Waziri Mkuu wa JMT na Rais wa Zanzibar nani yuko juu na kwanini?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,987
Kwa walioangalia protokali jana wakati wa siku kuu ya Uhuru waliona kuwa baada ya Rais na Makamu wake aliyefuatia kuingia au kutoka alikuwa ni Rais wa Zanzibar; ambaye naye alifuatiwa na Waziri Mkuu na nyuma yake walifuatia Makamu wawili wa Zanzibar. Lakini kilichonitatiza ni hicho cha Rais wa Zanzibar na Waziri Mkuu wa Muungano.

Kwanza kwa sababu wakija kwenye Baraza la Mawaziri RAis wa Zanzibar ni mjumbe na hana uwezo wa kukiendesha wakati kama Rais au Makamu hayupo Waziri Mkuu ndio anaweza kusimamia kikao cha baraza hilo.

Kama hili ni kweli kwanini Waziri Mkuu wa Muungano aje nyuma ya Rais wa Zanzibar? Proper Protocal ilitakiwa iwe:

Unaanza na viongozi wakuu wa Muungano
Rais
Makamu
Waziri Mkuu
Jaji Mkuu
Spika

Viongozi wa Zanzibar
Rais wa Zanzibar
Makamu wa kwanza
Makamu wa pili
Jaji Mkuu
Spika

Shilingi zangu mbili hizo au nakosea wapi?
 
Mkuu tuko pamoja naamini kabisa Rais wa Zanzibar ndani ya katiba ya sasa ya JMT uzito wake ni sawa na waziri yoyote wa JMT nashangaa itifaki haieshimiwi kabisa.Itifaki pia haizingatiwi zinapofanyika shughuli Zanzibar unakuta Rais wa JMT anakuwa chini ya Rais wa Zanzibar.
 
Hili jambo hata mimi linanitatiza,sina hakika kama hawa jamaa wa Itifaki wanafanya bahati mbaya au ni kwamba 'mazingira' yanawalazimisha..
Au labda kuna 'makubaliano' yoyote kuhusu hili..
 
Mkuu hii nchi yetu inaitwa Tanzania. Ina vijimambo vingi tu vya hovyohovyo kabisa na hili ni moja ya jambo la hovyo kati ya mengi tuliyonayo. Viongozi wetu wengine na hata watu wa protocal akili nadhani zimesha-expire kwa hiyo lolote laweza kutendeka hapa. Siku nyingine Bi Salma ataingia kabla ya makamu ya Rais na hakuna atakayehoji.
 
Sisi Watanganyika ni kichwa cha mwendawazimu na hiyo protokli inabadilisha kila kamati ya usluhishi ya muungano inapokaa halafu wananchi hatuambiwi kweli tumegeuzwa madebe matupu
 
Kwa walioangalia protokali jana wakati wa siku kuu ya Uhuru waliona kuwa baada ya Rais na Makamu wake aliyefuatia kuingia au kutoka alikuwa ni Rais wa Zanzibar; ambaye naye alifuatiwa na Waziri Mkuu na nyuma yake walifuatia Makamu wawili wa Zanzibar. Lakini kilichonitatiza ni hicho cha Rais wa Zanzibar na Waziri Mkuu wa Muungano.

Kwanza kwa sababu wakija kwenye Baraza la Mawaziri RAis wa Zanzibar ni mjumbe na hana uwezo wa kukiendesha wakati kama Rais au Makamu hayupo Waziri Mkuu ndio anaweza kusimamia kikao cha baraza hilo.

Kama hili ni kweli kwanini Waziri Mkuu wa Muungano aje nyuma ya Rais wa Zanzibar? Proper Protocal ilitakiwa iwe:

Unaanza na viongozi wakuu wa Muungano
Rais
Makamu
Waziri Mkuu
Jaji Mkuu
Spika

Viongozi wa Zanzibar
Rais wa Zanzibar
Makamu wa kwanza
Makamu wa pili
Jaji Mkuu
Spika

Shilingi zangu mbili hizo au nakosea wapi?

Hii nayo ni kero ya Muungano??? hivi Mtoto wa Mkulima akiamua kutoka baada ya Mkwere na kabla ya Dr. Shein atachukuliwa hatua za ki/sheria/nidhamu?...
 
JK ana-compromise sana na Wazanzibari na kusahau hata mambo mengine:: Sifahamu ki-mantiki (Shein, Seif M, Seif) walikuwa na nafasi gani kwenye Maadhimisho ya Uhuru wa Tanganyika? Wageni waalikwa? au?
 
JK ana-compromise sana na Wazanzibari na kusahau hata mambo mengine:: Sifahamu ki-mantiki (Shein, Seif M, Seif) walikuwa na nafasi gani kwenye Maadhimisho ya Uhuru wa Tanganyika? Wageni waalikwa? au?

Aiseee! Baba_Enock umefikiria vema kabisa. Tulisherehekea Uhru wa Tanganyika sio wa Tanzania. Nchi yetu tunaelekea kupotosha historia yetu! Ati Uhuru wa Tanzania! pambafu....1961 hakukuwepo na nchi inaitwa Tanzania...tulikuwa Tanganyika
 
Kwa walioangalia protokali jana wakati wa siku kuu ya Uhuru waliona kuwa baada ya Rais na Makamu wake aliyefuatia kuingia au kutoka alikuwa ni Rais wa Zanzibar; ambaye naye alifuatiwa na Waziri Mkuu na nyuma yake walifuatia Makamu wawili wa Zanzibar. Lakini kilichonitatiza ni hicho cha Rais wa Zanzibar na Waziri Mkuu wa Muungano.

Kwanza kwa sababu wakija kwenye Baraza la Mawaziri RAis wa Zanzibar ni mjumbe na hana uwezo wa kukiendesha wakati kama Rais au Makamu hayupo Waziri Mkuu ndio anaweza kusimamia kikao cha baraza hilo.

Kama hili ni kweli kwanini Waziri Mkuu wa Muungano aje nyuma ya Rais wa Zanzibar? Proper Protocal ilitakiwa iwe:

Unaanza na viongozi wakuu wa Muungano
Rais
Makamu
Waziri Mkuu
Jaji Mkuu
Spika

Viongozi wa Zanzibar
Rais wa Zanzibar
Makamu wa kwanza
Makamu wa pili
Jaji Mkuu
Spika

Shilingi zangu mbili hizo au nakosea wapi?

Mzee Mwanakijiji niambie,

Rais na waziri cheo kipi kipo juu ?
Anyway,
Mabadiliko yale ya katiba yaliyomuondolea Rais wa Zanzibar, Umakamu rais ndiyo yanazaa masuali kama haya. Ujanja mwingi ,mbele kiza. Huo ni muendelezo tu wa mkorogo unaofanywa na CCM na kutuumiza sisi vichwa.

Kama unashangaa hapo, siku ya Sherehe za Mapinduzi kule Zenj, Rais wa Zanzibar anaingia mwisho na anatoka Mwanzo. Rais wa Muungano anaingia kumsubiri Rais wa Zenj na anabaki jukwaani hadi pale Rais wa Zenj ameondoka uwanjani.

That happens only in Tanzania ! Made in Tanzania.
Tutashangaa sana. Bora zitie mfukoni shilingi zako mbili wajanja wasije wakaziyeyusha.

Unakumbuka pale mwalimu alipomwambia mjumbe mmoja kaa chini?
Huyu mjumbe alikuwa anaulizia usahihi wa kapu kuu, alisema hilo halikuwepo katika kanuni za CCM wakati huo.The guy was right but Mwalimu aliamua kum-shut him down. Akamwambia, "mwenyekiti akizungumza tia kitabu chako cha kanuni katika dust bin" Ubabe tu.

Kwa hiyo, usishangae mazingaombwe ya CCM na protokali zao!
 
Nadhani hakuna swali. Namaanisha ni vitu visivyofanana kwa uasilia wake. Mfano ni hivi moja ni kimiminika (liquid) na nyingine ni ngumu (solid). Sasa ukitaka kutumia mizani wale vimiminika watasema unawadhulumu. Ukigeuka tubes etc wale wagumu nao watakataa kwa vile haitawatendea haki. Kwa sasa huwezi kupata jibu, or at least a balanced answer. It's teribbly messed up u know.

So leave it for now, get a new proper Constitution then remind us and we'll sit and talk more.
 
Mbona hiyo protokali iliyofuatwa kwenye sherehe ina precedent kwenye katiba tayari, hivyo hivyo.
 
QUOTE=TzPride; Tulisherehekea Uhuru wa Tanganyika sio wa Tanzania.

Umenena vyema. Ila tunasheherekeaje uhuru wa nchi ambayo haiexist!? i.e. it's an abstract nation! Nini mantiki hapo?
 
Zanzibar ni nchi......sasa kwa nini tuumize vichwa kwa kuangalia nani mkubwa kati ya rais wa nchi kamili na waziri mkuu wa nchi ambayo ina rais pia?...............zanzibar kwa mujibu wa katiba yao ya sasa na ambayo viongozi wetu wa wadhaifu wa muungano wamekaa kimya si sehemu tena ya muungano bali nchi kamili...........
 
Kama hili ni kweli kwanini Waziri Mkuu wa Muungano aje nyuma ya Rais wa Zanzibar? Proper Protocal ilitakiwa iwe:

Unaanza na viongozi wakuu wa Muungano
Rais
Makamu
Waziri Mkuu
Jaji Mkuu
Spika

na mawaziri wengine wote
 
MMKJ umenena vyema. Kwakweli kuna mkanganyiko katika izo protokali. Kwasababu hata hao makamu 2 wa zenj kwny protokali za kikatiba hawapo. Kimsingi hao hawakupaswa kuingia kwa protokali siku iyo. Wangeenda kama wageni wa kawaida,ila usingizi wa waTZ ni mnono kiasi kwamba wengi wao hawakuona tatizo lolote.
 
Zanzibar ni nchi......sasa kwa nini tuumize vichwa kwa kuangalia nani mkubwa kati ya rais wa nchi kamili na waziri mkuu wa nchi ambayo ina rais pia?...............zanzibar kwa mujibu wa katiba yao ya sasa na ambayo viongozi wetu wa wadhaifu wa muungano wamekaa kimya si sehemu tena ya muungano bali nchi kamili...........

Hivi zanizar kwa katiba ya sasa imeungana na nani?.......Ukimuuliza Mwanasheria Mkuu atakwambia hajui... nidhamu ya woga
 
MMKJ umenena vyema. Kwakweli kuna mkanganyiko katika izo protokali. Kwasababu hata hao makamu 2 wa zenj kwny protokali za kikatiba hawapo. Kimsingi hao hawakupaswa kuingia kwa protokali siku iyo. Wangeenda kama wageni wa kawaida,ila usingizi wa waTZ ni mnono kiasi kwamba wengi wao hawakuona tatizo lolote.

Hivi hizo protocal nani anaandaaaa? lazima atakuwa kilaza sana
 
Mi naona ni sawa kabisa Raisi wa Zanzibar kumtangulia Waziri mkuu kwa kuwa. Waziri mkuu ni wa Tanzania bara (Tanganyika) zaidi kuliko kwenye muungano. Hivyo kimadaraka yupo chini ya raisi wa Zanzibar
 
Back
Top Bottom