Waziri Muhongo kutoa Suzuki Carry kama ambulance huo ni utani

Nshonzi

JF-Expert Member
Jul 19, 2016
3,046
1,867
Jana Profesa Muhongo ametoa msaada wa aliyoyaita ambulance magari aina ya isuzu carry, huu ni zaidi ya utani kama ule uliotokea kipindi kilichopita walivyoamua kutuletea bajaj eti ni ambulance. Kweli hii serikali ya CCM inatuona watanzania kama ni wasio na ufahamu.

===========

PROF. Muhongo asherehekea siku ya kuzaliwa kwa namna yake

WhatsApp-Image-20160625-1024x768.jpeg


Atoa magari matano ya wagonjwa


Roli moja
Vitabu 22,000 kwa Shule zote za msingi na Sekondari, Kuwaletea wabunge wenzake bila kujali itikadi ya vyama.
Aahidi madawati 8000, kesho kukabidhi 1,812.
Aleta Madaktari Bingwa kutoka China.

MBUNGE wa Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, leo tarehe 25 Juni 2016 ameadhimisha siku yake ya kuzalisha kwa namna tofauti kabisa huku chakula cha mchana kikiwa ugali na sato.

Prof Muhongo ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Madini, ameiadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa kuwakaribisha Madaktari Bingwa kutoka China.
Madaktari hao bingwa watatoa matibabu na dawa bure kwa wanavijiji jimboni humo kwa siku mbili kuanzia leo.
Katika siku hiyo ya kuzalia iliyoadhimishwa kwa aina yake, Prof Muhongo amegawa zaidi ya vitabu 22,000 kutoka Marekani (thamani: US $ 250,000), sawa na TSh500m.
Vitabu hivyo vimesambazwa katika shule za msingi 108 na Sekondari 20.

Lunch ya UGALI NA SATO
Katika sherehe hiyo, Profesa Muhongo aliandaa chakula cha mchana, ambapo yeye na wageni waalikwa walikula ugali na sato katika kijiji cha Kigera.

Waziri Muhongo aliitumia siku hiyo kukabidhi vitu mbalimbali alivyoahidi wakati wa kampeni ya uchaguzi wa Rais na Wabunge uliofanyika Oktoba mwaka jana.

Jimbo la Musoma Vijijini limekuwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na afya, elimu, barabara na mabadiliko ya tabia nchi.
Kufuatia mwaliko wa Waziri Muhongo, Madaktari Bingwa Sita kutoka nchini China wako jimboni na tayari wameanza kutoa huduma ya matibabu kwa wananchi wa jimboni humo.

Madaktari hao wameanza kutoa huduma hiyo katika Zahanati ya Mugango iliyopo kijiji cha Nyangoma, ikiwa ni awamu ya pili kufuatia huduma kama hiyo kutolewa na Madaktari wengine kutoka China mwezi Machi mwaka huu.

Akizindua huduma hiyo ya matibabu Awamu ya Pili, Profesa Muhongo alisema huduma hiyo ni bure na wananchi hao hawatalipia matibabu hayo yanayotolewa leo na kesho.


Profesa Muhongo alisema Madaktari hao wamebobea katika magonjwa ya Wanawake, Watoto, Meno, Vinywa na koo.
Aliongeza kwamba Madaktari wengine ni mabingwa wa macho, kisukari, presha, tumbo na upasuaji wa uvimbe kichwani na tumboni.

“Nimeleta rafiki zangu kutoka China na watawatibu kwa muda wa siku Mbili,” alisema Prof Muhongo.
Aliwaambia wananchi hao kuwa Madaktari hao wanaojitolea walikuja na rafiki zao kutoka China ambao wamewaletea kalamu na vitabu.


“Wamewaletea vitabu vya Sayansi, Hisabati, na Kiswahili, kwa ajili ya kugawa katika shule tano za Msingi, pamoja na mipira itakayogawiwa katika shule hizo na pia kwa timu za mpira za vijiji hivyo,” alisema Mbunge huyo msomi wa jiolojia.

WhatsApp-Image-201606252-1024x768.jpeg


Profesa Muhongo alisema kuwa vitabu hivyo vyenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 500, vimetolewa msaada na marafiki zake kutoka Marekani.


“lengo langu ni kuhakikisha kuwa wananchi katika Jimbo hili mnaelimika na kujenga utamaduni wa kujisomea, hivyo mbali na wanafunzi wetu, hata wananchi mnakaribishwa kuja kuvisoma,”alisema Profesa Muhongo.


Naye Mwakilishi kutoka Ubalozi wa China hapa nchini, aliyejulikana kwa jina la Bw Zhang, alisema kuwa uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi za Tanzania na China ndiyo umewafanya Madaktari hao kuja nchini kutoa huduma za matibabu.

“Ushirikiano wetu unazidi kupanuka na wanachi wengi wa China wanakuja Tanzania kufanya biashara, hali kadhalika wananchi wa Tanzania wanaenda China kwa masuala ya Bishara na Utalii, kwa ushirikiano huu tutazidi kuupanuka katika nyanja za kiuchumi,” alisema Zhang.


Alisema kuwa hadi sasa kuna Madaktari zaidi ya 20 kutoka China wanaotoa huduma za utabibu nchini ambao wapo katika mikoa ya Dar es Salaam, Tabora, Mara na Dodoma.


