Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,883
- 6,884
Titan, Masanja, Mwakatare na Sophist mimi naona mawazo yenu yamepitwa na wakati sana!!!
Kuna wanaosema eti Dual citizenship wafanyabiashara watakimbiza pesa nje je ni mfanya biashara gani ambae hawezi kukimbiza pesa nje kwasababu ya uraia. Hapa Marekani mtu yeyote anaweza kufungua account ya bank hata kama si raia, mtu yeyote anaruhusiwa kununua nyumba hata kama si raia!!! sasa mkisema kwasasa wafanyabishara hawapeleki pesa nje kwasababu ya uraia si ukweli kabisa, hata kuna Mawaziri na maraisi wana account nje. Hivyo hii hoja si ya kweli na niya ushabiki maana haina mfano zaidi ya maneno tu.
Hoja nyingine ni kwamba watu watafaidika! je watafaidika na nini? ambacho kwa sasa hawawezi kufaidika je Tanzania itawapa nini hawa watu walioko nje wafaidike?. Hakuna faidi yeyote nchi yetu ni masikini sababu kubwa ni ndugu na jamii. Kama Ndugu zako na mababu wawezikwa Tanzania ni vigumu kuomba visa ya kwenda kuangalia geneza la ndugu zako na ndiyo maana nimesema hii ni kwa watu waliozaliwa Tanzania na wenye wazazi Tanzania. Sasa nyie mnasema kama nina mtoto kazaliwa hapa na atakuwa raia wa marekani kuanzia siku ya kwanza na mimi nikitaka kumpa nyumba yangu kwa uzee haitawezekana na nyumba iende kwa serikali!!! je huyu mtoto au mimi nimefanya kosa gani bali kuwa nje.
Je Watanzania pesa zinazotoka Tanzania kuja kwa watu wanaoishi nje na pesa zinazoingia Tanzania kwa watu wanaoishi nje zipi ni nyingi?? na mnavyosema faida ni zipi hasa? mimi naona faidi ni kwa Tanzania na siyo kwa mtu anayeishi nje. Mimi nikija Tanzania serikali inanisaidia nini kuliko hapa Marekani?? Hakuna msaada wowote watu wa nje tunaoupata kutoka serikalini na sababu kubwa ya kuja na kutuma pesa Tanzania ni kwasababu ya uzawa na ndugu kama wazazi, wajomba, n.k
Kama hamna sababu ya msingi basi tukubaliane ni uivu tu na kutowapenda watanzania wanaoishi nje. Kitendo cha kusema kunawafanyabishara watakimbiza pesa si kweli kwani kunawafanyabishara wangapi wana account nje je mnafikiri Baresa, Mengi, n.k hawanapesa nje au wakitaka kwenda nchi yeyote wanaenda hata kama kuishi na kwa pesa yao wanapewa mpaka uraia.
Fikirieni nchi na si ubinafsi. Mnavyosema itamfaidisha vipi Mtanzania wa kawaida je nyie mnamsaidia vipi Mtanzania wa kawaida! kuna kidu gani ambacho wewe unafanya cha kuisaidia Tanzania kuliko mimi?
Tukubali wengi wetu ni wavivu wa kufikiri. Watanzania wakipata dual citizenship kuna faida kubwa 90% kuliko 10% hasara ya kufikirika tu kutokana na wachache ambao hawaepukiki hata kwa kutokuwa na dual citizenship. Mataifa yaliyoruhusu mfumo huo yananufaika zaidi na kujenga uchumi mkubwa katika nchi zao kwani raia waliopo nje ya nchi zao ni kiungo kuzuri cha biashara huria.
- China - Wachina wamejaa sana nchi za nje na hivyo wanasaidia kupata soko la bidhaa zao nchi za nje, kama USA, Europe nk.
- Philipine - Pesa ya kigeni inayoingia nchini homo kiasi kikubwa mno kinachangiwa na raia wao walioko mataifa ya nje.
- Marekani - Imeweza kujenga uchumi wake kutokana na wahamiaji, licha ya wahaniaji kuchota pesa lakini muda wanaoishi huko husaidia kujenga uchumi wa nchi kwa mkondo wa ajira.
- Mataifa ya West Afrika - Yamekuwa na kiungo kizuri cha kufanya biashara na mataifa ya nje kutokana na raia wake kuwa huru katika uraia.
- Kenya na Uganda - Tanzania tunahangaika kuzifukuzia nchi hizo kiuchumi lakini hatuzikuti ina tunaishia wao wana mbinu za kibiashara na kiuchumi na hivyo tutabaki kuweka vipingamizi kwa watanzania wenzetu na kuwaacha wakenya na waganda kuja kuchuma kwetu.
Ulimwengu wa sasa ni global village, sasa watanzania wenzetu wanaturudisha kwenye zama za analog wakati ulimwengu wa global village ni wa digital. Inachosha na kukatisha tamaa, kwani jitihada za kujenga uchumi si kulalamikia kodi tu, kuna njia nyingi sana na zile tunazopuuza na kuzidhara ndizo wenzetu wanazotumia kupiga hatua mbele.