Wakuu zangu naomba tujadili hii safari ya waziri mkuu wa Canada, Mheshimiwa Harper ambaye atatua nchini muda wowote itakuwa na manufaa gani kwetu na pia tujadili ni jinsi gani ujumbe wetu unaweza kumfikia..
Unajua binafsi yangu sielewi kabisa kama viongozi wetu wanajua walichokifanya na kwa faida ya Tanzania ama watanzania kwa sababu Mkataba wowote unaolinda Kampuni za Nje kwa kutumia sheria za nje unatuweka mahala pabaya sana. Special treatment kwa mashirika haya ni kukubali kukoloniwa - Ukoloni mamboleo.Mkuu Mkandara umeanzisha mada muhimu sana bahati mbaya vyama vya upinzani [mbadala] badala ya kuifanyia kazi ziara ya Mheshimiwa Harper utashangaa watakuwa na muda malumbano na RPC wa Iringa ambaye tunaye kila siku.
Ipo haja ya kuandaa maandamano makubwa ya kulaani makampuni ya Canada yanayoshirikiana na wanasiasa wezi atakapotua J N Airport.Nategemea pia kurugenzi ya mambo ya nje ya vyama vyote vya siasa makini watandaa waraka unaoelezea ufisadi wa makampuni yote ya Canada na kuukabidhi kwa Mheshimiwa Harper.
Nakala Ritz Mwita Maranya jmushi1 FJM na wengine.
Ningependa sana kuelewa ni mashirika gani yana import coffee, tea na cashews kutoka Tanzania maana sijawahi kuona hata kitu kimoja kimeandikwa made in Tanzania wakati mimi ni mtumiaji mkubwa wa vitu hivyo.Canada's main exports to Tanzania, amounting to $61.5 million in 2011, consisted primarily of used clothing, machinery, and wheat. Canadian imports from Tanzania amounted to $5.3 million, comprising mainly coffee, tea, and cashews. In July 2003, Canada and Tanzania signed an agreement to permit duty-free access for almost all goods produced in Tanzania.
Canada - Tanzania Relations