Waziri mkuu Uturuki asema Israel ni magaidi

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
0
Waziri mkuu Uturuki asema Israel ni magaidi | Matukio ya Kisiasa | DW.DE | 19.11.2012

IDHAA YA KISWAHILI/Matukio ya Kisiasa

[h=4]Matukio ya Kisiasa[/h][h=2][/h]

Waziri mkuu wa Uturuki ameitaja Israel kuwa ni taifa la ugaidi kutokana na mashambulizi yake dhidi ya ukanda wa Gaza, katika matamshi ambayo yameashiria uhasama wa wazi kwa mshirika huyo wa zamani wa Uturuki.
Matamshi ya Waziri Mkuu huyo Racep Tayyip Erdogan yamekuja baada ya karibu wiki nzima ya mashmabulizi ya roketi kutoka Palestina kwenda Israel na mashambulizi ya angani dhidi ya ukanda wa Gaza. Erdogan aliuambia mkutano wa baraza la Waislamu wa Ulaya na Asia unaofanyika mjini Instanbul kuwa wale wanaouhusisha Uislamu na ugaidi huwa wanafumba macho mbele ya mauaji ya halaiki dhidi ya Waislamu, na kugeuza vichwa vyao huku watoto wanauawa mjini Gaza. " Kwa sababu hii, nasema Israel ni taifa la kigaidi na matendo yake ni matendo ya kigaidi," amesema Erdogan.
Vifaru vya Israel vikiwa tayari kwa mashambulizi dhidi ya Gaza.
Watu 10 wa familia moja waliyouawa wazikwa
Wakati waziri mkuu erdogan akiyasema hayo mjini, Gaza maefu ya watu wamekusanyika kufanya mazishi ya watoto waliouawa katika shambulio moja jana Jumapili. Familia ya Dalu ilipoteza watu 10 pale shambulio la Israel lilipoilenga nyumba yao na kuauwa pamoja na mama yao na bibi yao. Israel imesema iliishambulia nyumba hiyo kwa sababu kuliwepo na kamanda moja wa kundi la Hamas.
Hala Al-Ash alikuwa nyumbani katika jengo la jirani wakati shambulio hilo likitokea. "Maneno hayatoshi kuelezea nini kilitokea kwa sababu raia wa kawaida walikuwa nyumbani wamekaa na ghafla. bila hata onyo wanashambulia nyumba. Lilikuwa ni shambulio baya sana na hii ndiyo tabia ya waisrael, mashambulio yao yanawalenga raia, sisi siyo wanajeshi sisi ni raia tu, ni kumbukumbu mbaya unapowaangalia wahanga, ni jambo ambalo halisahauliki," alisema msichana huyo mwenye umri wa miaka 16.
Raia wa Palestina wakiyakimbia makaazi yao baada ya mashambulizi y Israel.
Kiongozi wa kisiasa wa Hamas aliyeko uhamishoni Khalid Meshaal amewataka wapalestina kuacha tofauti zao na kuionya Israel kuwa itagundua kuwa ilifanya makosa kama itaanzisha mashambulizi ya ardhini. Meshaal alisema ni juu ya Israel kusitisha vurugu katika ukanda wa Gaza kwa sababu wao ndiyo waliyoanzisha vurugu hizo. Meshaal amekiri kuwa mauaji ya kiongozi wa tawi la kijeshi la chama hicho wiki iliyopita lilikuwa ni pigo kubwa, lakini akaongeza kuwa morali ya wapiganaji wa Hamas imeongezeka.
Hamas, Fatah wawa kitu kimoja
Na mjini Ramallah, Afisa mwandamizi wa chama cha Fatah, Jibril Rajoub ameuambia mkusanyiko wa watu karibu elfu moja waliyokusanyika kufanya maandamano kuonyesha mshikamano na wenzao wa Gaza, kuwa kuanzia sasa wametangaza kumaliza tofauti zao. Miongoni mwa waliohudhuria maandamano hayo ni pamoja na viongozi wa juu wa Hamas katika ukanda wa Magharibi, na maafisa wa kundi la Islamic Jihad.
Moshi ukitanda katika anga ya Gaza kufuatia shambulio la Israel.
Huku mashambulizi yakizidi na matumaini ya kusitishwa kwakwe yakiwa madogo sana, waziri mkuu wa Misri Hisham Qandil amesema katika mahojiano na shirika la habari la Reuters amesema juhudi za kusitisha mapigano zinaendelea na kwamba makubaliano yanaweza kufikiwa muda wowote, akiongeza kuwa majadiliano ya namna hii ni magumu kutabirika. Israel imesisitiza kuwa mashambulizi yatasimama tu pale mashambulizi ya roketi yatakapositishwa.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel naye alitoa wito wa kusitisha mashambulizi wakati waziri wake wa mambo ya kigeni, Guido Westerwelle akielekea mjini Tel Aviv. Merkel alielezea hofu kuwa kuendelea kwa mgogoro huo kunaweza kuchochea uvunjifu wa amani katika mashariki ya kati.
Mwandishi: Iddi Ismail Ssessanga/dpae, rtre,afpe
Mhariri: Saum Yusuf Ramadhan
 
