Waziri Mpina: Operation Sangara imeongeza tatizo la rushwa Kanda ya Ziwa

Zygot

JF-Expert Member
Apr 14, 2016
2,238
2,866
Kuna kiongozi wa CHADEMA amewahi kusema bungeni juu ya mwenendo wa kushughulikia mambo ya wizara ya uvuvi kwa operations. Pamoja na waziri Mpina kuitetea wizara yake, kumbukumbu yangu inaonesha hakuna operation ambayo imewahi kufanikiwa bila matatizo kwa wananchi, bahati mbaya wanaoendesha operation hizo huwa wanapewa kinga kwa uharifu wao hata kama ni nje ya kazi zao. Ilikuwa hivyo kwa Operation Tokomeza Sasa nimeishuhudia Operation Sangara ya bwana Mpina.

Nataka nizungumzie operation sangara ambayo imegeuka kuwa kichaka cha rushwa kwa kanda ya Ziwa. Kuna ufisadi bado unaendelea kwa jina la operation hiyo. Wilaya zote OCD na polisi wake, wakuu wa wilaya na maafisa uvuvi sasa wana mradi wa kudumu wa kuchukuwa rushwa.

Ninazo taarifa za ndani kutoka kwa afisa mwaminifu kwa ushuhuda wake kwa wilaya maarufu kwa uvuvi, Ukerewe. Bado nyavu aina ya makokoro zinatumika kinyume na Operation Sangara. Operation imekuwa ni mtaji kwa mkuu wa Wilaya, OCD na afisa uvuvi wa hamashauri. Polisi wanatumika hukusanya pesa toka kwa kila anayendesha uvuvi haramu na kuziwakilisha kwa OCD ambaye naye huwasiliana na mkuu wa wilaya. Polisi wamekuwa wakishinda barabarani kukusanya pesa kwa waendesha bodaboda wanaosafirisha samaki wadogo, wasioruhusiwa kuvuliwa.

Tatizo langu ni kwa viongozi wa serikali kama huyu mkuu wa wilaya ya Ukerewe na OCD. Inakuwaje aruhusu vitendo hivi haramu kuendelea badala ya kuzuia? Kibaya zaidi ukabila wa mkuu wa wilaya unatumika kujinasibu kwamba rais Magufuli ni ndugu yake. Ndiyo nini hiyo? Yaani mtu anakula rushwa kwa undugu na rais? Nadhani bado hatujapata watu wenye ubora wa kuwa wakuu wa wilaya.

Wakati haya yanatendeka, afisa usalama wa wilaya yupo. Je, anaripoti nini juu ya utendaji wa mkuu huyu wa wilaya? Je, ni mshirika ktk vitendo hivi? Matendo haya yote yanafanyika kwa kisingizio cha polisi wala rushwa, ukweli ni kwamba, polisi wameruhusiwa na wakuu wao kwa wilaya zote za kanda ya ziwa, Bunda, Musoma, Sengerema, Geita na ajabu hata Chato!
 
Ni huyu huyu au mwingine?
Naibu Waziri Mabula Aingilia Kati Mgogoro Kati Ya Mapadri Na DC Ukerewe - Kahama FM
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ameagiza kufanyika utambuzi wa mipaka sambamba na kuweka alama katika eneo lenye mgogoro wa ardhi kati ya Kanisa Katoliki, wananchi na shule ya msingi ya Kagunguli iliyopo wilaya ya Ukerewe mkoa wa Mwanza.

Uamuzi huo unafuatia kuibuka mgogoro kati ya Mapadri wa Kanisa Katoliki na Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Cornel Magembe kuhusu umiliki wa sehemu ya eneo la shule ya msingi Kagunguli jambo lililosababisha Mapadri kuandika waraka wa kutoshirikiana na mkuu huyo wa wilaya.

Akizungumza katika kikao cha utatuzi wa mgogoro huo uliohusisha Mapadri, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya na Serikali ya Kijiji jana wilayani Ukerewe mkoani Mwanza Dkt Mabula alisema maamuzi yote yaliyotolewa nje ya utaratibu kuhusiana na mgogoro huo ni batili na usubiriwe utambuzi wa mipaka ya eneo lenye mgogoro.

‘’ Wizara itatuma timu ya wataalamu ili kutafuta ufumbuzi wa mgogoro kwa kubainisha na kutambua mipaka ya hapa eneo Kagunguli na kuja na ufumbuzi wa kudumu’’ alisema Dkt Mabula.

Mkuu wa wilaya ya Ukerewe Cornel Magembe aliweka wazi kuwa, mgogoro uliopo katika eneo linalohusisha shule ya Sekondari Kagunguli inayomilikiwa na Kanisa Katoliki umechochewa kwa kiasi kikubwa na Mkuu wa shule ya Sekondari Kagunguli Padri Johanes Nawachi kwa kile anachodai padre huyo eneo la shule yake kuvamiwa.
 
Bandiko lako limekosa ushahidi mkuu, onyesha ushahidi wa moja kwa moja jinsi Polisi anavyopokea Pesa mpaka imfikie DC, Ukiweza taja majina ya Mtandao wote kama una nia njema. Vinginevyo unatetesi za vijiweni
 
Kuna baadhi ya Maandiko hulenga sana kutoa Ishara ya kinachoendelea....ningumu kukuta MTU ana tunga kitu chenye Masilahi kama iki.
Bandiko lako limekosa ushahidi mkuu, onyesha ushahidi wa moja kwa moja jinsi Polisi anavyopokea Pesa mpaka imfikie DC, Ukiweza taja majina ya Mtandao wote kama una nia njema. Vinginevyo unatetesi za vijiweni
So kuwepo ushahidi au kutokuwepo..Vyombo husika vianze kuchukua hatua zakufatilia.

