Waziri Mkuu: Watu Bilioni 3.9 Duniani jana walifuatilia Shughuli za Kumuaga Hayati Magufuli

Hivi Majaliwa anajua idadi ya watu duniani ni around 8b? anamaanisha zaidi ya 50% walifuatilia? Au alimaanisha 39milioni?
Kwa teknologia ya sasa, i
Mmmhh uongo wa kiwango cha SGR ,yaani amevunja mara nne rekodi ya Mohamad Ali alifatiliwa na idadi ya watu bilioni 1.
Hiyo ni kweli kabisa!! Ndiyo maana hakuna chombo cha magharibi kilichokanusha! Hii figure hakuibuni Waziri mkuu lakini amenukuu vyombo vya magharibi vilivyokuwa vinafuatilia. Kwa teknologia ya sasa, hilo ni Jambo dogo Sana. Magufuli alikuwa maarufu Sana duniani! Japo wazungu hawakuwa tayari kukiri hivyo!! Walikuwa wanashangaa mwafrika kuwa na msimamo thabiti na wa kweli kinyume na Dunia yote!
 
8b halafu wenye itaneti ni nusu ya hao, kwa hiyo watu wote wenye intaneti walikuwa wanaangalia tz jana
IMG_20210327_113819.jpg
 
Kwa hiyo alihamisha akili wakati akiea kwenye mazishi alianza kufanya sensa ya watu wanaotazama mazishi!
 
Nakumbuka PM alituambia kuwa watu zaidi ya bilioni 3.9 walifatilia msiba wa JPM

Huwa nashangaa sana, waziri mkuu kwanini anapenda kudanganya sana

My take:Majaliwa kwangu bado ni msafi na napenda misimamo yake ya kusimamia mali za umma!Sahivi anayepigwa vita ni yeye ili atoke pale, Jamaa ana vita nzito sana PM haendani na hii serikali kabisa

Serikali ya Samia ni kama tenga tu halishoneki tena matobo kila pahala, serikali inayonuka ufisadi, wizi,rushwa,uzembe na kutojali wananchi ndo hii.

Maskini PM namuonea huruma sana mizengwe yote anayopigwa ingekua ni mimi ningekaa pembeni niwaachie jahazi lao linalozama!!
 
Akiwa anatoa maelezo kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar, Waziri Mkuu amesema kwa taarifa walizonazo jana wakati wa shughuli za kumuaga Hayati JPM watu waliofuatilia tukio hilo duniani ni 3.9 bilioni kama siyo 4 bilioni.

Na hivyo amevishushukuru sana vyombo vya habari kwa kurusha matangazo ya moja kwa moja.

“Tunavishukuru vyombo vya habari vimekuwa na sisi toka siku ya kwanza kuwahabarisha Watanzania, hata tukio hili mnalirusha duniani kote. Mpaka jana jioni tunazo taarifa watu waliofuatilia tukio la kuaga kitaifa jana Dodoma ni zaidi ya watu bilioni 3.9” - Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Swali lenye lenye tija lingekuwa, "kumuaga kitaifa JPM anakwenda wapi?", kumbuka ilikuwa siku ya Ijumaa akiwa ndani ya msikiti aliwaambia waumini wenzake kuwa " rais yuko ofisini anachapa kazi, mlitaka mmuone Kariako?", hakuwahi kukanusha kuwa hayuko ofisini.
 
Back
Top Bottom