kamili

JF-Expert Member
Feb 10, 2011
1,007
2,000
Binafsi simwamini Racep Tayyip Erdogan alichosema ni unafiki tu. Kwa sababu kama anaamini alichosema kwanini asiende kukisemea UN? Au kwa nini asiwaambie Israel wenyewe badala yake anaenda kukisema mahali ambapo hapana athari yoyote. Itakumbukwa Uturuki ni mwanachama wa jumuiya ya ulaya na hata NATO, kama hivyo ndivyo anaweza kwenda kunyume na misimamo ya mataifa ya ulaya ambayo yanatoa baraka kwa Israel kuua inavyotaka huku wapelestina wakiwa hawana ruhusa ya kupata silaha kutoka mahali popote duniani, na tena njia zote za kuingilia Gaza za Ardhini, baharini na angani zikiwa zinazibitiwa na Israel? Israel imefanya mauaji mengi na kwa muda mrefu alikuwa wapi muda wote huo? Mataifa ya Magharibi yanachoamini ni kuwa Mpalestina akiua ni ugaidi lakini Israel akiua ni haki yake na inakubaliwa hata na Mungu. Ni vigumu sana mtu ambaye wazazi wake na wadogo wake waliuawa mbele yake na nyumba yako kusagwa sagwa na kuachwa hohe hahe maskini halafu abaki ametulia tulii.....

Waziri mkuu Uturuki asema Israel ni magaidi | Matukio ya Kisiasa | DW.DE | 19.11.2012

