Waziri mmoja ni Raia wa Marekani: Gazeti la Dira

green-card.gif

Hii si hati ya uraia, bali ni kitambulisho cha mkazi wa kudumu nchini Marekani (green card) mwenye kupata haki za kijamii zote isipokuwa kupiga na kupigiwa kura katika uchaguzi wa viongozi kisiasa. Hii ni hati ya ukazi tu si uraia. Na mwenye hati hii tu hawezi kupata passport ya wamarekani mpaka apate naturalization.

Green card hazipatikani kirahisi hivyo. Kwangu mimi sioni shida sana waziri kuwa na hiyo resident permit, swali je ali-declare yote haya kabla ya a) kugembea ubungu na b) tume ya maadali wanasemaje?
 
Dual citizenship kwa Tanzania bado kabisa kufikia huko, na kama tukifanya hivyo sasa ni hatari kubwa sana kwa uchumi na usalama wa nchi yetu. Tusiwe watu wa kukurupuka tu eti kwa kuwa nchi fulani na nchi fulani wana -dual citizenship basi na sisi TZ tuwe hivyo ,no, mazingira yetu bado hayaruhusu. Tukifanya hivyo, watu wabaya hasa viongozi na wafanyabiashara wakubwa watatumia mwanya huo kuhamisha mali zetu kupeleka huko kwenye makazi yao mapya kwa urahisi kabisa na kwa halali kwa kuwa ni mwananchi, na pia hawatajali usalama wa nchi yetu kwa kuwa wao na familia zao wana pa kukimbilia endapo itabidi. Dual citizenship sio mahitaji ya Watanzania hawa ambao hata mlo mmoja tu wa siku unawasumbua sembuse hiyo mitatu, dual citizenship ni mahitaji ya watu wachache sana 0.0001 ya watz milioni 45, ambao wameishaikana nchi yetu au wapo mbioni kuikana ila wanatamani maliasili za tz ambazo bado kwa kiasi kikubwa ni mali ya watz, sasa anaona atazikosa. Hoja zinazotolewa na watetezi wa dual citizenship, hasa waziri wa mambo ya nje wa TZ ni dhaifu mno kuweza kukubalika na watu wanaofanya uchanganuzi wa kina, eti ili hao watz waliopo nje ambao wameshaukana utz na kupata uraia wa huko waweze kuwekeza nchini,hivi kweli hii ndiyo sababu? kwani wote hao wawekezaji tunaowavutia kila siku waje wawekeze nchini ni watz au kwamba tumeweka sharti kwamba ili kuwekeza nchini lazima uwe raia wa tz? Hao Diaspora wanaweza tu kuwekeza nchini kama wageni wowote wa nje wanavyowekeza. Kwa kweli mimi napinga sana wazo hili kwa kuwa tz bado haijajiandaa wala kufikia maendeleo ya kuweza kuwa na dual citizenship, nchi itafirisika haitapata faida yoyote na wala hilo sio hitaji la watz ambao wengi wao hata hiyo passport hawajawahi kuiona, sasa vipi wafikirie kuwa na uraia wa nchi mbili?. Kwa maana hiyo kama kweli yupo waziri kwenye baraza letu la mawaziri mwenye uraia wa marekani, kwa maana kama ana passport ya marekani inatakiwa aachishwe kazi mara moja na kushtakiwa kwa kuvunja sheria ya uhamiaji na kujipatia ajira tz kinyume na sheria.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Nimestushwa kidogo na hii habari kuwa kuna waziri mmoja ni raia wa marekani...na ni mmoja kati ya hawa wawili waliopo katika picha hii!! Je ni yupi kati ya Cyril Chami;kushoto na Lazaro Nyalandu;kulia?

3.jpg
 
Sasa kama yupo ana mnamjua kinachowafanya msite kumtaja ni nini? Aidha mtajeni ama acheni udaku. Period!!
 
Kwa kuongezea, ni upeo finyu mtu mzawa katika nchi yake kuambiwa si raia. Ningeambiwa amezaliwa nje ya nchi hapo ni sawa, lakini kazaliwa tunza yenye nia na wazazi wake wakiwa wazawa pia nini tatizo?
Tuna watanzania wengi wanaotamani kuwekeza home na hata kufanya mengi home ili kusaidia kuinua uchumi wa taifa lakini tatizo ndio hilo wivu uliokithiri kati ya watanzania.

