Kimbunga
Platinum Member
- Oct 4, 2007
- 14,941
- 9,947
Wakuu tunakumbuka kwamba mirungi (miraa) ilipigwa marufuku hapa nchini kwa kuwa ni madawa ya kulevya. Mirungi hulimwa sana nchini Kenya na huwa inauzwa Somalia na Kenya kwenyewe na pia huwa inaingizwa Tanzania kiharamu kama yaingiavyo madawa mengine ya kulevya. Kwa kenya mirungi ni halali lakini kwa Tanzania ni haramu. Sasa kuna habari kwamba Waziri Mkuu wa Kenya Ndg. Raila Amollo Odinga ana mpango wa kumuomba JK aihalalishe nchini Tanzania ili Wakenya waomngeze soko la mirungi wanayosafirisha kihalali kwenda nchi za nje.
Mimi binafsi sijui kama mirungi ni madawa ya kulevya ama la. Lakini kama ilipigwa marufuku hapa nchini basi inaonekana ina matatizo kama Kuber. Sasa sijui Raila akimuomba JK ahalalishe na kweli ikahalishwa itakuwaje?