Waziri Mwakyembe, hili linakuhusu na ni muhimu kuzingatia

CHA The GREAT

JF-Expert Member
Nov 11, 2010
652
1,000
Kwamba, kumekuwa na tabia ya watu kurusha picha/video za wafu, au marehemu kwenye mitandao ya kijamii kama vile facebook n.k.. Kadhalika, picha za watu walioathirika na magonjwa kama vile cancer na mengineyo ya kutisha. Binafsi, huwa sipendezwi na tabia hii ya Watanznia wenzangu, ya kurusha picha za wafu. Picha au video hizo zinarushwa si kwa idhini ya marehemu au ndugu na jamaa za marehemu, bali kwa kiherehere cha watu ambao akili zao zinawaza kuwa kila picha, kila tukio ni sawa kuwekwa kwenye mitandao ya kijamii.

Mheshimiwa Waziri, huko Westminster, Uingereza, kulitokea ajali ya moto kwenye jengo la Grenfell, tarehe 14/6/2017, ambapo iliripotiwa vifo vya watu wapatao 70. Kama tabia ya Watanzania wengi wanaotumia mitandao ya kijamii ilivyo, Mtanzania mwenzetu anayeishi huko, alijikuta akipiga picha ya watu waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo na kuziweka kwenye mtandao wa kijamii wa facebook. Mtanzania huyo kwa majina ya Omega Mwaikambo (43), kutokana na kitendo chake hicho, alijikuta kwenye mkono wa sheria, ambapo alishitakiwa na kuhukumiwa miezi mitatu jela kwa kitendo chake hicho ambacho kwa kweli si cha kiungwana.

Mheshimiwa Waziri, natambua wewe ndiye mwenye dhamana ya wizara inayohusika na mambo ya habari ambapo mitandao ya kijamii ni sehemu yake. Sina hakika na sheria yetu inasemaje juu ya vitendo vya watu kurusha picha ambazo ni za udhalilishaji, au kurusha picha za watu bila idhini ya watu husika, sina hakika sheria inasemaje juu ya watu wanaorusha picha za watoto wadogo kabisa ambao kimsingi hawatoi idhini ya picha zao kurushwa, sina hakika, sina hakika. Na kwa kuwa sina hakika, naomba wizara yako iliangalie hili la baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii kurusha picha za wafu au watu walioathirika na magonjwa, mfano cancer na mengineyo ili wachukuliwe hatua kali ili iwe fundisho kwa walio na tabia kama hiyo.

Nawasilisha.
JUSTICE FOR GRENFELL: Man who posted grim Facebook photos of dead victims JAILED

mwaikambo.jpg
 

Perfectz

JF-Expert Member
May 17, 2017
7,211
2,000
Lazima kuwe na sheria inakayosimamia jambo hili.Huwezi mkamata mtu halafu akifika mahakamani ahukumiwe kwa kifungu kipi cha sheria??!!!
 

Kazetela

JF-Expert Member
Nov 12, 2016
1,613
2,000
2ef5cb60e84759d07014a0eae6fed87a.jpg
Mtanzania Ahukumiwa Jela Kwa kuweka picha ya mtu aliyefaki kwa moto Facebook.

Mwanaume mmoja anayedaiwa kuwa ni Mtanzania amehukumiwa kifungo cha miezi mitatu jela nchini Uingereza kwa kosa la kurusha katika ukurasa wake wa Facebook, picha za mtu aliyefariki dunia kutokana na moto uliounguza jengo la ghorofa la Mnara wa Grenfell lililopo nchini humo.

Pia, mtu huyo ametakiwa kulipa faini ya Sh579,880 kwa mwathirika wa tukio hilo.Mtanzania huyo, Omega Mwaikambo (43) alituma video na picha za mwili wa marehemu uliokuwa kwenye begi na baadaye picha nyingine tano zikionyesha uso wa marehemu huyo.

Gazeti la mtandaoni la The Telegraph limeandika kuwa Mwaikambo amekiri makosa ya kutuma mara mbili picha zisizopendeza kwa umma katika mitandao ya kijamii mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Westminster jana.

Mwaikambo ambaye anaishi hatua chache kutoka lilipo jengo la Grenfell akifanya shughuli za upishi, alishuhudia jinsi jengo hilo lilivyoungua moto usiku na alikuwa ni miongoni mwa wapishi waliowapikia chai wafanyakazi wa zimamoto walipokuwa wakizima moto huo.
48a8dbe669fb310e38bcaf8602835795.jpg

“Lakini juzi Jumatano asubuhi alipoangalia miili hiyo nje ya nyumba yake alichukua picha kwa kutumia simu yake aina ya iPad na kuzipakia kwenye mtandao wake wa Facebook,” liliandika gazeti hilo.
Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Tom Little amesema; “Anaishi karibu zaidi na mnara wa Grenfell, kama ambavyo mahakama inajua janga hilo lilitokea Juni 14.”

Akitoa hukumu, Jaji wa mahakama hiyo, Tanweer Ikram amesema; “Dunia nzima imeshtushwa na yaliyotokea hapa kutokana na janga la moto, ni hali ya kutisha isiyostahimilika, wafu ni lazima waheshimiwe.”

Ameongeza; “Ulichokifanya kupakia hizo picha kwenye Facebook ni dhahiri kuwa hujaonyesha heshima kwa waathirika wa tukio hilo, kuonyesha uso wake hadharani ni kosa kubwa na halielezeki.”

Mpaka sasa watu zaidi ya 30 wanadaiwa kufariki dunia kutokana na moto uliounguza jengo hilo refu na maarufu Magharibi mwa Uingereza.
e91fcb54b518d9567be55170ba43938a.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom