Waziri Mwakyembe na BASATA ongezeni umakini. Msanii Young Dee anawazidi akili na anachochea ujinga

Yani Bongo Hollywood yetu masaki daah kweli tupo bongo bahati mbaya tu karibu Ulaya
 
Wakuu aliye na mashairi...aweke.

Kazi ya sanaa sio ya kukurupukia title...
Huenda kilichoimbwa ni tofauti na mawazo ya mtoa mada...
 
Infantry Soldier,
Sasa kwani uongo? Nchi hii imekuwa ya CCM na vizazi vyao na sisi wengine tupo hapa TZ kwa bahati mbaya. Huyu Dogo anahitaji kupongezwa na kupewa tuzo kafikiria sana. Ni wajinga wachache tu kama wewe unao ona wimbo huu haufai.
 
Ninavyofaham mm 'Tueur de Lion' uzalendo daima huwa unakuwa accelerated na uwiano sawa wa hali za maisha kwa watu wote ktk taifa na mgawanyo sawa wa rasilimali za taifa.Kilichopo hapa Tz kwa hiv sasa kuna watu ni matajir including people from the politic block,na hawa watu utajir wao umetokana na kuiibia serikali au kuwaibia Common people na hawafanyi kaz yoyote ya maana tofauti na kuongea kwa maana rahis hawazalishi chochote kwa ustawi wa jamii...lakn watu wa tabaka chini wanafanya kaz nzito kwa masaa mengi kwa ujira MDOGO na bado wakpata ulemav,magonjwa na hata kupunguzwa kazn (Redundancy).

wengi huwa huwa hawapewi fedha za kwenda kuanzishia maisha huko waendako.Vlevle hawa watu wa hali ya chini sana pamoja na kulizalishia taifa bado wengi wanaishi kwenye vjumba hafifu na visivyo hata na umeme wakati watoto wao wanasoma saint kayumba au Swahili medium schools, kwa hali hii ww mtoa mada unadhani patakuwepo na uzalendo?

Ww unamlaumu huyo Dogo (Young Dee), kwa huo wimbo wake wa Bongo bahati mbaya, lakn nataka utambue ya kwamba hayo ni matokeo ya mabaya yote yaliyowahi kutendwa na yanayotendeka kwenye taifa letu.Haiwezekani mkulima wa nchi hii akawa na maisha mabov na mwanae kukosa mkopo wa elimu ya juu halaf akawa na uzalendo na taifa lake
 
Ukisoma mashahiri utaelewa nini nasema, huyu ajaponda huyu katetea bongo na ndio mana anasifia viunga vya bongo vyote, yeye katumia sana ya maneno na wjainga wasio tafakari wanshindwa kumuelewa.

Sijuhi huko shule mnasoma nini.
 
Mkuu mbona dogo ameeleweka sana kiana Fulani kaisifia bongo yetu huoni kuna sehemu anasema wanaogopa kusema lakini hapa ndo home, na yupo Happy!
 
Infantry Soldier,

Msanii anatumia uhuru wake wa kikatiba wa kujieleza.

Ibara ya 18 ya katiba inasema.

18.-(1) Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati.

(2) Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala muhimu kwa jamii.


Sasa huyo msanii kwa kutoa mawazo yake amevunja sheria gani?

https://www.bugando.ac.tz/attachments/Katiba_ya_Tanzania.pdf
 
Back
Top Bottom