Waziri Mwakyembe kutumia mshahara wake kuhakikisha anawafunga waliomdhulumu Mzee Majuto mamilioni

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
25f13a42e80fa1bc92420c4af074dcd0.jpg
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Harrison Mwakyembe amefunguka na kusema kuwa Mzee Majuto amedhulumiwa pesa milioni 25 na kampuni ya filamu ambayo jina lake amelihifadhi na kudai atatumia hata mshahara wake kuhakikisha anawafunga watu hao.

Mwakyembe amesema hayo leo Oktoba 27, 2017 alipokutana na wasanii mbalimbali kujadili changamoto za kazi ya sanaa nchini na kusema katika vitu ambavyo atapambana navyo ni pamoja na watu wanaowadhulumu wasanii haki yao na kuwaibia kazi zao za sanaa.

"Nilipopita Tanga nilikutana na msanii nguli wa filamu Mzee Majuto nilikwenda kumjulia hali na bahati nzuri saizi anaendelea vizuri, Mzee Majuto akaniomba kitu kimoja na kuniambia naumwa nahitaji pesa lakini nimeshafanya kazi na kampuni hii akanionyesha na kuwa ameshatengeneza filamu zaidi ya 100 na kampuni hiyo kwa mkataba wa kulipwa fedha ndogo tu shilingi milioni 25 lakini huu ni mwaka wa pili hajalipwa hata senti tano sasa hayo ndiyo mambo ambayo sifurahii, nimeshapeleka taarifa kwa hiyo kampuni tukutane Dar es salaam na Dodoma asipokuja tunajua njia za kumsafirisha kwenye Kalandinga mpaka Dodoma, huu ni wizi kama wa kwenda kumchomolea mtu mfukoni", alisisitiza Mwakyembe.

Waziri Mwakyembe aliendelea kufafanua kuwa kwa sasa yupo tayari kutumia pesa zake mfukoni kuhakikisha Mzee Majuto anapata haki yake kwa kazi mbalimbali alizofanya na kampuni hiyo.

"Mzee Majuto alikwenda Mwanza na familia ule mzigo, meneja kwa kumuheshimu akamfuata na kumwambia hiyo cheki hata senti tano hakuna na cheki iliyobaundi ni kosa la jinai, tunachezea watu hivi. Mzee Majuto amekaa Mwanza zaidi ya miezi sita anahangaika kuzipata hizo pesa, na mimi niko tayari nitatumia hata mshahara wangu twende mahakamani tufunge watu tumeshachoka huko ni kudharau watu", alisema Mwakyembe.

Waziri Mwakyembe alimtembelea msanii huyo nguli nyumbani kwake ambapo alikwenda kumjulia hali baada ya kupata taarifa kuwa anaumwa.
 
Utajiri wa dhuluma hua haufiki mbali hata siku moja,ogopa sana pesa ya kumdhulumu Masikini..
 
Sasa huyu Waziri anaficha nini hii kampuni kwanini asiisanue tu.. Hii tabia ya siri nilidhani labda kwenye mikataba ya siri, kumbe hata kuibiwa napo
 
Atakuwa namna gani billionaire ilhali unasikia kuwa kazi zao nyingi wanadhulumiwa na kuibiwa?
Ili swala la kuibiwa kazi zao sijawai kuliamini kwa sababu wanauza haki zao kwa msambazaji (steps) sasa wanaibiwaje wakati kazi wanapeleka wenyewe si bora mtu ujisambazie mwenyewe
 
Ili swala la kuibiwa kazi zao sijawai kuliamini kwa sababu wanauza haki zao kwa msambazaji (steps) sasa wanaibiwaje wakati kazi wanapeleka wenyewe si bora mtu ujisambazie mwenyewe
Sasa ikiwa kampuni moja tu imemdhulumu ml25 je yakiwa makampuni 20 huo utajiri utapatikana vipi?
 
Back
Top Bottom