2016-12-5_22-2-24.jpeg

upload_2016-12-5_22-2-47.jpeg

Atwambie hii kitu iko wapi? Hua natamani matamko ya wakuu wetu yangekua kweli au yanatekelezeka. Ni mafundi sana wa kauli lakini vitendo zero kabisa!
 
Wekeni picha yake (mwakyembe) tuone kama kweli yupo serious.
Sharti la picha ni Ile akiwa na ukurutu mwili mzima.
 
Nafikiri ile milioni 10 kwa wabunge wa CCM haikuwa rushwa, ilikuwa ni takrima.
 
Rushwa ni lazima iwe in monetary form? Je mtumishi akipambana usipofanya hivi utafukuzwa Siyo rushwa?
 
Back
Top Bottom