Waziri Mponda, Dk. Nkya wajiweka kando na madaktari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Mponda, Dk. Nkya wajiweka kando na madaktari

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Mar 29, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 29, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda


  Tangu kumalizika kwa mgomo wa madaktari wa hospitali za umma ambao walikuwa wanashinikiza kujiuzulu kwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda na naibu wake, Dk. Lucy Nkya, mawaziri hao wamejiweka kando katika shughuli za kitaifa zinazowahusu madaktari.

  Dk. Mponda na Dk. Nkya wanalalamikiwa na madaktari kwamba wameshindwa kuiongoza Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na kwamba wamechangia katika mgomo wa madaktari ulionza Januari mwaka huu.


  Mgomo huo uliowahusisha madaktari wa hospitali za umma ulisababisha kusimamishwa kazi kwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Blandina Nyoni, na Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Deo Mtasiwa, Februari 9, mwaka huu.

  Hatua ya kuwasimamisha ilitangazwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ili tuhuma dhidi yao zichunguzwe, na kusema kuwa suala la Dk. Mponda na Dk.

  Nkya litashughulikiwa na Rais Jakaya Kikwete.

  Madaktari waligoma tena Machi 7 hadi 9, mwaka huu wakishinikiza viongozi hao wafutwe kazi huku wakiwatangaza kuwa ni maadui wao.
  Hata hivyo, tangu kumalizika kwa mgomo huo, baada ya madaktari kukutana na Rais Jakaya Kikwete, mawaziri hao hawaonekani katika shughuli za kitaifa zinazohusisha madaktari.

  Baadhi ya shughuli ambazo viongozi hao hawakukuhudhuria ni maadhimisho ya siku ya Utepe Mweupe wa Uzazi Salama iliyofanyika jijini Dar es Salaam Machi 15 mwaka huu katika viwanja vya Mnazi Mmoja, ambapo mgeni rasmi alikuwa mke wa Rais, Salma Kikwete.

  Kwa kuwa shughuli hiyo iliihusu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, alitakiwa kuwepo Dk. Mponda au Dk. Nkya kama viongozi wakuu wa wizara kwa ajili ya kuwa mwenyeji wa mke wa rais.

  Mratibu wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama Tanzania, Rose Mlay, alisema katika maadhimisho hayo walimualika Waziri Mponda na Dk. Nkya, lakini viongozi hao walitoa udhuru kwa Salma Kikwete kwamba wasingeweza kuhudhuria katika shughuli hiyo.

  Hata hivyo, haikuweza kufahamika ni udhuru gani uliwapata viongozi hao wawili kwa wakati mmoja na wizara kuwakilishwa na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Regina Kikuli.

  Aidha, Dk. Mponda na Dk. Nkya hawakuweza kuhudhuria katika mkutano wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno uliofanyika wiki mbili zilizopita jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais Jakaya Kikwete.

  Daktari wa Upasuaji kinywa na meno wa Hospitali ya Muhimbili, Baraka Kileo, alisema hawakuweza kumwalika waziri Mponda na naibu wake kutokana

  na mgogoro uliokuwa unaendelea kati ya adaktari juu ya viongozi hao ambao walikuwa wanatakiwa kujiuzulu.

  Alipoulizwa kuhusiana na kutoonekana katika shughuli zinazowahusu madaktari, Dk. Nkya, alisema kuwa hakuwepo ofisini kwa wiki moja na alikuwa nje ya Mkoa wa Dar es Salaam hivyo hawezi kujua kama alipelekewa mialiko.

  “Nilikuwa katika Kazi nyingine pindi matukio hayo yakitokea, nilikuwa nje ya Dar es Salaam kwa muda wa wiki moja na siyo lazima nihudhurie matukio yote, kuna watendaji wengine ambao wanaweza kuhudhuria matukio kama hayo,” alisema Nkya.

  Kwa upande wake, Waziri Mponda alisema hakupewa mwaliko wowote.

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. H

  Huihui2 JF-Expert Member

  #2
  Mar 29, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Haya mambo yamekwisha, naina vyombo vya habari vinataka viuze magazeti yao tu.
   
 3. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Dr Nkya alikuwa na kiburi cha ajabu na majibu ya kiserikali na dharau sasa wahamishiwe wizara za ajabu ajabu huko alikotokea kwa Sofia mama nonihino!!
   
Loading...