Waziri Mkuu wa Kenya (Odinga) kumuomba Kikwete ahalalishe mirungi Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Mkuu wa Kenya (Odinga) kumuomba Kikwete ahalalishe mirungi Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kimbunga, Oct 6, 2011.

 1. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #1
  Oct 6, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Wakuu tunakumbuka kwamba mirungi (miraa) ilipigwa marufuku hapa nchini kwa kuwa ni madawa ya kulevya. Mirungi hulimwa sana nchini Kenya na huwa inauzwa Somalia na Kenya kwenyewe na pia huwa inaingizwa Tanzania kiharamu kama yaingiavyo madawa mengine ya kulevya. Kwa kenya mirungi ni halali lakini kwa Tanzania ni haramu. Sasa kuna habari kwamba Waziri Mkuu wa Kenya Ndg. Raila Amollo Odinga ana mpango wa kumuomba JK aihalalishe nchini Tanzania ili Wakenya waomngeze soko la mirungi wanayosafirisha kihalali kwenda nchi za nje.

  Mimi binafsi sijui kama mirungi ni madawa ya kulevya ama la. Lakini kama ilipigwa marufuku hapa nchini basi inaonekana ina matatizo kama Kuber. Sasa sijui Raila akimuomba JK ahalalishe na kweli ikahalishwa itakuwaje?
   
 2. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #2
  Oct 6, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  nilitumia sana hilo jani nikiwa o'level magamba sekondari, ipo mingi sana kule.
   
 3. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Huyu jamaa ni bure kabisa, yeye husema chochote anachojua wananchi wangependa kukisikia ata kama anajua kabisa kuwa hakitekelezeki...
   
 4. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #4
  Oct 6, 2011
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Nitashangaa sana JK kukubali maana hiyo mirungi ndiyo ilikuwa sababu ya vifo vingi sana TZ kipindi kile mpaka ikathibitika kuwa madereva walikuwa wanaipenda sana maana huila ile wakaendesha gari bila kujihisi kuwa wamechoka matokeo yake wakawa wanasababisha ajali mbaya sana. Kama sikosei ndiyo kisa cha mirungi kupigwa marufuku Tanzania. Na ndiyo maana yale ma FIAT ya zamani yote yakahamishiwa Kenya na Wasomali.
  Hiyo biashara Kenya ni hatari si mchezo. Magari yao yanapokuwa yamebeba hiyo miraa kuelekea uwanja wa ndege, hata wakikanyaga mtu au kukwaruza gari ya mtu huwa hayasimami, ni biashara ya kishenzi sana. Maeneo inakolimwa vijana hawaendi shule kabisa. Itakuwa si jambo la busara hata kidogo kwa biashara hiyo kuruhusiwa nchini. Umaskini tulio nao hautaondoka kwa kuruhusu mihadarati hiyo! Isije ikawa wao wanatafuta watu wa kuwalimia miraa ili waondoe hiyo adha nchini mwao.
   
 5. Malipesa

  Malipesa JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2011
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 310
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hii haijatulia, kama ilishakatazwa kama akikubali kwa sasa itakuwa hajatumia akili sawasawa.
   
 6. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #6
  Oct 6, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,972
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Source ya habari mbona hukuweka, au ni wewe mwenyewe? Nachelea kuchangia isije ikawa unawapakazia tu hawa wakulu!
   
 7. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #7
  Oct 6, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Source Citizen TV
   
 8. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #8
  Oct 6, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
 9. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #9
  Oct 6, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  ndiyo maana WTZ wengi waigomea jumuiya ya Afrika Mashariki
  anataka tulewe tusiwe na akili timamu alafu wao wapate nafasi ya kutala nyanja zote za Uchumi Afrika Mashariki eeh

  MUNGU tunusuru na hili balaa
   
 10. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #10
  Oct 6, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Msione ajabu huyu M/kiti wa hawa magamba akaruhusu mirungi kutinga hp nchi! Na kwa kweli Mi nafsi yangu nawaambia ya kwa mirungi ni madawa ya kulevya kwani nimeshaitumia na nina sababu kuu kadha ya kunifanya niseme ni madawa ya kulevya na ni kama hii: (1) Ukiwa unakula mirungi na ukanywa na pombe kama bia,konyagi na hata pombe kali kali zile ya wenzetu wa pesa ndefu hakika hautalewa kamwe na mpaka ukalewe ni baada ya kutema ile taksima yake na kwa mfano unakunywa bia hakika hata kreti 2 unaweza ukakata yote na usipepesuke hata chembe. (2) Kwa upande wa mapenzi! Hakika kama andas yake haijaku2ma kuwa na mwanamke hakika nakwambieni hata ukiletewa mwanamke wa namna gani hakika hautamtaka na ikikutuma kuwa na mwanamke hakika hauwezi lala bila ya kuwa na mwanamke hata kama unaishi Arusha mwanamke akawa anakaa Moshi nawaambia kama uko njema kifedha unamfuata huko huko kwa gharama yeyote. Kwa hiyo Mi nafsi yangu sioni sababu ya mirungi iingizwe kwe2 kihalali hata punje. (3) Mlaji akishakuwa anachanja hataki tena kazi starehe yake kubwa ni akae mpk amalize na wengi walaji wanaume hawana tabia ya uasherati. Ni hayo tu niliyokutana nayo wakati ule nachanja. Asanteni!!
   
