Waziri Mwakyembe aiagiza BMT ya Tenga kuzuia ubinafsishaji wa klabu za wanachama

escrow one

JF-Expert Member
Nov 29, 2014
547
1,000
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison George Mwakyembe ameutaka uongozi mpya wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kuhakikisha vyama na klabu hawabinafsishi vyama na klabu wanazoziongoza na hivyo kuwavunja mioyo wanachama wao.
Waziri Mwakyembe ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi baraza la 14 la michezo la Taifa leo mjini Dar es Salaam, sherehe ambazo zilihudhuriwa na viongozi wapya wa BMT, akiwemo Mwenyekiti, Leodegar Chilla Tenga, Waziri Mwakyembe amesema Serikali imewateua kwa kuzingatia umakini na uwezo wa kila mmoja wakiwa na malengo ya kuongeza ufanisi wa chombo hicho muhimu katika usimamizi wa Maendeleo ya Michezo nchini.

“Mmeteuliwa ili kuleta mabadiliko makubwa katika Sekta ya Maendeleo ya Michezo. Kazi kubwa mnayokwenda kuifanya imefafanuliwa vyema katika Sheria inayounda Baraza la Michezo la Taifa, ambayo ni Sheria ya Bunge Na. 12 ya mwaka 1967 na marekebisho yake Namba 6 ya mwaka 1971,”amesema na kuongeza kwamba sheria hiyo imeaainisha vema kazi na wajibu wa BMT katika kuendeleza michezo nchini.

“Baraza hili litapewa majukumu ya ziada au ya nyongeza kutokana na hali halisi ya michezo ilivyo kwa sasa hapa nchini. Nyongeza hii, itatokana na ukongwe wa Sheria yenyewe, hali inayosababisha baadhi ya kazi kushindwa kutekelezeka kama inavyotarajiwa hivyo yanahitajika maelekezo ya ziada,”amesema.

Amezitaja kazi za nyongeza ambazo zinahitaji utekelezaji wa haraka ni pamoja na kuanzishwa kwa Mfuko wa Maendeleo ya Michezo nchini ambao utakuwa na vyanzo endelevu vya mapato na Mwakyembe amesema ili kufanikisha jambo hilo, lazima vyanzo vya mapato vya kisheria viboreshwe na vyanzo vipya vibuniwe na kuanzishwa ili kumudu majukumu mapana ya BMT.

“Kwa mfano, moja ya chanzo cha mapato ya BMT ni asilimia kumi (10%) ya bei ya kiingilio ya tiketi katika michezo yenye viingilio. Hili halijawahi kutekelezwa na Baraza. Vilevile, ukusanywaji wa maduhuli kutoka katika Michezo ya Bahati Nasibu ya Taifa haufuatiliwi,”.
Mambo mengibe aliyioyataja Waziri huyo makini ni;

“2. Kuendelea kufanya Mapitio ya Sheria iliyounda BARAZA ili kuwa na Sheria inayoendana na hali halisi pamoja na matakwa ya Maendeleo ya Michezo ya leo Tanzania na Duniani kote,”.

3. Chini ya Uongozi wako pamoja na timu uliyonayo hakikisheni mnafanya Mikutano na Wadau wa Michezo katika ngazi za Mikoa na Wilaya kubaini changamoto zao na kufuatilia maendeleo yao. Hivi sasa Mikoa na Halmashauri zote zimejitahidi kuajiri Maafisa Michezo, ambapo kazi yao ni kusimamia na kuhamasisha michezo katika ngazi hizo za Mikoa na Wilaya,”.
“Iwapo kutakuwa na mipango endelevu ya Maendeleo ya Michezo katika ngazi ya Taifa (BARAZA) hadi Wilaya ambako ndiko chimbuko la vipaji vya michezo na mipango hiyo ikisimamiwa vilivyo kwa ushirikiano baina ya BMT, Mikoa na Wilaya, ni dhahiri tutapata maendeleo mazuri katika Sekta ya Michezo. Ili kufanikiwa katika jambo hili, ninaliagiza Baraza lako kuhakikisha kuwa linaongeza ushirikiano kwa kupitia Vikao na Mikutano yenye tija kwa Mikoa na Wilaya zote,”.

