Waziri Mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu ataka miito ya ibada misikitini (Adhana) kupunguza kelele

amygdala

JF-Expert Member
Jul 11, 2016
1,082
997
_92427479_f36295a7-3f32-415a-be72-67d9b869b229.jpg

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anaunga mkono pendekezo la kupunguza sauti za wito wa ibada 'adhan', akisema kuwa amepokea malalamishi ya kelele.

Baadaye siku ya jumapili kamati ya serikali itajadili mswada ulio na mpango huo.

Vyombo vya habari vya Israel vinasema kuwa mikakati hiyo itazuia misikiti kutotumia vipaza sauti mara tano kwa siku ili kuwaita wafuasi wa dini hiyo kufanya ibada.

Wakosoaji wanasema hatua hiyo itakuwa ya ukadamizaji.

Sheria hiyo itaathiri dini zote lakini itatumika sana miongoni mwa wito wa ibada miongoni mwa waislamu au 'adhan'.

Adhan ya kwanza hufanyika mapema alfajiri huku ya mwisho ikifanyika baada ya jua kutua.

Takriban asilimia 17.5 ya raia wanaoishi Israel ni Waarabu na wengi wao ni Waislamu.

Netanyahu ataka sauti za 'adhan' kupunguzwa misikitini - BBC Swahili
 
Yetu macho. Mji unaoongoza zaidi kwa kelele za adhana duniani ni Dhaka, Bangladesh.
 
Hakuna shida,sasa hivi technology imekuwa sana wanaweza kuwafungia waumini wao vifaa maalumu mara muda wa adhana unapowadia mambo ya kuwaita watu wasiohusika ni mambo ya kizamani sana.

Wakati wa Mtume Mohamed SAW hapakuwepo na vipaza sauti,kadri muda ulivyokwenda vipaza sauti vilichukua nafasi kubwa sasa tuko karne ya 21 waislam wanaweza kuweka access katika simu zao muda wa adhana unafika automatic wanapata ujumbe,hii isiwe Israel tu hata huku Tanzania tuanze kufukiri hili jambo.
 
Serikali ya Israel ipo mbioni kupeleka Muswada bungeni kutunga sheria itakayo itaka misikiti yote nchini Israel kupunguza sauti ya miito ya ibada (Adhana).

Hii imetokana na bwana Netanyahu kupata malalamiko kwamba miito hio imekua ikisababisha kelele kwa wananchi wengine wasio waislam.

Chanzo: BBC Swahili
 
Serikali ya Israel ipo mbioni kupeleka Muswada bungeni kutunga sheria itakayo itaka misikiti yote nchini Israel kupunguza sauti ya miito ya ibada(Adhana).
Hii imetokana na bwana Netanyahu kupata malalamiko kwamba miito hio imekua ikisababisha kelele kwa wananchi wengine wasio waislam.
Chanzo:BBC Swahili
Sheria ya noise pollution itaondoa hisia za ubaguzi wa kidini
 
Serikali ya Israel ipo mbioni kupeleka Muswada bungeni kutunga sheria itakayo itaka misikiti yote nchini Israel kupunguza sauti ya miito ya ibada(Adhana).
Hii imetokana na bwana Netanyahu kupata malalamiko kwamba miito hio imekua ikisababisha kelele kwa wananchi wengine wasio waislam.
Chanzo:BBC Swahili
Safi sana
 
Back
Top Bottom