Waziri Mkuu wa Uingereza asimamisha Bunge hadi Oktoba 14. Wanaopinga Brexit wapatwa hasira wakidai hatua hiyo inaweza kuzuia Bunge kujadili mpango huo

MkamaP

JF-Expert Member
Jan 27, 2007
8,142
3,217
Hatua ya Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson kusababisha bunge kusitisha vikao vyake imezusha mjadala. Kiongozi wa upinzani Jeremy Corbyn akimwandikia barua Malkia Elizabeth kueleza kusikitishwa kwake na mpango huo.

Kiongozi wa chama cha upinzani cha Labour nchini Uingereza Jeremy Corbyn amemwandikia barua Malkia Elizabeth kueleza kusikitishwa kwake na mpango wa waziri mkuu wa taifa hilo Boris Johnson wa kusitisha shughuli za bunge hadi Oktoba 14 baada ya malkia kuridhia ombi la serikali.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani ya chama hicho, Corbyin pia ameomba kukutana na Malkia Elizabeth. Chama kingine kidogo cha kiliberali cha upinzani, ambacho kimekuwa kikipinga hatua ya Uingereza kujiondoka katika Umoja wa Ulaya-Brexit, nacho kimeandika barua inayofanana na ya Corbyn kwa Malkia kuonesha kusikitishwa kwao na hatua ya Boris Jonhson.

Katika muendelezo wa kupingana na jitihada za Johnson, Ireland vilevile imesema haitabadili msimamo wake kuhusu hatua ya Brexit. Akiulizwa na mtangazaji wa kituo cha redio cha taifa RTE, kuhusu msimamo wa Ireland baada ya hatua ya waziri mkuu wa Uingereza, ambayo itaweza kuzuia nafasi ya bunge kuijadili Brexit kabla ya tarehe ya mwisho ya makubaliono ya mpango huo ya Oktoba 31, waziri wa upande wa Ireland, Paschal Donohoe aliongeza kwa kusema hakuna uondokaji wa holela wa Uingereza katika Umoja usiweza kuepukika

Kwa upande wake Waziri wa kiongozi wa Scotland, Nicola Surgeon amesema:

"Kulifunga bunge ili kulazimisha Uingereza kuondoka katika Umoja wa Ulaya bila makubaliano jambo litakalosababisha athari kubwa na ya muda mrefu kwa taifa, kinyume na matakwa ya bunge, ni udiktekta. Na kama wabunge hawajaungana pamoja kumzuia Boris Johnson na mwenendo wake, nadhani kwa sasa demokrasia ya Uingereza utakuwa inakufa"

Mapema leo Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson amefanya jaribio la kudhibiti fursa ya fursa ya bunge kujaidili mchakato wa Brexit kwa kupunguza muda kuanzia sasa hadi tarehe iliyopangwa na Umoja wa Ulaya ya taifa hilo kujiondoa ya Oktoba 31, akiwagadhibisha wapinzani wanaomtuhumu kuendesha mambo kwa kutumia mabavu.

Jitihada yake ya sasa ni kuiondoa Uingereza nje ya Umoja wa Ulaya iwe kwa makubaliano au kinyume chake. Hatua ya sasa inaweza kufanikishwa kuhitimishwa kwa ngwe ya vikao vya bunge la Uingereza katikati ya mwezi ujao ikiwa ni takribani mwezi mmoja kabla ya tarehe ya mwisho ya Brexit.

Kwa wanaopinga mpango wa Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya bila ya maridhiano, unapungua pia muda wa kuwasilisha mswaada wa sheria kuzuwia nchi hiyo kujitoa kwa kila hali ifikapo Oktoba 31 inayokuja.
 
Sisi Kama Tanzania tunajifunza nini kisiasa hasa pale waziri mkuu wa uingereza anapoamua kuvunja bunge ili asibugudhiwe na ili apitishe mambo anayotaka?

Anakiuka katiba na mbaya zaidi safari hii amemshirikisha Malkia Elizabeth na bibi wa watu na uzee wote huo wamemwingiza kwenye mgogoro.

Nafahamu watu watasema kuna katiba lakini Borisi Johnson ameamua asimamishe bunge kwa wiki mbili (kinyume na katiba) ili azuia bunge hilo lisijadili suala la Brexit.