4. Kutoa mafunzo ya Utawala bora na namna nzuri ya kuongoza Vyama na Mashirikisho ya Kitaifa ili kupunguza changamoto mbalimbali ikiwemo migogoro isiyo ya lazima na kuleta ustawi katika kuendeleza michezo nchini,”.

“5. Nina matarajio makubwa chini ya uongozi wako, kwamba kwa mara ya kwanza BARAZA litatekeleza matakwa ya Sheria ya kuandaa tarifa kila mwaka za utendaji na shughuli za BARAZA ambazo, kwa mujibu wa Sheria, zikiwasilishwa kwangu, na mimi naziwasilisha Bungeni,”.

“6. BARAZA lihakikishe kuwa vyama vya michezo vinaheshimu Katiba zao kwa kuheshimu VIPINDI VYA UONGOZI na KUFANYA UCHAGUZI muda unapofika. Tuhakikishe kuwa viongozi hawabinafsishi vyama wanavyoviongoza na hivyo kuwavunja moyo wanachama wao. Natuhakikishe kuwa viongozi wa vyama vya michezo (Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Waweka Hazina hawashiki nafas iza uongozi zaidi ya MOJA kwenye vyama tofauti katika aina moja ya mchezo,”.

Mwakyembe amesema anaweza kuendelea kuagiza utekelezwaji wa kazi nyingine nyingi, lakini anaamini hizi chache pamoja na zile zilizopo katika Sheria ya BMT zikitekelezwa vizuri, Maendeleo ya Michezo hayawezi kuwa ndoto ya mbali sana.

source: Bin Zubeiry Online
 
Mchochezi

JF-Expert Member
Feb 29, 2012
8,284
2,000
Simba na Yanga ni mali za Serikali.

Japo haijaandikwa sehemu lakini ndio ukweli huo.
 
LAPTOP2016

JF-Expert Member
Oct 20, 2016
734
1,000
Hivi BMT inatambuliwa na FIFA or CAF?? kama wanachama wameamua kwa ridhaa yao serikali inakua inawashwa washwa nini? Yanga hao wanachama wameshindwa kuendesha club serikali imesaidia nini?? Sheria za FIFA zaniakataza serikali kuingilia vilabu, huyu ujasiri huu anautoa wapi??? Mfano FIFA wakasema kwa kua serikali inaingilia vilabu haitavitambua hivyo vilabu serikali itakua imefaidika nini?? Sisi wanamsimbazi tumeamua kwa moyo mmoja team apewe Mo aiendeshe kibiashara, wao inawakera nini??
 
escrow one

JF-Expert Member
Nov 29, 2014
547
1,000
Hivi Mwakyembe ashafunua mioyo yetu na kuona jinsi ilivyovunjika kwa aina ya uendeshaji wa hizi timu?? juzi tu hapa wachezaji wa timu pendwa wamegoma ila ye anaona sawa tu.
 
nankumene

JF-Expert Member
Nov 12, 2015
5,920
2,000
Hivi BMT inatambuliwa na FIFA or CAF?? kama wanachama wameamua kwa ridhaa yao serikali inakua inawashwa washwa nini? Yanga hao wanachama wameshindwa kuendesha club serikali imesaidia nini?? Sheria za FIFA zaniakataza serikali kuingilia vilabu, huyu ujasiri huu anautoa wapi??? Mfano FIFA wakasema kwa kua serikali inaingilia vilabu haitavitambua hivyo vilabu serikali itakua imefaidika nini?? Sisi wanamsimbazi tumeamua kwa moyo mmoja team apewe Mo aiendeshe kibiashara, wao inawakera nini??
Sheria za nchi ziko palepale mkuu hata kwe nchi zilizoendelea ukitaka kubinafsisha club kuna taratibu za kufuatwa kulingana na sheria ya nchi husika
 
Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
7,150
2,000
Sisi wanachama na wapenzi wa klabu ya Simba hatukubaliani na Mwakyembe. Timu yetu tunaibinafsisha kwa Mo ili mkwanja wa kuendeshea timu uwepo na uwe wa uhakika.