IDHAA YA KISWAHILI/Matukio ya Kisiasa

Matukio ya KisiasaWaziri mkuu wa Uturuki ameitaja Israel kuwa ni taifa la ugaidi kutokana na mashambulizi yake dhidi ya ukanda wa Gaza, katika matamshi ambayo yameashiria uhasama wa wazi kwa mshirika huyo wa zamani wa Uturuki.
Matamshi ya Waziri Mkuu huyo Racep Tayyip Erdogan yamekuja baada ya karibu wiki nzima ya mashmabulizi ya roketi kutoka Palestina kwenda Israel na mashambulizi ya angani dhidi ya ukanda wa Gaza. Erdogan aliuambia mkutano wa baraza la Waislamu wa Ulaya na Asia unaofanyika mjini Instanbul kuwa wale wanaouhusisha Uislamu na ugaidi huwa wanafumba macho mbele ya mauaji ya halaiki dhidi ya Waislamu, na kugeuza vichwa vyao huku watoto wanauawa mjini Gaza. " Kwa sababu hii, nasema Israel ni taifa la kigaidi na matendo yake ni matendo ya kigaidi," amesema Erdogan.
Vifaru vya Israel vikiwa tayari kwa mashambulizi dhidi ya Gaza.
Watu 10 wa familia moja waliyouawa wazikwa
Wakati waziri mkuu erdogan akiyasema hayo mjini, Gaza maefu ya watu wamekusanyika kufanya mazishi ya watoto waliouawa katika shambulio moja jana Jumapili. Familia ya Dalu ilipoteza watu 10 pale shambulio la Israel lilipoilenga nyumba yao na kuauwa pamoja na mama yao na bibi yao. Israel imesema iliishambulia nyumba hiyo kwa sababu kuliwepo na kamanda moja wa kundi la Hamas.
Hala Al-Ash alikuwa nyumbani katika jengo la jirani wakati shambulio hilo likitokea. "Maneno hayatoshi kuelezea nini kilitokea kwa sababu raia wa kawaida walikuwa nyumbani wamekaa na ghafla. bila hata onyo wanashambulia nyumba. Lilikuwa ni shambulio baya sana na hii ndiyo tabia ya waisrael, mashambulio yao yanawalenga raia, sisi siyo wanajeshi sisi ni raia tu, ni kumbukumbu mbaya unapowaangalia wahanga, ni jambo ambalo halisahauliki," alisema msichana huyo mwenye umri wa miaka 16.
Raia wa Palestina wakiyakimbia makaazi yao baada ya mashambulizi y Israel.
Kiongozi wa kisiasa wa Hamas aliyeko uhamishoni Khalid Meshaal amewataka wapalestina kuacha tofauti zao na kuionya Israel kuwa itagundua kuwa ilifanya makosa kama itaanzisha mashambulizi ya ardhini. Meshaal alisema ni juu ya Israel kusitisha vurugu katika ukanda wa Gaza kwa sababu wao ndiyo waliyoanzisha vurugu hizo. Meshaal amekiri kuwa mauaji ya kiongozi wa tawi la kijeshi la chama hicho wiki iliyopita lilikuwa ni pigo kubwa, lakini akaongeza kuwa morali ya wapiganaji wa Hamas imeongezeka.
Hamas, Fatah wawa kitu kimoja
Na mjini Ramallah, Afisa mwandamizi wa chama cha Fatah, Jibril Rajoub ameuambia mkusanyiko wa watu karibu elfu moja waliyokusanyika kufanya maandamano kuonyesha mshikamano na wenzao wa Gaza, kuwa kuanzia sasa wametangaza kumaliza tofauti zao. Miongoni mwa waliohudhuria maandamano hayo ni pamoja na viongozi wa juu wa Hamas katika ukanda wa Magharibi, na maafisa wa kundi la Islamic Jihad.
Moshi ukitanda katika anga ya Gaza kufuatia shambulio la Israel.
Huku mashambulizi yakizidi na matumaini ya kusitishwa kwakwe yakiwa madogo sana, waziri mkuu wa Misri Hisham Qandil amesema katika mahojiano na shirika la habari la Reuters amesema juhudi za kusitisha mapigano zinaendelea na kwamba makubaliano yanaweza kufikiwa muda wowote, akiongeza kuwa majadiliano ya namna hii ni magumu kutabirika. Israel imesisitiza kuwa mashambulizi yatasimama tu pale mashambulizi ya roketi yatakapositishwa.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel naye alitoa wito wa kusitisha mashambulizi wakati waziri wake wa mambo ya kigeni, Guido Westerwelle akielekea mjini Tel Aviv. Merkel alielezea hofu kuwa kuendelea kwa mgogoro huo kunaweza kuchochea uvunjifu wa amani katika mashariki ya kati.
Mwandishi: Iddi Ismail Ssessanga/dpae, rtre,afpe
Mhariri: Saum Yusuf Ramadhan
 
Hute

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,559
2,000
anahangaika tu huyo, ana la kuifanya israel? udini utammaliza. bora afyate mkia, na kwa kufanya hivyo ndo hawatapata nafasi EU kabisa...ndo maana wamewasaliti hata waislam wenzao kwa nia ya kujibembeleza wawepo kwenye EU...hopeless
 
Top Bottom