“Hii yote inatokana na urafiki na undugu uliopo kati ya nchi hizi mbili, uliojengwa na Mwalimu Nyerere na Mao Tse Ntung,” aliongeza.


Wakati huohuo Profesa Muhongo amezindua ugawaji wa vitabu zaidi ya 22,000 katika Shule za Msingi na Sekondari za Jimbo la Musoma vijijini. Uzinduzi huo umefanywa katika shule ya msingi Kwibara katika kata ya Mugango.
Mbunge huyo alisema kuwa shule zote za msingi 108 na Sekondari 20 jimboni humo zatapata vitabu hivyo.


“Kila shule ya msingi itapata maboksi ya vitabu mawili huku kila shule ya sekondari ikipata maboksi 16,” alifafanua.


ATOA LORI NA MAGARI YA WAGONJWA
WhatsApp-Image-201606251-1024x575.jpeg



Profesa Muhongo alisema kuwa katika kutimiza ahadi zake, amewapelekea wananchi wa jimbo laki gari aina ya Canter.
Gari hilo litatumika kwa ajili ya katika shughuli za misiba, ujenzi wa shule, maabara na vituo Vya Afya.
Tayari Mbunge huyo ameshatimiza ahadi yake ya gari la kubebea wagonjwa ambapo mwezi Machi, 2016 alikabidhi Gari hilo kwa hospitali ya Murangi.
“Leo nawataarifu kuwa baada ya wiki mbili nitawaletea gari nyingine 4 za kubebea wagonjwa na zitagawanywa katika zahanati za Kurugee iliyoko kata ya Bukumi na Zahanati ya Masinono iliyoko kata ya Bugwema.
Gari nyongine za wagonjwa zitapelekwa katika Zahanati ya Mugango katika kata ya Mugango na Zahanati ya Nyakatende katika kata ya Ifulifu.

VITABU VINGINE VINAKUJA

Vilevile alisema kuwa bado kuna vitabu vingine vinavyoendelea kuletwa nchini ambapo awamu nyingine ya tatu inategemewa kufika mwezi Agosti mwaka huu.

Baadhi ya vitabu hivyo atavigawa katika Majimbo mengine ya Mkoa wa Mara bila kubagua itikadi ya Chama kwani wananchi wote wana haki ya kupata maendeleo.

Alisema awamu ya 4 ya vitabu inategemewa kufika nchini mwezi Octoba, 2016.

“Mbunge wetu ameanza na kasi kubwa, ndani ya miezi sita ametimiza ahadi zake na kuzidi, huyu Bwana ni mchapakazi na atatufikisha mbali sana,” alisema Nyambarilo.

Chanzo: Chanel Ten
 
Jana muhongo ametoa msaada wa aliyo yaita ambulance magari aina ya isuzu cary, huu ni zaidi ya utani kama ule uliotokea kipindi kilicho pita walivyo amua kutuletea bajaj eti ni ambulance kweli hii serikali ya ccm inatuona watanzania kama ni wasio na ufahamu
mbona hivi sasa ndio zinazotumika
 
Ccm wanawadharau sana,afadhali hiyo suzuki cary mkuu,watawapa trekta
Teeeeeeeeh teeeeeeeeh teeeeeeeeeh mkuu wewe ni kiboko yaani mgonjwa anapandishwa kwenye trekta
 
Huwezi amini mkuu nashabeba sana wamama wajawazito na wagonjwa kwenye trekta,na ndo wajinga wanaoipa kura ccm kila mwaka,na si waonei huruma haswa linapokuja swala la malipo
Hutakiwi kuwaonea huruma mkuu maana wameamua wenyewe kuishi maisha hayo
 
better something than nothing

hata hivyo Tanzania tunawapa wabunge majukumu yasiyo yao
 
Kama ni kweli tumpongeze,kazi hiyo sio yake alitakiwa kuchochea maendeleo jimboni mwake kwa kuliwakilisha vizuri bungeni sasa kama ametoa hayo kaonesha moyo wa kujali sana juhudi za maendeleo pamoja na kwamba bado tuna safari ndefu,Au tumuhukumu sababu ni WAZIRI?
 
Jan Profesa Muhongo ametoa msaada wa aliyoyaita ambulance magari aina ya isuzu cary, huu ni zaidi ya utani kama ule uliotokea kipindi kilichopita walivyoamua kutuletea bajaj eti ni ambulance. Kweli hii serikali ya CCM inatuona watanzania kama ni wasio na ufahamu.

Something is better than nothing.Ulitaka watu waendelee kubeba waja wazito kwenye baiskeli? au Ulitaka atoe mercedes benz kama za ikulu kama ambulance? Hizo gari alizotoa ni four wheel drive zinafaa kwa jimbo lake ambalo miundombinu yake barabara zake sio za lami,.Ambulance yaweza uwa gari yoyote hata trekta kutegemea mazingira. Cha muhimu ijengewe bodi lenye huduma zote zinazotakiwa za kitabibu ndani ya hiyo gari
 
Hakuna kitu kinaitwa Isuzu Carry. Ipo Suzuki Carry. Weka picha kama sio uzushi
Sawa mkuu maana waliyo sema kuwa elimu haina mwisho walikuwa na maana yao kwa mambo kama hayo
 
Back
Top Bottom