Waziri Mpango awateua wajumbe wawili watakaoiwakilisha Serikali kwenye Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya madini ya Twiga

Hazina

Member
Jun 4, 2018
7
63
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), amewateua wajumbe wawili watakaoiwakilisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Madini ya Twiga (Twiga Minerals Corporation Limited).

Wajumbe walioteuliwa ni
  1. Bw. Casmir Sumba Kyuki
  2. Bw. Michael Jonathan Kambi
Uteuzi wa wajumbe hao watakaotumikia nafasi zao kwa kipindi cha miaka mitatu, unafuatia makubaliano mapya ya namna ya kuendesha Kampuni hiyo kwa ubia, yaliyofikiwa kati ya Serikali na Kampuni ya Barrick Gold, na kutiwa saini tarehe 24 Januari, 2020, Jijini Dar Es Salaam.

Kampuni ya Madini ya Twiga inasimamia migodi mitatu ya Buzwagi, North Mara na Bulyanhulu ambapo Barrick Gold inamiliki asilimia 84 ya hisa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inamiliki hisa asilimia 16.

Uteuzi wa wajumbe hao unaanza leo tarehe 22 Machi 2020

D5C01C3E-A3C2-4AB2-BF92-C271DF7E77D0.jpeg
 
Back
Top Bottom