Hii itasaidia haya..

1-kama nikweli basi wahusika watajulikan.

2-kama ni uongo, itatia Hofu na kuongeza Uadilifu kwa walotajwa kwa wao kuendelea kujua kua Jicho linawatizama.

NB..Jicho sio hili mnalolijua la MMU
 
kanda ya ziwa kula samaki ni haramu, hakuna sehemu yenye sheria za hovyo kama hiyo kanda.
Siyo kweli, isipokuwa kuna vipimo vya samaki wanaostahili kuvunwa na kutumika kama kitoweo usipotoshe. Njoo hapa Villa Park mitaa ya Kirumba ule sato na Ugali wa Donna saaafi.
 
Bandiko lako limekosa ushahidi mkuu, onyesha ushahidi wa moja kwa moja jinsi Polisi anavyopokea Pesa mpaka imfikie DC, Ukiweza taja majina ya Mtandao wote kama una nia njema. Vinginevyo unatetesi za vijiweni
Kuna wakati nashindwa kuelewa maana ya 'thinking' Hivi wewe ni mtu mzima kwa umri? Hayo uliyoandika kuna thinking? Yaani ushahidi unaotafuta ni ule wa kusubilia askari awe anachukuwa rushwa halafu umpige picha? Dah! Labda kama hukuwa nchini wakati wa matukio haya yote.

Hawa ni watu walioweza kuingia hata jiko la mgahawa, Dodoma na kuanza kupima urefu wa samaki mbichi. Nasema hayo ili uone kiwango ya upuuzi wa hiyo iliyoitwa operation.
 
Siyo kweli, isipokuwa kuna vipimo vya samaki wanaostahili kuvunwa na kutumika kama kitoweo usipotoshe. Njoo hapa Villa Park mitaa ya Kirumba ule sato na Ugali wa Donna saaafi.
Ulimaanisha kwenye shughuli ya umalaya?
 
Achana na huyu mtu! Kisha ondolewa na uzembe wake. Nikiangalia elimu yake, sijui ilikuwaje akapewa nafasi muhimu kiasi hicho? Kaishia kufuga ngómbe morogoro tu!
 
Mkuu hii ni kweli. Kokoro zinapiga kazi kama kawa ila fungu wanatenga kuwalipa wakuu wa vituo vta police na maafisa uvuvi.
 
Kuna kiongozi wa CHADEMA amewahi kusema bungeni juu ya mwenendo wa kushughulikia mambo ya wizara ya uvuvi kwa operations. Pamoja na waziri Mpina kuitetea wizara yake, kumbukumbu yangu inaonesha hakuna operation ambayo imewahi kufanikiwa bila matatizo kwa wananchi, bahati mbaya wanaoendesha operation hizo huwa wanapewa kinga kwa uharifu wao hata kama ni nje ya kazi zao. Ilikuwa hivyo kwa Operation Tokomeza Sasa nimeishuhudia Operation Sangara ya bwana Mpina.

Nataka nizungumzie operation sangara ambayo imegeuka kuwa kichaka cha rushwa kwa kanda ya Ziwa. Kuna ufisadi bado unaendelea kwa jina la operation hiyo. Wilaya zote OCD na polisi wake, wakuu wa wilaya na maafisa uvuvi sasa wana mradi wa kudumu wa kuchukuwa rushwa.

Ninazo taarifa za ndani kutoka kwa afisa mwaminifu kwa ushuhuda wake kwa wilaya maarufu kwa uvuvi, Ukerewe. Bado nyavu aina ya makokoro zinatumika kinyume na Operation Sangara. Operation imekuwa ni mtaji kwa mkuu wa Wilaya, OCD na afisa uvuvi wa hamashauri. Polisi wanatumika hukusanya pesa toka kwa kila anayendesha uvuvi haramu na kuziwakilisha kwa OCD ambaye naye huwasiliana na mkuu wa wilaya. Polisi wamekuwa wakishinda barabarani kukusanya pesa kwa waendesha bodaboda wanaosafirisha samaki wadogo, wasioruhusiwa kuvuliwa.

Tatizo langu ni kwa viongozi wa serikali kama huyu mkuu wa wilaya ya Ukerewe na OCD. Inakuwaje aruhusu vitendo hivi haramu kuendelea badala ya kuzuia? Kibaya zaidi ukabila wa mkuu wa wilaya unatumika kujinasibu kwamba rais Magufuli ni ndugu yake. Ndiyo nini hiyo? Yaani mtu anakula rushwa kwa undugu na rais? Nadhani bado hatujapata watu wenye ubora wa kuwa wakuu wa wilaya.

Wakati haya yanatendeka, afisa usalama wa wilaya yupo. Je, anaripoti nini juu ya utendaji wa mkuu huyu wa wilaya? Je, ni mshirika ktk vitendo hivi? Matendo haya yote yanafanyika kwa kisingizio cha polisi wala rushwa, ukweli ni kwamba, polisi wameruhusiwa na wakuu wao kwa wilaya zote za kanda ya ziwa, Bunda, Musoma, Sengerema, Geita na ajabu hata Chato!
SA itakuwaje?
 
Back
Top Bottom