Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Kwa walioangalia protokali jana wakati wa siku kuu ya Uhuru waliona kuwa baada ya Rais na Makamu wake aliyefuatia kuingia au kutoka alikuwa ni Rais wa Zanzibar; ambaye naye alifuatiwa na Waziri Mkuu na nyuma yake walifuatia Makamu wawili wa Zanzibar. Lakini kilichonitatiza ni hicho cha Rais wa Zanzibar na Waziri Mkuu wa Muungano.
Kwanza kwa sababu wakija kwenye Baraza la Mawaziri RAis wa Zanzibar ni mjumbe na hana uwezo wa kukiendesha wakati kama Rais au Makamu hayupo Waziri Mkuu ndio anaweza kusimamia kikao cha baraza hilo.
Kama hili ni kweli kwanini Waziri Mkuu wa Muungano aje nyuma ya Rais wa Zanzibar? Proper Protocal ilitakiwa iwe:
Unaanza na viongozi wakuu wa Muungano
Rais
Makamu
Waziri Mkuu
Jaji Mkuu
Spika
Viongozi wa Zanzibar
Rais wa Zanzibar
Makamu wa kwanza
Makamu wa pili
Jaji Mkuu
Spika
Shilingi zangu mbili hizo au nakosea wapi?