Waziri Mwakyembe na BASATA ongezeni umakini. Msanii Young Dee anawazidi akili na anachochea ujinga

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
4,357
2,000
Habari za asubuhi members wa JF.

Kuna siku Jumamosi ile ya wiki iliyopita nikiwa ninafunga ubuyu kwenye mfuko na kuchomea na kibatari kwa ajili ya kwenda kuuza kwa wanafunzi pale shule ya Rutihinda nikasikia wimbo unaimbwa eti 'Tupo Bongo Bahati Mbaya' nikawauliza wadogo zangu niliokuwa nao karibu wakasema eti Kuna msanii anajiita Young Dar es Salaam (Young Dee) ndio ameimba tupo bongo bahati mbaya.

Na sasa kila kijana mpaka madereva wa boda boda wanaimba eti wapo hapa bongo bahati mbaya.

Waziri wa Habari, Vijana na Utamaduni, Mzee Mwakyembe pamoja na BASATA wanajua nyimbo kama hizi zinaua that sense of patriotism kwenye akili za vijana taratibu taratibu.

Vijana wanaanza kuichukia nchi wangali wadogo sana. Wanapandikizwa mentality mbovu na serikali inaona lakini bado wapo kimya tu hakuna wanachofanya. Sijui hawajausikia huu wimbo ama wameamua kuupotezea tu.

Ninawasilisha mada. Mimi mropokaji tu wahusika fanyieni kazi hili.Infantry Soldier,

Msanii anatumia uhuru wake wa kikatiba wa kujieleza.

Ibara ya 18 ya katiba inasema.

18.-(1) Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati.

(2) Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala muhimu kwa jamii.


Sasa huyo msanii kwa kutoa mawazo yake amevunja sheria gani?

https://www.bugando.ac.tz/attachments/Katiba_ya_Tanzania.pdf
 

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
3,950
2,000
Wengi tungepata chance ya kuchagua tuzaliwe wapi tusingechagua bongoo..

Tupo bongo kwa bahati mbaya tu..

Umeona wapi vigezo vya bosi ni kujua kusoma na kuandika.. huku subordinate vigezo ni degree, masters, phd etc.....

Yaani mjinga anasimamia msomiii eti

Waziri anakwambia kuwa na cherehani 4 ni kiwanda eti.. huku wenzetu wanatengeneza hadi ndege na meliiiii... sisi kila kitu tumetengenezewa na wenzetu wenye akili
 

leonaldo

JF-Expert Member
Oct 26, 2014
1,856
2,000
Ila mi bro nawalaani kwa juhudi zote wanaJF kwa kufunga kurasa mbili bila kusapoti uzi wako, pamoja na hayo lazima ujue kuwa kontena lililokuwa limebeba patriotism ya Tanzania liliangukia pale kwenye kona za mangungo treat, iliniuma sana. Kwani hadi leo halijapata mtu wa kulinyanyua,ila tu juzi ndio nikasikia crane toka IPTL ndo inaomba tuipe miaka miwili linyanyuke hadi mlma Kilimanjaro du!!!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom