Waziri Muhongo uko wapi uumalize mgawo wa umeme?

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,278
25,846
Mgawo wa umeme unaendelea kurindima hapa Tanzania,hususani jijini Dar es Salaam. Mgawo wa umeme umekuwa kero sugu nchini. Umeme unakatika na hata wananchi wamezoea huku wakiumia kiuchumi na kijamii.

Waziri wa Nishati na Madini,Prof. Sospeter Muhongo uko wapi uumalize mgawo huu? Au kero hii imeshindikana kutatulika?
 
Huu uzi tangu juzi wamegoma kuchangia mkuu,wanachungulia na kusepa,maana yake ni kuwa hawakubaliani na ulichoandika,naomba ujirekebishe please.......
 
Dr Kalemani (naibu waziri wa nishati na madini) juzi alikuwa Geita na akampa meneja TANESCO mkoa masaa 24 kuhakikisha umeme haukatiki ktk mkoa wake na wilaya zake!!

Alimwambia ukikatika basi na yeye na mameneja waje wengine wakatike moja kwa moja (wajifukuzishe kazi) yaani asisubiri kuja kukatwa na yeye!!

Kidogo nilicheka na agizo hili lakini nikasema acha watu waji - magufulishe tu!!
 
Mgawo wa umeme unaendelea kurindima hapa Tanzania,hususani jijini Dar es Salaam. Mgawo wa umeme umekuwa kero sugu nchini. Umeme unakatika na hata wananchi wamezoea huku wakiumia kiuchumi na kijamii.

Waziri wa Nishati na Madini,Prof. Sospeter Muhongo uko wapi uumalize mgawo huu? Au kero hii imeshindikana kutatulika?
Bado hamjateua Waziri kivuli wa NISHATI na madini !? Halafu neno stahiki ni MGAO na sio MGAWO.
 
Mgawo wa umeme unaendelea kurindima hapa Tanzania,hususani jijini Dar es Salaam. Mgawo wa umeme umekuwa kero sugu nchini. Umeme unakatika na hata wananchi wamezoea huku wakiumia kiuchumi na kijamii.

Waziri wa Nishati na Madini,Prof. Sospeter Muhongo uko wapi uumalize mgawo huu? Au kero hii imeshindikana kutatulika?
hapa Arusha umeme unakatika kila siku kuanzia saa mbili mpaka saa kumi na mbili hasa sehemu ya Ngaramtoni. hivi huo umeme wa gesi unafanya kazi?
 
Back
Top Bottom