Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,279
- 25,857
Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo amewataka watanzania kukubaliana na ukweli kuwa mikataba yote ya umeme iliyopo hapa nchini ni mibaya. Waziri Muhongo ameyasema hayo alipokuwa akijibu changamoto zilizoelekezwa katika Wizara yake katika Mkutano wa Baraza la Taifa la Biashara, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Hatahivyo,Waziri Muhongo hakufafanua kuhusu wahusika wa mikataba hiyo;mikataba husika na namna ya kuifanya iwe mizuri. Mtakubaliana nami kuwa mikataba ya umeme kati ya TANESCO na Makampuni ya kuzalisha umeme imekuwa ikizalisha kashfa za kifisadi pamoja na kesi mbalimbali za jinai na madai kwa miaka mingi sasa.
Nini kifanyike?