Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Waziri Muhongo amesikika akiwaambia walio chini yake kwamba wizara inahitaji watendaji makini na wale ambao wanajiona hawana viwango waondoke. Ni kauli nzuri lakini ushauri wangu kwake ni kwamba atazame namna ambavyo anaweza kutengeneza mfumo wa kikazi ambao utamuwezesha kupata mrejesho wa kazi wa TANESCO (feedback) kutoka kwa watendaji wa kata, ambao wapo karibu na wananchi moja kwa moja.
Hawa watendaji walio chini yake huweza kuweka siasa na kumtaarifu kile ambacho wanajua atapenda kukisikia. Watafanya hivyo ili kulinda vibarua vyao visiote nyasi. Kuna matatizo ya line za mitaa. Unakuta mtaa mmoja kuna nyumba nne zenye umeme halafu mtaa huo huo kuna nyumba sita ambazo hazina umeme, yaani unakatika saa tatu asubuhi unarudi saa moja usiku. Watanzania wengi huchukua mikopo kutoka kwenye taasisi mbalimbali za fedha, hivyo kuna masharti ya urudishaji wa mikopo hiyo. Watanzania wengi wanaishi maisha ya kujiajiri ambayo kwa kweli ni ya kuungauunga. Hivyo sio jambo jema mtu anashindwa kufanya biashara kwa sababu ya umeme halafu akiitazama nyumba inayofuata inao umeme, akiuliza anaambiwa line yake ina matatizo.
Waziri Muhongo nakuomba tengeneza aina ya mfumo wa kikazi ambao utakuwezesha ukapata mrejesho kutoka kwa watendaji wa kata, ili waweze kukupatia picha halisi ya shida za umeme. Sisemi kwamba usiwategemee maafisa wa kanda, nachosema ni kuwa ipo haja ya ofisi yako kupata taarifa zilizo kamili ili uweze kujipanga vyema katika kutatua kero za umeme.