Waziri Mpina apiga marufuku mifugo kupigwa mnada bila kupimwa


miss zomboko

miss zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Messages
1,514
Likes
2,588
Points
280
miss zomboko

miss zomboko

JF-Expert Member
Joined May 18, 2014
1,514 2,588 280
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Luhaga Mpina amemepiga marufuku mifugo inayokamatwa kwenye hifadhi mbalimbali nchini kupigwa mnada bila maafisa mifugo kuipima na kujiridhisha ili kuepuka kuenea kwa magonjwa ya wanyama hao sambamba na kuwachukulia hatua kali wananchi ambao wamekuwa wakipokea na kubeba dhamana ya mifugo kutoka nje ya nchi huku wakidai kuwa ni ya kwao.

Akishiriki zoezi la ukamataji wa mifugo zaidi ya mia moja na sabini iliyoingia wilayani Kasulu mkoani Kigoma kutoka nchi jirani ya Rwanda Waziri Mpina amesema ni kinyume cha sheria na amewataka wafugaji wanaokamatiwa mifugo yao kujitokeza mara moja ili kuepuka usumbufu unaojitokeza.

Aidha Waziri Mpina amesema serikali itaendelea kuwachukulia hatua kali wananchi ambao wamekuwa wakipokea na kukubali kubeba dhamana ya mifugo kutoka nje ya nchi huku wakidai kuwa ni ya kwao.


luhanga-mpina-jpg.619811


ITV
 

Forum statistics

Threads 1,236,992
Members 475,348
Posts 29,275,243