Watanzania wako tayari na kuwapa uhuru mkubwa wageni wanaochota utajiri wetu na kuupeleka nje badala ya wazawa watakaoleta mali zanje kunufaisha Tanzania. Na wivu huu unaanzia na viongozi wetu wa serikali na bunge.

Nadhani kuna haja ya kuipenda Tanzania kuliko kujipenda wenyewe. Dual citizenship hakiwezi kuwa kipaumbele cha wala mkakati wa maendeleo kwa watanzania kwa sasa. Siamini kuwa Tanzania itapata maendeleo kwa kutegemea watu wasioaminika, walioamua kuukana utaifa wao ili kupata manifaa binafsi. Hawa ni watafuta chakula above all, period. Ni kutokana na kutafuta chakula tu, hawa jamaa waliamua kuukana uraia wa Tanzania, na sasa wangependa kurudi kwa kupitia mlango wa nyuma; kwamba wanakuja kuwekeza! Hapa hakuna suala la wivu ndugu zangu, it is the matter of sticking to the principle; nani ni raia, nani si raia, period!
Kama diaspora wanataka kuwekeza, si waje wawekeze kama mabepari wengine? Kwani Barrick, Anglogold Ashanti, Resolute Mining, na wengineo walipokuja waliomba uraia wa Tanzania? Hapana, waliomba leseni na mikataba ya uwekezaji.
Uwekezaji na uraia wa nchi mbili havihusiania hata kidogo. Litakuwa ni jambo la ajabu iwapo serikali itaanza kuwakirimu watoro ilihali raia wa kawaida wanaendelea kusota. Mtu yeyote aliyewahi kuwa raia wa nchi hii halafu akakana uraia wa nchi yake hawezi kuaminika, ati apewe uraia tena, kwa kisingizio cha kuleta vitegauchumi (vyake!). Lakini iwapo diaspora yuko huko Ulaya au Amerika, bado hajaukana uraia wa Tanzania na sasa anataka kurudi nyumbani, si arudi? Nadhani huyu hazuiwi na si sehemu ya mjadala huu.
Uraia wa nchi unaweza kulinganishwa na kuwa mwanafamilia. Huwezi kukana familia yako na kuhamia familaia ya jirani, halafu utake kutambuliwa kama mwanafamilia zote mbili; kwa familia inayoheshimika au kujiheshimu haiwezi kukupokea tena aslani. Uliidhalilisha!
Hata hivyo, wahemeaji hawawezi kuleta maendeleo nyumbani, hilo tusahau kabisa, na CCM ikitaka kujichimbia kaburi, basi serikali yake ipeleke muswada wa dual citizenship Bungeni ione.
Wakhtanabahu
 
green-card.gif

Hii si hati ya uraia, bali ni kitambulisho cha mkazi wa kudumu nchini Marekani (green card) mwenye kupata haki za kijamii zote isipokuwa kupiga na kupigiwa kura katika uchaguzi wa viongozi kisiasa. Hii ni hati ya ukazi tu si uraia. Na mwenye hati hii tu hawezi kupata passport ya wamarekani mpaka apate naturalization.

Well said hata mm na resident permit ya nchi fulani huku nikiwa na passport ya Tanzania. Ni watu wachache wenye kuelewa BUT labda wana strong argument dhidi ya huyo waziri let us give them space and time to see..

Mbona kwanza kama ni hii imesha expire 1994?
 
View attachment 30073Ndugu wanajukwaa,
Nimeshtushwa na taarifa iliyochapwa na gazeti la Dira la leo juu ya waziri kijana wa serikali ya CCM kuwa ana uraia wa Marekani na mpaka nakwenda mitamboni hapa jamvini bado serikali ya JK haijazungumza kitu kuhusu tuhuma hizi, je maana yake ni kweli? na kama kweli JK anangoja nini? je kwanini asiachie ngazi haraka kwa jinai ya kuteua raia wa Marekani kuwa waziri kwenye nchi yetu?....

If Not Me Who? And If Not Now When?

Hivi ni lini watu wata-engage vichwa vyao kwa namna ya kuvitendea haki? Hivi unadhani kila tukio linahitaji rais aliyechaguliwa kwa ridhaa ya wananchi ajiuzulu tu kwa udaku huu ambao hauna kichwa wala miguu? Hivi wewe ungekuwa rais halafu ukakurupuka kuchukua maamuzi ya kitoto kama unayopendekeza wananchi wangekutizama tu? Wewe na gazeti lako hilo la udaku mtuache tupumue na kumwacha rais afanye mambo ya maana kuliko kusikiliza maneno ya mtaani.
 