Duniani kote timu zilizo na mafanikio ni zile zilizo chini ya matajiri.

Mwakyembe akizingua tunaenda kumshitaki FIFA
 
fofre

JF-Expert Member
Nov 16, 2016
735
1,000
Hivi BMT inatambuliwa na FIFA or CAF?? kama wanachama wameamua kwa ridhaa yao serikali inakua inawashwa washwa nini? Yanga hao wanachama wameshindwa kuendesha club serikali imesaidia nini?? Sheria za FIFA zaniakataza serikali kuingilia vilabu, huyu ujasiri huu anautoa wapi??? Mfano FIFA wakasema kwa kua serikali inaingilia vilabu haitavitambua hivyo vilabu serikali itakua imefaidika nini?? Sisi wanamsimbazi tumeamua kwa moyo mmoja team apewe Mo aiendeshe kibiashara, wao inawakera nini??
Timu zikichukuliwa na matajiri/wawekezaji watakosa pa kujichotea fedha, ki ukweli yan sisi wapenda soka kwa nchi yatu ya Tanzânia tusahau kuona simba na yanga Zikiwa na maendeleo kisoka.
Mfano hai ni kuhusu swala la kuzibinafsisha timu kwa wawekezaji, hivi kwa akili zao Kuna mtu mwenye akili timamu awekeze fedha alafu asiwe na mamlaka não. Hili swala la mwekezaji kuwa na asilimia 49 na wanachama 51% linaakisi mambo Mengi Sana.
 
fofre

JF-Expert Member
Nov 16, 2016
735
1,000
Sisi wanachama na wapenzi wa klabu ya Simba hatukubaliani na Mwakyembe. Timu yetu tunaibinafsisha kwa Mo ili mkwanja wa kuendeshea timu uwepo na uwe wa uhakika.

Duniani kote timu zilizo na mafanikio ni zile zilizo chini ya matajiri.

Mwakyembe akizingua tunaenda kumshitaki FIFA
Hili tusahau ndugu yangu, kwanza ukae ukijua serikali haipendi simba na yanga ziendelee, hiv ushajiuliza hizo timu Zikiwa na viwanja vyao, watapata wapi mapato na uwanja wao taifa si utadoda.
 
Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
7,150
2,000
Hili tusahau ndugu yangu, kwanza ukae ukijua serikali haipendi simba na yanga ziendelee, hiv ushajiuliza hizo timu Zikiwa na viwanja vyao, watapata wapi mapato na uwanja wao taifa si utadoda.
Duuh! Bora ningezaliwa paka Ulaya
 
muafi

JF-Expert Member
Oct 6, 2015
1,387
2,000
Huyu mwakyembe kwenye hii wizara no mzigo
Hajui hats namna ya kukuza soka

Hill ndio tatizo la kugawiwa vyeo
 
bene michael

Senior Member
Mar 1, 2017
130
225
yeah hizi timu zina nguvu sana
Hawana shida na MO. Hawawezi kuona Simba inabadilisha mfumo kabla Yanga haijajitayarisha. Kwa wenye kumbukumbu za miaka 1975, turejee kwa nini kwa ajili ya mgogoro wa Yanga, alifukuzwa nchini marehemu Tambwe Leya wa Zaire, Kocha wa Yanga, na kocha mpendwa wa Simba marehemu Nabi Kamara wa Guinea Conackry? kwa visingizio mgogoro wa yanga ulikuwa na harufu ya kisiasa, ooh makocha wa nje ni wachochezi......
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom