Waziri Mpina: Wasingechoma moto vifaranga ningewafukuza wote

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Waziri wa Ufugaji na Uvuvi Luhaga Mpina amesema serikali ilichoma moto vifaranga 6000 kutoka Kenya ili kuzuia magonjwa ya ndege na kuteketeza mtaji wa aliyevileta ili kama kuna njia nyingine alizokuwa anatumia kuingiza vifaranga kutoka nje ya nchi hawezi kurudia tena

Na amesema askari waliohusika kamawasingechoma moto vifaranga vile, basi angewafukuza wote

[/MEDIA]

Hii ni zaidi ya roho mbaya, yaani Serikali imekuwa kama mtu binafsi duuh..
 
Mh. Naibu waziri angefukuza kwani yeye ni mwajiri...aseme ningeshauri mamlaka za juu/muajiri awasimamishe kazi..Muongozo kutoka wizara ya Utumishi unahitajika Kwa viongozi Mwajiri mkuu ni Rais na Katibu mkuu Kiongozi full stop...

Mawaziri na Manaibu waziri wajue kuwa wao si wajiri kumfukuza mtu kazi si rahisi hivyo inabidi wapewe semina elekezi...serikali italipa fidia nyingi Mbele ya safari sheria ni msumeno masuala ya kitaalam yasiendeshwe kisiasa .. .2006 adi 2017 means ndio vifaranga wa kwanza kuingizwa?

Hapo kuna mtu alienda bank akakopa leo mtaji anapataje fedha za kulipa Bank..nazan diplomasia iliitajika na walitakiwa wapimwe au wapatiwe chanjo Kwa gharama za mhusika ila si kuteketeza mtaji wa binadamu mwingine..
 
Hivi mtu ukipewa Uwaziri akili zinafyatuka siyo! ninamkumbuka huyu jamaa wakati akiwa Mbunge wa kawaida alivyokuwa anajinasibu kutetea wananchi wake!
Kelele zote ilikuwa ni gia ya kutaka naye aonekane. Na hili ni tatizo kubwa linaloikabili nchi yetu. Watu wanapewa uwaziri kwa kuangalia jinsi wanavyopiga kelele na sio kwa merit. Majirani zetu waliliona hili ndiyo maana wabunge ni wapipa kelele wasioweza kuwa mawaziri na mawaziri ni watu wanaowajibika kwa bunge toka nje ya bunge.
 
Waziri wa Ufugaji na Uvuvi Luhaga Mpina amesema serikali ilichoma moto vifaranga 6000 kutoka Kenya ili kuzuia magonjwa ya ndege na kuteketeza mtaji wa aliyevileta ili kama kuna njia nyingine alizokuwa anatumia kuingiza vifaranga kutoka nje ya nchi hawezi kurudia tena

Na amesema askari waliohusika kamawasingechoma moto vifaranga vile, basi angewafukuza wote

Mwenye vifaranga angekuwa mtu wa Chato wangevichoma moto?
 
Waziri wa Ufugaji na Uvuvi Luhaga Mpina amesema serikali ilichoma moto vifaranga 6000 kutoka Kenya ili kuzuia magonjwa ya ndege na kuteketeza mtaji wa aliyevileta ili kama kuna njia nyingine alizokuwa anatumia kuingiza vifaranga kutoka nje ya nchi hawezi kurudia tena

Na amesema askari waliohusika kamawasingechoma moto vifaranga vile, basi angewafukuza wote

Hii yoote ni kumfurahisha mkuu!
 
Hivi mtu ukipewa Uwaziri akili zinafyatuka siyo! ninamkumbuka huyu jamaa wakati akiwa Mbunge wa kawaida alivyokuwa anajinasibu kutetea wananchi wake!
Acheni siasa kama hao vifaranga wangekuwa na ugonjwa wowote mngesema serikali sio makini. Sasa mnalalama. Ujinga sana. Prevention is better than cure. Iko siku mtaelewa.
 
Mbona ng'ombe waliokamatwa walipigwa mnada..? Hawakuweza kuwa na magonjwa wao..? Mbona hawakupimwa kabla..? Na hao vifaranga kwanini wasipimwe..? au kwanini wasirudishwe walikotoka kwa gharama za muingizaji..? Sheria haina ukatili kwa wanyama.. Na waziri anajisifia kabisa wamefanya hivyo ili kumfilisi huyo mfanyabiashara asiweze tena kufanya biashara.. Ukiwa na akili za matope tuuu ndo unaweza kusapoti ujinga huu uliofanywa..
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom