Waziri Mkuu wa Italia katika Zengwe Jipya na Binti wa Miaka 18 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Mkuu wa Italia katika Zengwe Jipya na Binti wa Miaka 18

Discussion in 'International Forum' started by Pdidy, May 24, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  May 24, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,606
  Likes Received: 5,781
  Trophy Points: 280
  Waziri Mkuu wa Italia katika Zengwe Jipya na Binti wa Miaka 18

  [​IMG]
  Sunday, May 24, 2009 6:58 AM

  Waziri mkuu wa Italia, Silvio Berlusconi ameingia kwenye zengwe jingine baada ya picha zake mpya akiwa na msichana wa miaka 18 aliyesababisha ndoa yake ivunjike kuchapishwa kwenye magazeti ya Italia. Picha zinazomwonyesha waziri mkuu wa Italia, Silvio Berlusconi akiwa na mrembo Noemi Letizia, binti wa miaka 18 ambaye inasemekana ndiye aliyechangia kwa kiasi kikubwa kuvunjika kwa ndoa yake zilichapishwa kwenye gazeti la La Repubblica la Italia.

  Picha hizo zilipigwa katika party ya krismasi ambayo Berlusconi aliwaandalia wachezaji wa timu yake ya AC Milan anayoimiliki.

  Gazeti hilo lilichapisha picha na video kwenye tovuti yake zikimwonyesha Letizia akiwa kwenye party hiyo pamoja na mama yake.

  Maswali mengi yamezuka baada ya kuchapishwa kwa picha hizo, watu wakihoji msichana huyo ambaye alikuwa hajulikani wala hahusiki na chochote na AC Milan alikuwa amefuata nini kwenye party hiyo?.

  Picha hizo mpya zinasemekana zitazidisha hasira za mke wa Berlusconi Veronica Lario ambaye aliomba talaka yake mwezi uliopita baada ya Berlusconi kuhudhuria sherehe ya kuzaliwa na kutimiza miaka 18 ya Letizia na kumzawadia kidani cha almasi chenye thamani ya dola 8,300.

  Mke huyo wa waziri mkuu alisema wakati akidai talaka yake kwamba Berlusconi alihudhuria sherehe ya kuzaliwa ya Letizia wakati sherehe za watoto wake mwenyewe hajawahi kuhudhuria hata moja.

  "Siwezi kuwa na mwanaume ambaye muda wote anapenda kuwa na wasichana wadogo" alisema mke huyo Berlusconi.

  Gazeti la La Repubblica ambalo linajulikana kwa upinzani wake na Berlusconi liliuliza swali moja tu kuhusiana na picha hizo "Noemi Letizia alifuata nini kwenye sherehe za AC MIlan?".
   
 2. g

  grandpa Senior Member

  #2
  May 24, 2009
  Joined: Aug 24, 2008
  Messages: 185
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wanauliza jibu. Of course alifuata dudu!
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  May 25, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Granpa asante kwa jibu zuri
   
 4. u

  urithiwetu Senior Member

  #4
  May 25, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 103
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Fataki!
   
Loading...