Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Mimi namkubali sana Waziri wa Nishati na Madini, Waziri Muhongo kwa uendeshaji wake wa hiyo Wizara sema nafikiri tatizo kubwa alilonalo ni kwamba haeleweki na baadhi ya watu, na mengi anayoyasema ni kweli kabisa ila tatizo baadhi ya watu amabo ni simple minds wanatafsiri vibaya!
Kwa mfano suala la kuwanyima akina Mengi vitalu vya Gesi, hili ni sawa kabisa kwani hawana uwezo wa kuviendeleza hivi vitalu na walichotaka kufanya ni kuvihodhi halafu kuja kuviuza baadaye kwa makampuni makubwa sasa kama ni hivyo ni kwa nini Serikali isifanye yenyewe?
Kwangu mimi chini ya Uongozi wa Waziri Muhongo, Wizara ya Nishati na Madini imefanya mambo mengi sana yanayoonekena na yale yasionekana kama vile watoto wengi wa Kitanzania kupewa udhamini kwenda kusomea Mafuta na Gesi ndani na nje ya nchi, uboreshwaji wa ufanisi wa Tanesco jambo lililopelekea hivi karibuni kushushwa kwa gharama ya Umeme na mengine mengi sana, hivyo Waziri Muhongo ni moja kati ya hazina kubwa ya viongozi tuliyo nayo Tanzania.
Kwanza kwangu mimi naona hata ilikuwa sawa alivyoukosa u CEO wa UNESCO kwa maana kama angeupata leo hii kama nchi tusingefaidika na ujuzi na weledi wake ambao tunauhitaji sana!