Me nilisikia mtaa baba riz analipwa USD 2000 per year ambapo n mil 25 kwa mwez[/QUOTE]
??? Hujaeleweka mkuu.
Ivi na jakaya je?[/QUOTE
Inawezekana JK analipwa mshahara mkubwa ila si unajua kuwa viongozi wa TZ huwa hawapendi kutangaza kipato chao,
au umesahau kipindi kile Dr Slaa alipoamua kutangaza mshahara wake bungeni kila mbunge alitaka kummeza na kusema amekosea kuwa ni kwanini watz wajue kipato chao,,,
At least for the kenyan its known to the public how much Is kenyan PM siphoning. Informtion is knowledge....
So can u allocate your callories to get us information about the Salary and entittled benefits of our honorable PM and even President .?
Waiting to learn from your critical and analytical comment
- Do u know how much (financially) is allocated for Retired Mkapa, Mwinyi , Msuya Wariob, Lowasa?
- Do u know how much (finanacially) is allacted for family of Nyerere, Sokoine. Is it a right or its a favour?
Si wengi wanaofahamu kuwa kwa sasa wanasiasa wa Kenya wanalipwa mishahara minono kuliko nchi nyingi duniani. Bunge la Kenya liliridhia nyongeza ya mishahara ya wabunge na kuidhinisha kila mbunge kulipwa mshahara wa dola 126,000 kwa mwaka, sawa na Sh. 201 milioni au Sh. 16.8 milioni kwa mwezi.
Kiasi hicho cha mshahara, kina maana ya kiwango sawa na mshahara wa mbunge wa Marekani.
Bunge hilohilo ndilo lilipitisha mshahara wa Waziri Mkuu ambao unazidi ule anaolipwa Obama na Waziri Mkuu wa Uingereza. Aidha, wabunge wa Kenya, wamo katika harakati za kutaka mishahara yao isikatwe kodi.
Fikiria: Wakati kipato cha mwananchi wa Marekani kwa wastani ni dola 50,000 kwa mwaka (Sh. 80 milioni), kipato cha mwananchi wa kawaida wa Kenya kwa wastani ni dola 730 tu (Sh. 1.1 milioni) kwa mwaka au chini ya dola 2 kwa siku.
Lakini kwa nchi ambayo wanasiasa wake wanalipwa viwango sawa na wale wa Marekani, mtu angeweza kutarajia nchi hiyo ina miundombinu safi, huduma bora za jamii zikiwamo elimu, maji na afya bure, umeme kwa wingi na bei rahisi na kadhalika.
Wakati Kenya inajitanua kimatumizi kwa wanasiasa wake wakubwa, bado inategemea kusaidiwa na wafadhili kujaza pengo la bajeti yake ya kila mwaka ingawa kiwango cha ufadhili kinashuka mwaka hadi mwaka.
Kutokana na mishahara mikubwa kwa wanasiasa wa Kenya, mtu angetarajia kwamba hakuna haja tena kwao kuliibia taifa kupitia vitendo vya kifisadi. Wizi na ufisadi vimekuwa vitendo vilivyoshamiri katika sekta ya umma nchini humo.
HII HAPA NI ORODHA YA VIONGOZI WANAOLIPWA MISHAHARA MIKUBWA DUNIANI.
HIVI KWELI KENYA NI TAJIRI SANA KUIZIDI MAREKANI???????
- Lee Hsien Loong Waziri Mkuu wa Singapore: Dola 2,856,930 (Tsh 4.5bn) kwa mwaka.
- Donald Tsang Mtawala Mkuu wa Hong Kong ambayo sasa ni sehemu ya China: Dola 513,245 (Tsh 821m/-) kwa mwaka.
- Raila Odinga Waziri Mkuu wa Kenya: Dola 427,886 (TSh 684m/-) kwa mwaka.
- Barack Obama Rais wa Marekani: Dola 400,000 (Tsh 640m/-) kwa mwaka.
- Nicolas Sarkozy Rais wa Ufaransa Dola 345,423 (TSh 552.6m/-) kwa mwaka.
- Stephen Harper Waziri Mkuu wa Canada: Dola 296,400 (Tsh 474.2m/-) kwa mwaka.
- Mary McAleese Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Ireland: Dola 287,900 (Sh. 460.6 milioni) kwa mwaka.
- Julia Gillard Waziri Mkuu wa Australia: Dola 286,752 (Sh. 458.8 milioni) kwa mwaka.
- Angela Merkel Waziri Mkuu (Chancellor) wa Ujerumani: Dola 283,608 (Sh. 453.7 milioni) kwa mwaka.
- Naoto Kan Waziri Mkuu wa Japan: Dola 273,676 (Sh. 437.8 milioni) kwa mwaka.
- Jacob Zuma Rais wa Afrika ya Kusini: Dola 272,280 (Sh. 435.6 milioni) kwa mwaka.
- John Key Waziri Mkuu wa New Zealand: Dola 271,799 ( Tsh 434.8m/-) kwa mwaka.
- David Cameron Waziri Mkuu wa Uingereza: Dola 215,390 (Sh. 344.6 milioni) kwa mwaka.
- Ma Ying-jeu Rais wa Taiwan: Dola 184,200 (Sh. 294.7 milioni) kwa mwaka.
- Lee Myung-bak Rais wa Korea Kusini: dola 136,669 (Sh. 218.6 milioni) kwa mwaka.
uchumi wa kenya unaruhusu. Pia wanasiasa madharan wa kenya wanawajibika sana. Mbona hujasema kima cha chini? Ambao huwa karibu laki tano za kibongo. Hawa ni kada ya chn ktk utumish wa umma. Shortly jamaa wako fit uchumi unaruhusu
hacha tu hiyo ya kuruhusu wameweka wazi, kwa hiyo kama kuna mwenye hoja kama mwananchi wa kenya anaweza kuitoa
sasa hapa kwetu hata ya wabunge haturuhusiwi kujua, waraisi ndio kabisa usalama wa taifa
kwa hapa nasema kenya hoye
tuna mengi ya kuiga kutoka kenya
nimeongea na mzee mmoja aliyekua IKULU anasema raisi wetu anachukua zaidi ya nusu ya hela inayotengwa kama bajeti ya IKULU
in fact posho na mengineyo ndio utajiri wa maraisi wetu, wanalipwa hela chafu na haina limit wala wa kuuliza hiyo hela imekwenda wapi ni matumizi yake, na yako clissfied kama NATIONAL SECURITY