 11. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #11
  Oct 6, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu mbona iko safi tu. Ila tu mlaji aombe isimtume kwa wanawake.
   
 12. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #12
  Oct 6, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Kimbuga! Kwa kweli kwangu Mi naona kama ingeruhusiwa ktk umri fulani kwani ingekuwa bomba sana,maana kwa kweli kuna vijana hawataweza gharama ya kwani inaweza ikakupeleka kutaka kutamani ki2 ambayo hauna uwezo nayo. Lakini ujuwe ina gharama sana!!
   
 13. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #13
  Oct 6, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Mbona Jeiro alisimamishwa kazi na kisha akarudishwa kazini na yeye akampumzisha tena?
   
 14. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #14
  Oct 6, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Mbona Kenya hamna ajali kama hapa Tanzania?
  Usikurupuke, ugomvi wa Mirungi ilikuwa na kati ya Mrema na wapinzani wake.
  Hayo mambo ya ajali yana wizara yake na si ya mambo ya ndani ambayo Lyatonga alikuwa anaiongoza.
   
 15. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #15
  Oct 6, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Alikwambia nani Mirungi inalewesha?
  Usikurupuke.
   
 16. KALYOVATIPI

  KALYOVATIPI JF-Expert Member

  #16
  Oct 7, 2011
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,419
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  kwani kile kifungu kama cha matembele kinauzwa shngapi?
   
 17. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #17
  Oct 7, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,307
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  Tupunguzeni mambo ya kuuliza source jamani. Kama nyuzi yake huiamini unaweza kuipotezea na siku ikaenda. source hata yeye aweza kuwa.
   
 18. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #18
  Oct 7, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Inategemea.
  Kifungu kimoja cha mrungi toka Tanzania ni shilingi 1500 mpaka 2500.

  Na mrungi kutoka Kenya ni shili elfu 5.
  Hii inatokana kuwa mrungi toka Kenya ni mkubwa na pia ni mwingi.

  Any question abt Mirungi?
   
 19. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #19
  Oct 7, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  mkuu wa hichi kichaka cha maskini zaidi duniani lazima atakubali! Maana maamuzi yake,dah!!
   
 20. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #20
  Oct 7, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  1. Uache kukurupuka na kutangaza kuwa Mirungi ni madawa ya kulevya.
  Usiandike kitu ambacho huna uhakika wala ushahidi nacho.

  2. Hoja yako ya kusema eti ukiwa unakula Mrungi then unakunywa bia au Lique unakuwa hulewi mi naona kama ushuzi tu.
  So unataka kutuambia Mirungi isiliwe hapa nchini eti kisa ukinywa na pombe hulewi?
  Hii sheria peleka nyumbani kwako.

  3. Unapokuja na hoja kuwa Mirungi ikikutuma kuwa na mwanamke basi utamfuata umbali wowote na ikikutuma kutokuwa nae basi hutamtamani mwanamke yeyote mi napingana nayo.
  Kumfuata mwanamke umbali wowote sio tu ukila Mirungi.
  Hii inategemea mnapendana kiasi gani na mko na ukaribu gani.
  So hata mlevi anaweza kufunga safari akamfuata mwanamke wake mile kadhaa.
  So kwa hapo pia nakuona wewe saa mbovu tu.

  4. Unapoandika na kusema eti mlaji wa Mrungi akishaanza kutafuna tu basi anakuwa hana mpango wa kufanya kazi kwa siku hiyo nao ni uharo tu na wala sio hoja ya kupelekea mtu kukatazwa kula mrungi. Swali nalokuuliza je wakati wewe unakula Mirungi je uliwahi kula mirungi sambili asubuhi? Au umewahi kuona vijana au mijuve ya Kenya ikilaumiwa kwa kula mti wakati wa kazi?
  Au wewe uliwahi kuacha kufanya kazi na kula Mrungi tu?

  Then kwa kukupongeza tu ni kuwa hapo u pia walaji Mirungi hawana tabia za uasherati...thats good.
  Je unataka taifa lenye waasherati?
  Na madhara ya uasherati?
   
Loading...