[/SIZE][/FONT]

Nadhani kuna haja ya kuipenda Tanzania kuliko kujipenda wenyewe. Dual citizenship hakiwezi kuwa kipaumbele cha wala mkakati wa maendeleo kwa watanzania kwa sasa. Siamini kuwa Tanzania itapata maendeleo kwa kutegemea watu wasioaminika, walioamua kuukana utaifa wao ili kupata manifaa binafsi. Hawa ni watafuta chakula above all, period. Ni kutokana na kutafuta chakula tu, hawa jamaa waliamua kuukana uraia wa Tanzania, na sasa wangependa kurudi kwa kupitia mlango wa nyuma; kwamba wanakuja kuwekeza! Hapa hakuna suala la wivu ndugu zangu, it is the matter of sticking to the principle; nani ni raia, nani si raia, period!
Kama diaspora wanataka kuwekeza, si waje wawekeze kama mabepari wengine? Kwani Barrick, Anglogold Ashanti, Resolute Mining, na wengineo walipokuja waliomba uraia wa Tanzania? Hapana, waliomba leseni na mikataba ya uwekezaji.
Uwekezaji na uraia wa nchi mbili havihusiania hata kidogo. Litakuwa ni jambo la ajabu iwapo serikali itaanza kuwakirimu watoro ilihali raia wa kawaida wanaendelea kusota. Mtu yeyote aliyewahi kuwa raia wa nchi hii halafu akakana uraia wa nchi yake hawezi kuaminika, ati apewe uraia tena, kwa kisingizio cha kuleta vitegauchumi (vyake!). Lakini iwapo diaspora yuko huko Ulaya au Amerika, bado hajaukana uraia wa Tanzania na sasa anataka kurudi nyumbani, si arudi? Nadhani huyu hazuiwi na si sehemu ya mjadala huu.
Uraia wa nchi unaweza kulinganishwa na kuwa mwanafamilia. Huwezi kukana familia yako na kuhamia familaia ya jirani, halafu utake kutambuliwa kama mwanafamilia zote mbili; kwa familia inayoheshimika au kujiheshimu haiwezi kukupokea tena aslani. Uliidhalilisha!
Hata hivyo, wahemeaji hawawezi kuleta maendeleo nyumbani, hilo tusahau kabisa, na CCM ikitaka kujichimbia kaburi, basi serikali yake ipeleke muswada wa dual citizenship Bungeni ione.
Wakhtanabahu

Unapochukua uraia wa USA huna haja ya kuukana utanzania. You can keep your passport.
 
Unapochukua uraia wa USA huna haja ya kuukana utanzania. You can keep your passport.

Na huwezi kuwa na passport ya TZ bila ya kuonyesha uthibitisho wa uraia

USA wanakubali dual nationality Tanzania haina

Sheria za Tanzania ziko wazi ukitaka uraia wa nchi nyingine inabidi uukane uraia wako wa TZ
 
Kuna habari kuwa CHADEMA wana mbunge ambaye si raia wa Tanzania...tena kwa kuukana uraia wake. Na kuna taarifa ambazo zinadai kuwa ana passport ya nje (kama Plan B just in case)

Lakini sasa hivi huyu mheshimiwa yuko bungeni kama mmoja ya wanaotunga na kupitisha sheria katika nchi hii

Je hii inaukweli wowote au ndio smear campaigns? Inawezekana CHADEMA wenyewe kwa wenyewe washalizungumza internally.

Mindhali CHADEMA wako humu wanaweza kutuweka sawa kwenye hili.
 
unaweza kumtaja
 
Na huwezi kuwa na passport ya TZ bila ya kuonyesha uthibitisho wa uraia

USA wanakubali dual nationality Tanzania haina

Sheria za Tanzania ziko wazi ukitaka uraia wa nchi nyingine inabidi uukane uraia wako wa TZ

Nimechukua uraia wa US na nina passport 2, hii ya blue na ya kijani yangu ya kibongo. Sioni tatizo lolote kwangu ama kwa huyo waziri. Shida iko wapi jamani? Yeye bado ni mbongo mwenzetu. Tuko wengi sana wenye pasi mbili wengine wanazo hadi 4
 
Back
Top Bottom