Waziri Mwakyembe kutumia mshahara wake kuhakikisha anawafunga waliomdhulumu Mzee Majuto mamilioni


Ghazwat

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Messages
17,647
Likes
51,682
Points
280
Ghazwat

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2015
17,647 51,682 280
25f13a42e80fa1bc92420c4af074dcd0.jpg
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Harrison Mwakyembe amefunguka na kusema kuwa Mzee Majuto amedhulumiwa pesa milioni 25 na kampuni ya filamu ambayo jina lake amelihifadhi na kudai atatumia hata mshahara wake kuhakikisha anawafunga watu hao.

Mwakyembe amesema hayo leo Oktoba 27, 2017 alipokutana na wasanii mbalimbali kujadili changamoto za kazi ya sanaa nchini na kusema katika vitu ambavyo atapambana navyo ni pamoja na watu wanaowadhulumu wasanii haki yao na kuwaibia kazi zao za sanaa.

"Nilipopita Tanga nilikutana na msanii nguli wa filamu Mzee Majuto nilikwenda kumjulia hali na bahati nzuri saizi anaendelea vizuri, Mzee Majuto akaniomba kitu kimoja na kuniambia naumwa nahitaji pesa lakini nimeshafanya kazi na kampuni hii akanionyesha na kuwa ameshatengeneza filamu zaidi ya 100 na kampuni hiyo kwa mkataba wa kulipwa fedha ndogo tu shilingi milioni 25 lakini huu ni mwaka wa pili hajalipwa hata senti tano sasa hayo ndiyo mambo ambayo sifurahii, nimeshapeleka taarifa kwa hiyo kampuni tukutane Dar es salaam na Dodoma asipokuja tunajua njia za kumsafirisha kwenye Kalandinga mpaka Dodoma, huu ni wizi kama wa kwenda kumchomolea mtu mfukoni", alisisitiza Mwakyembe.

Waziri Mwakyembe aliendelea kufafanua kuwa kwa sasa yupo tayari kutumia pesa zake mfukoni kuhakikisha Mzee Majuto anapata haki yake kwa kazi mbalimbali alizofanya na kampuni hiyo.

"Mzee Majuto alikwenda Mwanza na familia ule mzigo, meneja kwa kumuheshimu akamfuata na kumwambia hiyo cheki hata senti tano hakuna na cheki iliyobaundi ni kosa la jinai, tunachezea watu hivi. Mzee Majuto amekaa Mwanza zaidi ya miezi sita anahangaika kuzipata hizo pesa, na mimi niko tayari nitatumia hata mshahara wangu twende mahakamani tufunge watu tumeshachoka huko ni kudharau watu", alisema Mwakyembe.

Waziri Mwakyembe alimtembelea msanii huyo nguli nyumbani kwake ambapo alikwenda kumjulia hali baada ya kupata taarifa kuwa anaumwa.
 
stephot

stephot

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2012
Messages
6,644
Likes
4,431
Points
280
stephot

stephot

JF-Expert Member
Joined Mar 1, 2012
6,644 4,431 280
Utajiri wa dhuluma hua haufiki mbali hata siku moja,ogopa sana pesa ya kumdhulumu Masikini..
 
Ghazwat

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Messages
17,647
Likes
51,682
Points
280
Ghazwat

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2015
17,647 51,682 280
Sasa huyu Waziri anaficha nini hii kampuni kwanini asiisanue tu.. Hii tabia ya siri nilidhani labda kwenye mikataba ya siri, kumbe hata kuibiwa napo
 
Ghazwat

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Messages
17,647
Likes
51,682
Points
280
Ghazwat

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2015
17,647 51,682 280
Utajiri wa dhuluma hua haufiki mbali hata siku moja,..
Aliyezoea kudhulumu haangalii kufika mbali, yeye madamu amempata hitaji lake. Ukweli dhulma ni mbaya hakika.
 
Tajirimsomi

Tajirimsomi

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2017
Messages
4,635
Likes
4,750
Points
280
Age
48
Tajirimsomi

Tajirimsomi

JF-Expert Member
Joined Jan 12, 2017
4,635 4,750 280
Hela za mboga katengeneza sema ni mpenda bebez sana wakipigika ndy wanakumbuka wanaowadai

Ova
Uyu hawezi pigika katengeneza movie nyingi zitamlipa mpaka kufa mambo ya hakimiliki
 
Tajirimsomi

Tajirimsomi

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2017
Messages
4,635
Likes
4,750
Points
280
Age
48
Tajirimsomi

Tajirimsomi

JF-Expert Member
Joined Jan 12, 2017
4,635 4,750 280
Atakuwa namna gani billionaire ilhali unasikia kuwa kazi zao nyingi wanadhulumiwa na kuibiwa?
Ili swala la kuibiwa kazi zao sijawai kuliamini kwa sababu wanauza haki zao kwa msambazaji (steps) sasa wanaibiwaje wakati kazi wanapeleka wenyewe si bora mtu ujisambazie mwenyewe
 
LUCKY BANANA

LUCKY BANANA

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Messages
470
Likes
220
Points
60
LUCKY BANANA

LUCKY BANANA

JF-Expert Member
Joined Jun 28, 2016
470 220 60
mshahara wake unatunikaje sasa naombeo maelezo?
 
Zanika

Zanika

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
1,058
Likes
584
Points
280
Zanika

Zanika

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2015
1,058 584 280
Pole Majuto. Mungu akujaalie upine
 
Zanika

Zanika

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
1,058
Likes
584
Points
280
Zanika

Zanika

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2015
1,058 584 280
Ili swala la kuibiwa kazi zao sijawai kuliamini kwa sababu wanauza haki zao kwa msambazaji (steps) sasa wanaibiwaje wakati kazi wanapeleka wenyewe si bora mtu ujisambazie mwenyewe
Na hiyo cheque fake aliyopewa unaisrmeaje?
 
Tajirimsomi

Tajirimsomi

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2017
Messages
4,635
Likes
4,750
Points
280
Age
48
Tajirimsomi

Tajirimsomi

JF-Expert Member
Joined Jan 12, 2017
4,635 4,750 280
Na hiyo cheque fake aliyopewa unaisrmeaje?
Uko sitaki kwenda sema natakaga kujua wanapodai kazi zao zinaibiwa na wakati hakimiliki wanamuuzia step uwa wanamanisha nini
 
Ghazwat

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Messages
17,647
Likes
51,682
Points
280
Ghazwat

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2015
17,647 51,682 280
Ili swala la kuibiwa kazi zao sijawai kuliamini kwa sababu wanauza haki zao kwa msambazaji (steps) sasa wanaibiwaje wakati kazi wanapeleka wenyewe si bora mtu ujisambazie mwenyewe
Sasa ikiwa kampuni moja tu imemdhulumu ml25 je yakiwa makampuni 20 huo utajiri utapatikana vipi?
 
Saint Ivuga

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Messages
45,357
Likes
31,571
Points
280
Saint Ivuga

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2008
45,357 31,571 280
mshahara wake hagusagi huyo itakuwa
 

Forum statistics

Threads 1,235,092
Members 474,351
Posts 29,212,003