Kisha ikifika muda wa kupitisha uamuzi wa kuiondoa Uingereza bila kufanyika dili lolote yaani "No deal Brexit" Bunge litakuwa halijahusishwa kikatiba kujadili suala hilo.

Yaani Boris Johnson anafanya "By-passing" utaratibu wa bunge kujadili hiyo No deal Brexit (ambayo wengi wa wabunge hawataki iwe No deal Brexit) ili tu Uingereza itoke kwenye jumuiya ya Ulaya.

Huo ndo waitwa unafiki wa kiwango cha juu yaani "hypocrisy of the highest level".
 
This is the best contribution on this thread. I wish you could use the same type of arguments when it comes to what is going on in our beloved country for the last four years.

Anakiuka katiba na mbaya zaidi safari hii amemshirikisha Malkia Elizabeth na bibi wa watu na uzee wote huo wamemwingiza kwenye mgogoro.

Nafahamu watu watasema kuna katiba lakini Borisi Johnson ameamua asimamishe bunge kwa wiki mbili (kinyume na katiba) ili azuia bunge hilo lisijadili suala la Brexit.

Kisha ikifika muda wa kupitisha uamuzi wa kuiondoa Uingereza bila kufanyika dili lolote yaani "No deal Brexit" Bunge litakuwa halijahusishwa kikatiba kujadili suala hilo.

Yaani Boris Johnson anafanya "By-passing" utaratibu wa bunge kujadili hiyo No deal Brexit (ambayo wengi wa wabunge hawataki iwe No deal Brexit) ili tu Uingereza itoke kwenye jumuiya ya Ulaya.

Huo ndo waitwa unafiki wa kiwango cha juu yaani "hypocrisy of the highest level".
 
Anakiuka katiba na mbaya zaidi safari hii amemshirikisha Malkia Elizabeth na bibi wa watu na uzee wote huo wamemwingiza kwenye mgogoro.

Nafahamu watu watasema kuna katiba lakini Borisi Johnson ameamua asimamishe bunge kwa wiki mbili (kinyume na katiba) ili azuia bunge hilo lisijadili suala la Brexit.

Kisha ikifika muda wa kupitisha uamuzi wa kuiondoa Uingereza bila kufanyika dili lolote yaani "No deal Brexit" Bunge litakuwa halijahusishwa kikatiba kujadili suala hilo.

Yaani Boris Johnson anafanya "By-passing" utaratibu wa bunge kujadili hiyo No deal Brexit (ambayo wengi wa wabunge hawataki iwe No deal Brexit) ili tu Uingereza itoke kwenye jumuiya ya Ulaya.

Huo ndo waitwa unafiki wa kiwango cha juu yaani "hypocrisy of the highest level".
Ana hatari kubwa Sana huyu PM, atakuja kuondolewa madarkani kwa kura ya kutokuwa na imani naye. Yatamtokea puani hayo maamuzi yake
 
Ana hatari kubwa Sana huyu PM, atakuja kuondolewa madarkani kwa kura ya kutokuwa na imani naye. Yatamtokea puani hayo maamuzi yake

Hayo tayari yaliwahi kutokea huko nyuma ndo maana kusoma Historia kuna faida yake.

Mwaka 1649 mfalme Charles wa kwanza alinyongwa kwa kukatwa kichwa kwa kuleta mchezo huu wa kusimamisha bunge lisiendelee na shughuli zake.

Hiyo ilikuwa ni kabla ya vita vya wenyewe vya Uingereza English Civil War ya mwaka 1649 -1651 ambapo wafuasi wa mfalme Charles wa kwanza walikung'utwa na wabunge katika vita iloitwa "Battle of Worcester"

Mfalme Charles wa kwanza alitaka kuweka kodi mpya ya kichwa kwa kila raia na wabunge wakakataa hilo wazo na ndipo alipoamua kulivunja huku akipiga kazi kwenye kasri yake.

Bunge lilikuwa halipo kwa miaka 20 huku Charles wa kwanza akipeta tu bila kudhibitiwa lakini watu wakimlia "timing"

Siku ya siku vita ikazuka na iliposindwa Charlea wa kwanza hakuwa na jinsi zaidi ya kusalisha kichwa chake..

Mwanae Charles wa pili ilibidi akimbilie uhamishoni.

Usicheze na haya mambo ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.
 
Back
Top Bottom