Waziri mkuu wa Somalia aidhinishwa na Bunge

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Bunge la Somalia limeidhinisha uteuzi wa Hassan Ali Kheyra kuwa waziri mkuu.

Kheyra ambaye aliwahi kufanya kazi kama mshauri na mkurugeni mkuu wa kampuni ya mafuta anatarajiwa kuteua baraza lake la mawaziri.

Akihutubia bunge, alisema kuwa lengo lake kuu ni kukabiliana na ukame uliopo, kuimarisha usalama mbali na kukabiliana na ufisadi.

Hatahivyo kazi ya mkuu huyo wa serikali ya Somalia huenda ikapungua baada ya Umoja wa Mataifa kuonya kwamba Somalia ipo katika hatari ya kukumbwa na baa la njaa pamoja na tishio la usalama linalotolewa na kundi la wapiganaji wa al-Shabab.

Chanzo: BBC
 
Back
Top Bottom