Waziri Mwakyembe: Rushwa haina nafasi awamu hii ya tano

Mtumishi akiambiwa usipofanya hivi (hata kama ni kinyume na sheria) utafukuzwa kazi ni rushwa au ni nidhamu kazini?
 
Rushwa ipo Kwa wingi tu. Kilichobadilika ni kuwa imepungua kwenye maofisi yao but mtaani ipo kama kawaida.
 
mwakyembe.gif

Waziri wa Katiba na Sheria,Mhe. Dr. Harrison Mwakyembe amesema kuwa rushwa na ufisadi havina nafasi katika awamu hii ya tano. Akifungua wiki ya Huduma za Kisheria, Waziri Mwakyembe amesema rushwa na ufisadi vina athari kubwa kwa jamii na nchi kwa ujumla. Amewaasa wananchi kutotoa wala kupokea rushwa.

Katika uzinduzi huo uliofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam,walikuwepo pia Waziri wa Utumishi, Mhe. Angela Kairuki,Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU,Kamishna Valentino Mlowola na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binaadamu,Mhe. Bahame Nyanduga.

Chanzo: ITV Habari
Rushwa ina nafasi kubwa katika Mahakama za mwanzo na Wilayaa kwani ni wimbo wa kila siku angekuwa anapitia hukumu zinazotolewa huko asingediriki kusema hivyo.
 
Back
Top Bottom