Waziri Mkuu: Vijana wamekopeshwa Shilingi Bilioni 1.88

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesema serikali kupitia mfuko wa maendeleo ya vijana imetoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 1.88 kwa ajili ya kuwezesha miradi 85 ya vijana katika sekta za kilimo, viwanda na biashara kwenye halmashauri 28.

Ft15xTfWYAIeFxE.jpg

Ameyasema hayo Aprili 16, 2023, wakati akizindua mradi wa kuwezesha vijana kielimu na kiuchumi kupitia KCB 2jiari wa KCB Foundation na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Ujerumani (GIZ), katika ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

“Ni ukweli usiopingika kuwa suala la uwezeshaji wa vijana ni muhimu katika kukuza uchumi, hii ni kutokana na ukweli kwamba vijana ni nguvu kazi inayotegemewa na ni kundi kubwa katika nchi yetu, kwa msingi huo maendeleo yetu yanategemea sana vijana kwani hili ni kundi kubwa na muhimu lenye umri wa kufanya kazi, wingi wa vijana wenye ujuzi, ni chachu ya kuharakisha maendeleo endelevu," amesema Waziri Mkuu

Ft15xTdWIAAWC7G.jpg

Waziri Mkuu amesema kuwa serikali itaendelea kushirikiana na wadau wote zikiwemo taasisi za kifedha, mashirika ya kimataifa na sekta binafsi katika kujenga nguv ukazi yenye ujuzi itakayoshiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya Taifa.

"Serikali kwa upande wake inaendelea kutekeleza mikakati na programu mbalimbali za uwezeshaji wa vijana ili kuhakikisha wananchi wanaendelea kuwekewa mazingira mazuri na wezeshi ya kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo," ameongeza.

Chanzo: Ofisi ya Waziri Mkuu
 
Tutasikia kila njia za upigaji
Hata tukiomba orodha tutapewa Ile ya wapiga kura

Yaani wanapiga cha juu kila kona
 
Shilingi bilioni 1.88 bado ni pesa ndogo sana PM kujinadi kwenye public kwamba serikali imekopesa vijana ukilinganisha na uhitaji.
 
Ni haohao kwani haya mambo
Vijana Gani Hao UVCCM?
Huwa yanafanywa kwa usiri mkubwa sana ndani ya ofisi za CCM, nami nimemsikia japo sikuelewa slipomshukuru rais Samia kwakutoa hizo pesa huku mwisho akiishukuru KCB na GIZ kwa kutoa hizo pesa!
 
Ni haohao kwani haya mambo

Huwa yanafanywa kwa usiri mkubwa sana ndani ya ofisi za CCM, nami nimemsikia japo sikuelewa slipomshukuru rais Samia kwakutoa hizo pesa huku mwisho akiishukuru KCB na GIZ kwa kutoa hizo pesa!
Nan katoa hizo pesa kcb a; giz au serikali?
 
Ni haohao kwani haya mambo

Huwa yanafanywa kwa usiri mkubwa sana ndani ya ofisi za CCM, nami nimemsikia japo sikuelewa slipomshukuru rais Samia kwakutoa hizo pesa huku mwisho akiishukuru KCB na GIZ kwa kutoa hizo pesa!
Alafu Hatujui sisi Kama Tz kupitia wanaoitwa vijana Wanaipa Nini KCB na GIZ?

Mana Wanaweza Lipwa Tanzanite Ya Watanzania Wote Kwa Manufaa Ya UVCCM.

Kupata Mkopo HALMASHAURI/SIJUI WAPI Bila Konekshen Ni Kipengele Mana Hawapigi Filimbi Ya Kuwakusanya Ili Kuwapa Taarifa Vijana
 
Back
Top Bottom