Waziri muhongo aitaka TPDC na wabia kuongeza kasi katika uwekezaji wa kiwanda cha gesi kimiminika

News TZ

Senior Member
Jun 17, 2015
127
69
Muhongo+PHOTO.jpg

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Muhongo ametaka kasi iongezwe katika mradi wa ujenzi wa kiwanda cha uchakataji na usindikaji wa gesi kimiminika unaotarajiwa kuanza mkoani Lindi mara baada ya taratibu za maandalizi kukamilika.

Profesa Muhongo alisema hayo katika kikao kwa ajili ya kujadili hatua iliyofikiwa ya maandalizi ya ujenzi wa kiwanda hicho kilichoshirikisha watekelezaji wa mradi huo ambao ni Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) na makampuni yanayojishughulisha na shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi nchini.

Makampuni ya utafiti wa mafuta na gesi yanayotekeleza mradi huo ni pamoja na Shell, Statoil, Ophir Energy, Pavilion na Exxon Mobil. Pia kikao hicho kilishirikisha watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST)

Mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kuchakata na kusindika gesi kimiminika Profesa Muhongo alilitaka shirika la TPDC kushirikiana kwa karibu na makampuni ya utafiti wa mafuta na gesi yanayotekeleza mradi huo na kwa kasi ya haraka ili mradi huo uweze kukamilika kwa wakati.

Profesa Muhongo alisema Tanzania ina utajiri mkubwa wa gesi hivyo ni vyema watekelezaji wakachangamkia fursa hiyo ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata na kusindika gesi kimiminika ambayo mahitaji yake ni makubwa duniani hususan katika bara la Asia.

“Ifikapo mwaka 2025 inategemewa kuwa mahitaji ya gesi duniani yatakuwa ni kiasi cha tani milioni 440 kwa mwaka hususan katika nchi za Asia ambazo ni karibu na Afrika, hii ni fursa ambayo tunatakiwa kuichangamkia ili kuendana na soko itakapofika kipindi hicho,” alisema Profesa Muhongo.

Profesa Muhongo aliendelea kusema kuwa gesi ya kimiminika imekuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi zinazoendelea huku akitolea mfano wa Algeria ambayo ni nchi ya kwanza duniani kwa kuwa na kiwanda cha kuchakata na kusindika gesi kimimika ambayo kwa sasa imepiga hatua kubwa kimaendeleo.

Katika maandalizi ya awali ya mradi huo, Profesa Muhongo aliagiza uundwaji wa timu kwa ajili ya maandalizi ya mradi huo ikishirikisha wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Fedha, Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), taasisi mbalimbali pamoja na wawakilishi kutoka katika makampuni yanatofanya utafiti wa gesi na mafuta nchini ambayo ni mtekelezaji wa mradi huo.

Alisisitiza kuwa ni vyema timu hiyo ikawa na wataalam wenye uzoefu mkubwa watakaofanya kazi kwa weledi na kukamilisha kazi hiyo kwa wakati.Aliagiza kuwa timu hiyo kukamilisha taratibu zote za maandalizi kabla ya mwezi Novemba, mwaka huu.

Naye Mkurugenzi Mtendaji kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Dkt. James Mataragio alisema kuwa shirika lake limekuwa likishirikiana na wabia wa ujenzi wa kiwanda hicho katika hatua zote za maandalizi ya awali na kuahidi kuongeza kasi ili kazi hiyo iweze kukamilika kwa wakati.

Chanzo: Dar waya
 
Kama nahisi kaharufu ka maendeleo Tz,,,, bt cjui yatamia maana drama ni nyingi,,
 
Wazawa wasiishie kunawa katika hili maana mabaharia wanalia kila siku.
 
Kwa mradi mkubwa kama huo, ambao major stakeholders ni makampuni makubwa ya mafuta na gesi duniani, lazima wana mpango kabambe na kasi ya kuuendeleza ni priority namba moja. Anachosema Waziri ni kama kocha wa Barcelona kumwambia Messi aongeze kasi akifika goli kwenye 18 ya Arsenal
 
Back
Top Bottom